Mwakilishi wa Kampuni ya Fleva Unit ambayo ndiyo imekabidhiwa studio ya kurekodia muziki (Mastering Studio) na Mheshimiwa Rais Jakaya Kikwete, Said Fella (kushoto) akitoa ufafanuzi juu ya vifaa hivyo Jumatatu wiki hii kwenye Jukwaa la Sanaa BASATA. Katikati ni Katibu Mtendaji wa BASATA, Ghonche Materego na Mkurugenzi Msaidizi anayeshughulikia Sanaa Bi. Angela Ngowi Mbunge wa Mbeya Mjini Joseph Mbilinyi (Kulia) akihoji masuala mbalimbali kwenye Jukwaa la Sanaa BASATA wiki hii kuhusu Studio iliyotolewa kwa wasanii na Rais Jakaya Kikwete miaka mitatu iliyopita. Kulia kwake ni Mratibu wa Jukwaa hilo, Ruyembe C.Mulimba.
Mkurugenzi wa Idara ya Utamaduni kitengo cha Sanaa kutoka Wizara ya Habari,Vijana,Utamaduni na Michezo, Bi. Ngowi akitoa tamko la Rais Jakaya Kikwete kuhusu Studio aliyoitoa kwa wasanii kwenye Jukwaa la Sanaa.Katikati ni Katibu Mtendaji wa BASATA Bw. Materego na Said Fella.
Katibu Mtendaji wa BASATA, Bw. Materego akisisitiza jambo kwenye Jukwaa hilo kuhusu Studio ya kurekodia Muziki (Mastering Studio) iliyotolewa kwa wasanii na Rais Jakaya Kikwete.
Sehemu ya wadau wa Sanaa waliohudhuria kwenye Jukwaa la Sanaa wakifuatilia kwa makini masuala mbalimbali yaliyokuwa yakijitokeza.

Na Mwandishi Wetu
Serikali kupitia Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Idara ya Utamaduni imesema kwamba studio ya kurekodia muziki (mastering studio) iliyotolewa na Rais Jakaya Mrisho Kikwete ni ya wasanii waliyoiomba na hao ndiyo waliokabidhiwa.

Msimamo huu wa serikali umekuja kufuatia kuwepo kwa mkanganyiko miongoni mwa wadau wa sanaa hususan muziki wa kizazi kipya juu ya nani hasa amekabidhiwa studio hiyo na umetolewa na Mkurugenzi Msaidizi Sanaa Bi. Ngowi wiki hii kwenye Jukwaa la Sanaa linalofanyika Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA).

Alisema kwamba, studio hiyo ya Rais Kikwete imetolewa kufuatia maombi zaidi ya kumi na moja yaliyotolewa na wasanii waliohudhuria sherehe za miaka mitatu toka kuanzishwa Nyumba ya vipaji nchini (THT) na imekabidhiwa kwa wasanii hao waliokuwepo kupitia Kampuni ya Fleva Unit ambayo imesajiliwa kwa msajili wa makampuni nchini (Brela).

“Msimamo wa Rais Kikwete ndiyo huu. Studio ameitoa kwa wasanii waliomuomba na wengine wanaotaka kusaidiwa wapeleke maombi yao milango haijafungwa.
Aliongeza “Najua kauli hii itawaumiza wengi wenu hapa ila lazima mjue kwamba. Serikali haifanyi kazi kupitia maneno matupu. Wizara kwa muda mrefu imekuwa kimya ikifuatilia msimamo wa Rais mwenyewe kuhusu studio hii na tayari tumeshapata kauli yake katika maandishi ndiyo hiyo niliyowaambia”, alisistiza Bi. Ngowi.

Kwa upande wake Katibu Mtendaji wa BASATA aliwaomba wadau wa sanaa hasa chama kilichosajiliwa kisheria cha wasanii wa muziki wa kizazi kipya cha Tanzania Urban Music Association (TUMA) kutumia fursa hiyo kuomba msaada kwa Rais huku akisisitiza kwamba, Baraza lake litapitisha maombi hayo.

“Ndugu zangu kauli ya Rais ni ya mwisho. Kumekuwa na maneno mengi sana juu ya hili nadhani leo tumepata majibu kutoka sehemu husika na malumbano yatakuwa yameisha”Aliongea Materego huku akisisitiza kwamba TUMA ndicho chama cha wasanii wa kizazi kipya kinachotambulika na BASATA haitakuja kusajili Chama kingine.

