HI KAKA MICHUZI,

NAOMBA NAMI LEO UNILUSHIE OMBI LANGU MANAKE IMEKUWA NI MUDA MREFU SANA TUNATAFUTA SOLUTION LAKINI HAIPATIKANI, SASA TUMEONA TURUDI KWENYE GLOB YA JAMII KUOMBA MSAADA NA TUNAIMANI TUTAFANIKIWA KWANI WENGI WAMEFANIKIWA UMU.

NIANDIKA HAPA NIKIWA NA NIA YA KUMTAFUTA MZEE WANGU MMOJA AITWAE ISSA SHAWEJI HUYU MZEE MIAKA YA 78 ALIKUWA ANAFANYA KAZI KAMPUNI YA MADINI PALE MOSHI, KISHA AKAAMIA MADINI ARUSHA NA MWISHO AKAAMIA MADINI DODOMA KATIKATI MIAKA YA 80, MZEE HUYU ALIKUWA NI MTU WA KARIBU SANA NA MZEE WANGU NA FAMILIA YETU HIVYO KUNA AMANA(MALI) ALIIACHA KWENYE FAMILIA YETU KATIKA MIAKA HIYO YA 80 NA KWA BAHATI NZURI AU MBAYA FAMILIA YETU IKAHAMA NA KUHAMIA NJE YA NCHI(UJERUMANI) NA MPAKA TUNAREJEA TENA NCHINI TUKAWA TUMEPOTEZA KABISA MAWASILIANO NA HUYU MZEE. WAZEE WETU WALIANZA KUMTAFUTA MZEE ISSA SHAWEJI ILI WAWEZE KUMPATIA AMANA YAKE LAKINI IKAWA NGUMU KUMPATA, NA KWA BAHATI MBAYA WAZEE WAKAFARIKI GHAFRA KATIKA AJALI, SASA KATIKA KUPEKUA PEKUA TUKAKUTANA NA DIALY YA ZAMANI MNO AMBAYO NDANI YA HIYO DIALY TUMEKUTA MZEE KASISITIZA MNO KUHUSU KUIRUDISHA AMANA YA MZEE ISSA SHAWEJI, HIVYO NDIO SISI KAMA WANAFAMILIA TUNAHANGAIKA KUMTAFUTA HUYU MZEE ILI TUWEZE KUTEKELEZA DHAMILA YA MZEE.

MZEE ISSA KWA SASA ATAKUWA NA ZAIDI YA MIAKA 60 KAMA YU NGALI HAI, NA TUNAMATUMAINI ANAWEZAKUWA ANAWATOTO AU NDUGU AU MTU YEYOTE WA KARIBU HIVYO KAMA TUKIMPATA MTU WA AINA HIYO ATATUSAIDIA MNO KATIKA ILI. HIVYO BASI TUNAOMBA SANA MZEE WA BLOG YA JAMII TUWEKEE ILI TANGAZO ILI WATU WAWEZE KUTUSAIDIA KULIMALIZA ILI.

KWA MAWASILIANO ZAIDI YA KIMTANDAO TUANDIKIE

salum2011@yahoo.com

S. S. SHAWEJI

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 5 mpaka sasa

  1. Kuna familia ya kina Shaweji Ni waumini wa Kadiyani wanapatikana pale mnazi mmoja kwenye msikiti wao. Ukitafuta taarifa zao inaweza kukusaidia kidogo.
    Kila la kheri

    ReplyDelete
  2. Jihadhari kuna matapeli watatafuta hata vyeti vya kuzaliwa vya huyo mzee wanajua umetoka ughaibuni kuchuma dola

    ReplyDelete
  3. Mh ! asante kwa angalizo michuzi on how to comment..however i smell a RAT in this ombi.. yangu ni hayo tu !

    ReplyDelete
  4. kuna familia za kina shaweji pale tabata na wengine wameamia kibaha..by any chance mkewe alikuwa anaitwa nora au na jee alikuwa na mtoto anitwa sefu au???

    ReplyDelete
  5. S. S. ShawejiMarch 11, 2011

    Hi Zepporah,
    Thanks a lot kwa maelekezo yako, samahami unaweza japo kunipatia contact ya hoa kina Shaweji please?, naomba uniandikie kwenye e mail salum2011@gmail.com please.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...