Home
Unlabelled
pikipiki maalum za kubeba wagonjwa zazinduliwa leo
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Most read Swahili blog on earth
Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.
hizo zitasabbisha vifo kila siku na huo uendeshaji wa daladala. labda sheria ya kuheshimu magari ya wagonjwa itiliwe mkazo
ReplyDeletekwa upande wangu sidhani kama hiyo pikipiki inausalama sababu kwa mwendo wa pikipiki haupo safe na kubebwa mtu mgonjwa sipati picha
ReplyDeletewe want more info about this issue michuzi,,,i am only imagining,picha kamili cpati,wapi naweza kuapata habari zote?,,thanks for the post lakini
ReplyDeleteHUU NI UPUUZI HUYO MGONJWA ATAVAA HELMET AKIPAKIWA HUMO
ReplyDeleteJE MAMA MJAMZITO ATABEBWA NA HIYO PIKIPIKI KWA STYLE GANI MBONA VIONGOZI WETU HAWAPIMI?
HIYO 5900 DOLA KWELI WANGEKOSA GARI ZENYE AKILI YA KIAMBULANSI ILI IWASAIDIE WATANZANIA.
MPAKA HAPO WAMECHEMSHA MNO
MDAU
da! serikali kwa kuharibu hii!
ReplyDeleteyaani kutwa kujaribu staili ya kuua wananchi wake,mara mabomu mara pikipiki sipati picha! fikiria mke wa waziri anakimbizwa hospitali ndani ya pkpk( au wao haziwahusu?)kwa hakika tukubaliane, nchi haina viongozi walioenda shule,hivi kweli unaweza kukaa mbele ya wananchi ukasema maneno hayo kuwa hii ni njia ya kuwahisha wagonjwa hospitali?hivi kweli dola 6000 ( badala ya kununua pkpk 3 ikanunuliwa gari moja la ukweli,kumbukeni kuwa magari kama hayo ya hospitali hayana ushuru bongo)zinaweza kukosa magari hata yakiwa used ya kuwawezesha wagonjwa kuwa sio wafu wafu wakiwa wanakimbizwa hospitali?pata picha mtu anayekuhusu anaumwa na umesikia amechukuliwa na pkpk kuwahishwa hospitali!hawa watu kwa kusema ukweli hawapo serious.twende kihesabu zaidi, pkpk ya mgonjwa moja ni dola 6000(kasoro dola mia) na gari la mbunge ni karibu dola 60000,wakati kati ya dola 10000 na 20000 wanapata magari mazuri kabisa! na je tuna wabunge wangapi kwenye bunge letu?je ni kweli serikali inashindwa kuongea na kampuni ya magari ikapatiwa magari ya bei nafuu,mazuri ,yaani yawe special oda.sasa turudi kwenye mahesabu ya pikipiki,ni kweli pikipiki ni suruhisho ? zitatumika wapi? kijiji gani kinaweza kutumia pikipiki,jamani mnajua vijijini barabara zao zilivyo?mimi ninafikiri kuwa serikali kama kweli ingekuwa inawapenda wananchi wake, isingekuja na ujinga huu..bora hata wangeimarisha nguvu kwenye hospitali za wilaya na baadae kuhakikisha angalau kila wilaya ipate magari mawili matatu tu ya kusaidia wananchi wake.sipati picha mama mjamzito anakuja kufuatwa na pikipiki,achana na mwenye marelia tu,ambaye anaweza kuhisi sasa ndio kifoo!vipi kama mtoto anaumwa,imeletwa pikipiki,sijui mzazi na mtoto ndio watabebwa vipi kwenda hospitali. sina uhakika kama viongozi huwa wanafanya research kabla ya kuamua upuuzi kama huu.wenzetu wanapiga hatua kwenda mbele ,sisi tunapiga hatua kurudi nyuma.mungu ibariki tanzania,lakini sio viongozi waliopo madarakani sasa.wameoza kwa kila kitu mpaka fikra.
Nadhani sasa tunafanyiwa majaribio ya design mpya ya pikipiki...!!! I cant imagine dola 5900 si unanunua saloon yenye kitanda kabisa na mgonjwa akabebwa confortable sio upuuzi huu. hapo mgonjwa kama anajisikia baridi si atakufa kwa upepo utakaomwongezea baridi hapo??
ReplyDeleteMimi
hii project huko south africa yenyewe haijapitishwa bado,halafu Tanzania tunakurupuka kununua bila hata ya kufikiria itawork out vipi,kuna usalama gani wa kubeba mgonjwa katika hicho kitanda,hii drip itashikwa vipi,nurse ataweza vipi kumonitor progression ya mgonjwa,incase mgonjwa atahitaji cpr au any invasive procedure wakati wa usafirishaji itafanywaje?