Awali Mbunge wa Mbeya Mjini ambaye pia ni moja ya waasisi wa chama hicho, Joseph Mbilinyi (Sugu) sambamba na wadau wengi wa Jukwaa la Sanaa walihoji masuala mbalimbali kuhusu studio hiyo huku wakihoji uhalali wa vifaa hivyo kukabidhiwa watu binafsi badala ya Wizara, BASATA au TUMA ambavyo ni vyombo vinavyotambulika kisheria serikalini.

Walihoji pia wapi vifaa hivyo vya studio vilikuwa kwa muda wote wa miaka mitatu toka vitolewe kwani kwa mujibu wa kauli ya Mwakilishi wa Kampuni ya Fleva Unit Said Fella kwenye Jukwaa hilo la Sanaa, Kampuni hiyo imepata usajili wiki moja iliyopita.

Mjadala huo kuhusu Studio ya Mheshimiwa Rais Jakaya Kikwete ulitanguliwa na Mada ya Dhana na Mtizamo Juu ya Ukuzaji wa Fani ya Usanifu Majengo kama Tanzu ya Sanaa Kutokana na Urithi wa Utamaduni Wetu iliyowasilishwa na Dkt. Lwamayanga kutoka Chuo Kikuu cha Ardhi (ARU).

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 4 mpaka sasa

  1. Nadhani hao walioomba hiyo studio ni kwa niaba ya wasanii wenzao, hivyo si vyema wakajifanya hiyo studio ni yakwao peke yao huo ni ufisadi mkubwa...na sidhani kama Rais anaweza kupokea maomba ya mtu mmoja mmoja kama inavyosemwa na hao wanaojifanya eti huo ni "msimamo wa Serikali" je hiyo Serikali inapesa kiasi gani za kuwapatia kila kundi la wasanii mastering studio? au mnawampango wa kuendeleza kundi fulani la wasanii? au ulaji wa mtu binafsi? sidhani hata kama mheshimiwa Rais analitambua hilo....ndio maana maendeleo ni ya shida sana kwenye hizi nchi zetu za maskini maana tuna roho mbaya na ni wabinafsi. ebu chukulia mfano wa leo karibu kundi zima la wasanii wa taarabu limetoweka kwenye ajali..je kungekuwa hakuna kundi lingine la taarabu lililo imarika ingekuwaje? inamaana usanii wa taarabu ndo ungekuwa mwisho kwa mda huu??ebu jaribuni kupunguza roho mbaya na kuangalia zaidimaslahi ya watu wenye hali ya chini kwani ndo silaha ya kupunguza umaskiniii

    ReplyDelete
  2. Umempa kweli vidonge vyake..ufisadi sana bongoKila metu ni "me" "me" "me" tu ...na kama ni zawadi je amelipa gift tax? na Huyo rais analipia tax au ni chukua chukua tu...Kama ni zawadi ya personal kwanini anatangaza basi hiyo ilikua ya group lote...au kurecord kwa wasanii wasio na uwezo kucharge cheap nitaelewa..Kama atafanya bishara kama wengine I am wondering what we have become?

    ReplyDelete
  3. hio ni kweli kabisa mdau. ubinafsi na chuki havita tufikisha popote kila siku wasanii mnaimba kuwa nyie ni kitu kimoja na ndugu sasa huo uMIMI unatoka wapi tena jamani, tunaomba yaliyotokea temeke enzi za wanaumefamily yasitokee tena..tudumishe ushirikiano na umoja hio studio imenunuliwa kwa kodi zetu sote..Tujaribu kutumia busara tu!
    pia wawakilishi wa wizara wafuatilie kwa makini uhalali wa aliyekabithiwa studio hio..sio kweli kamba rais alikuwa na lengo la kusaidia au kuinua kundi flani tu!!?

    ReplyDelete
  4. Hiyo hela ya kodi ya watu. Serikali basi igawie watu wote wenye kutaka vitu kama ni hivyo. I need a commercial printer. Nasota na kujinyima ili ninunue na mimi nikipeleka maombi nitapewa? Niliomba kusaidiwa hela ya kusoma sikupata majibu mpka nikamaliza shule. Tuambiwe hiyo hela ilitoka wapi? Hii sasa ni kubwa kuliko yote. Hapo juu wote wamesema ukweli.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...