
Kwa mujibu wa Beda Msimbe ambaye ni mmoja kati ya watoto 6 wa Mzee Luwanda,aliewahi kuwa mtangazaji wa zamani wa Radio Tanzania ambaye alistaafu kazi hiyo mwanzoni mwa miaka ya 1990 alikuwa amelazwa katika hospitali ya Muhimbili akisumbuliwa na kisukari huku akifanyiwa uchunguzi wa kansa ya kibofu cha mkojo.
Mtoto wake huyo alisema kwamba madaktari walimwambia kwamba baba yake alikufa kutokana na ugonjwa wa uti wa mgongo.
Mzee Luwanda ambaye atakumbukwa zaidi na watu wa vikundi vya sanaa kwa uandalizi wa michezo ya kuigiza ya radio.
Mara baada ya kustaafu Marehemu Mzee Luwanda alikuwa anaishi katika kijiji cha Goba akilima bustani na kufuga mifugo.
Mipango ya mazishi inafanyika nyumbani kwake Goba kijijini na anatarajiwa kuzikwa siku ya Jumamosi wiki hii.
Mungu aiweke Roho ya Marehemu Mahala pema Peponi.
- Ameen
pole beda msimbe.
ReplyDeletePole sana Beda.Tunamuomba Mwenyezi Mungu ailaze roho ya Mzee mahali pema peponi.
ReplyDeleteRIP sekulu Luanda
ReplyDeletePole sana mpiganaji. Tupo pamoja katika wakati huu mgumu.
ReplyDelete