
Katibu Tawala Wilaya ya Rufiji, Benjamini Mwombeki akimwagilia maji baada ya kupanda mti kuzindua kampeni ya upandaji ambayo ni sehemu ya mradi wa mkaa wa Dar es Salaam Charcoal Project katika kijiji cha Nyambili, Rufiji, Pwani wikiendi hii. Mradi huo unafadhiliwa na Shirika la Hifadhi ya Mazingira Duniani (WWF) na Benki ya Barclays. Wa pili kushoto ni Mratibu Misitu Ukanda wa Pwani wa WWF, Forest Landscape Coordinator) Isaac Malugu.

Katibu Tawala Wilaya ya Rufiji, Benjamini Mwombeki (katikati), Mratibu Misitu Ukanda wa Pwani wa WWF, Forest Landscape Coordinator) Isaac Malugu (kushoto) wakiangalia vipande vya mkaa Mara baada ya uzinduzi wa kampeni hiyo.

Baadhi ya wananchi wa kijiji cha Nyambili, wakishiriki zoezi la
kuipanda miti wakati wa uzinduzi wa kampeni ya upandaji miti ambayo ni
sehemu ya mradi wa mkaa wa Dar es Salaam Charcoal Project katika
kijiji cha Nyambili, Rufiji, Pwani.

Baadhi ya wananchi wa kijiji cha Nyambili, wakishiriki zoezi hilo

Baadhi ya wananchi wa kijiji cha Bumba msoro, watumishi wa Shirika la Hifadhi ya Mazingira Duniani wakiangalia moja ya matanuru ya kuchomea mkaa baada ya hafla ya uzinduzi wa zoezi hilo la kupanda miti
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...