ReplyDeleteinaniumiza roho sana kuona kuwa kodi zenu zinatumika kipumbavu kiasi hiki
US blog
kila mtu ameandika na maoni yake kuhusu upumbavu huu, suala langu ni hili mja mzito akenda kuchukuliwa atavalishwa na helment juu baada ya kutiwa gesi kumsaidia maumivu? na jee mja mzito anataka kuwahishwa hospital kisha mvua ndo imenoga? atavishwa kuzuia mvua kwanza? duuuhh si atazalia kwenye pikipiki? na hata kama mgonjwa alikuwa akiumwa kidogo basi ata akifikishwa uko hospital lazma awe mahututi, naninani hasa alowaza upumbavu huu?
ReplyDeleteduhh!! me izo bei hoiiiiiiiiiiii
ReplyDeleteNdio maana gari la wagonjwa huwa na wauguzi ambao wanamshughulikia mgonjwa wakati wako njiani kuelekea hospitali. Sasa sijui watakuwa wanasimamasima ili Muuguzi afanye kazi yake wakati mgonjwa anazidiwa. Huu ujinga wa wasomi wengine unasikitisha.
ReplyDeleteAkijisikia uchungu au kutapika huyo mwendesha pikipiki na nesi watajuaje?
ReplyDeleteMaana mkao wa mgonjwa akitapika matapishi yatakwenda ktk mapafu na kusababisha gonjwa jingine au kufa.
Hivi kwa nini serikali ya CCM imechanganyikiwa namna hii ktk kufanya maamuzi ya busara au kelele za CHADEMA zimewavuruga?
Mdau-Jembe na Nyundo.
afadhaali wangenunua vitandanda vya hospitali katika kila wilaya kwani katika hospitali zetu vitanda havitoshi wagonjwa wanalala wawili mpaka watatu kitanda kimoja, kama unabisha tembelea Mhimbili ,AMANA na Temeke, hizo ni baadhi tu ya hospitali,
ReplyDeleteNi ahadi ya mheshimiwa Raisi aliyoitoa mbeya sasa inatekelezwa. Ilani ya CHAMA CHA MAPINDUZI INATEKELEZEKA. Tulipe Dowans
ReplyDeleteJamani yote tisa hapo juu; barabara ziko wapi za kutumika hizo piki piki. Maaana hizi barabara zetu za leo , piki piki humo, bajaj humo humo, baskeli, maguta ndio usiseme na mikokoteni achilia mbali madaladala yenye vurugu. Nadhani hapa Dar sio sahihi kuwa na chombo kama hiki kwa sasa.
ReplyDeleteMdau- Loliondo..!!!
Tena wakati anazindua hizo pikipiki Mheshimiwa Wazira katoa agizo kwa Mkuu wa Mkoa wa Arusha kwenda kusimamisha matibabu ya Babu Loliondo.
ReplyDeleteNa Waandishi Wetu
WAZIRI wa Afya na Ustawi wa Jamii, Dk Haji Mponda amemtaka Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Isdori Shirima kuzuia haraka matibabu ya magonjwa sugu yanayoendeshwa na Mchungaji Mstaafu wa Kanisa la KKKT, Ambilikile Mwasapile katika Kijiji cha Samunge, Tarafa Sale, Loliondo.
Dk Mponda alisema hayo jana alipokuwa akijibu swali la waandishi wa habari baada ya kumaliza kuzindua matumizi ya Bajaji kwa ajili ya kusafirishia wagonjwa. Alisema amemwagiza Mkuu wa Mkoa wa Arusha kumzuia mchungaji huyo kuendelea na utoaji wa dawa mpaka serikali itakapojiridhisha na hali ya usalama pamoja na uwezo wa dawa hiyo.
“Kutokana na hali halisi ya usalama wa kiafya kwa sasa katika eneo hilo, kuna hatari ya kuwepo kwa milipuko ya magonjwa kwa kuwa idadi ya watu inazidi kuongezeka,” alisema Dk Mponda.
lakini ndugu zangu hamuoni kwamba hii ni bora zaidi ya kumbeba mgonjwa kwenye machela au miti juu ya baiskeli kama kule kwetu Kyela?
ReplyDeleteHivi ni hela zetu au wahisani??
ReplyDeleteSerikali kwa mizaha hii sijapata ona!
ReplyDeletekweli ijitahidi
ReplyDeleteYaani inachekesha na kuhuzunisha kwa wakati mmoja!
ReplyDeleteI am speechless...!
ReplyDeleteHapo hakuna privacy kwa mgonjwa, wala usalama. Hawa watu sidhani kama huwa wanatafakari wanachokifanya b4 acting.
Wanatia hasira saaaaaaaaaaaaaana.
Ysha
sijajua tunaelekea wapi,
ReplyDeletesijajua tunaelekea wapi,
ReplyDeletesijajua tunaelekea wapi,
ReplyDeleteSasa kama wakibeba mjamzito halafu anataka kuzaa atazaa uku deleva wa pikipi anaona au anendesha
ReplyDelete