Baadhi ya wasamalia wema waliokuwa kwenye foleni ya magari baada ya kutokea kwa ajili ya Basi ndogo la Wasanii wa Kundi la Five Stars Moden Taarab wakichunguza kwa makini iwapo kuna mtu aliyebanwa ama kusahauliwa kuokolewa ama miili wake kubakia eneo hilo baada ya basi hilo kuparamia lori lililosheheni mbao lililokuwa limeharibika njiani , katika barabara kuu ya Iringa- Morogoro , eneo la Hifadhi ya Taifa ya wanyama ya Mikumi, karibu na Kijiji cha Doma, Wilaya ya Mvomero usiku wa kuamkia leo.
Lori lililoparamiana na basi la wanamuziki wa Five Stars

Msanii wa kikundi cha Taarab cha East African Melody Bi Mwanahawa Ally ( 55) akiwa wodini katika Hospitali ya Mkoa wa Morogoro leo baada ya kujeruhiwa kwenye ajali ya basi dogo la wasanii wa Kundi la Five Stars Moden Taarab la Jijini Dar es Salaam. Yeye alikuwa msanii mwalikwa kwenye safari hiyo ya kikazi katika mikoa ya nyanda za juu kusini . Picha zote na habari na John Nditi wa Globu ya Jamii, Morogoro


Majina ya wanamuziki wa bendi ya Five Star Modern Taarab waliokufa katika ajali ya gari Mikumi mkoani Morogoro usiku wa kuamkia leo yamefahamika.

Kwa mujibu wa mkuu wa kikosi cha usalama barabarani mkoani Morogoro Be. Ibrahim Mwamakula, marehemu hao ni Issa Kijoti, Nasoro Madenge, Mapande, Fembe Juma, Omary Hashim, Tizo ,Omari Tall,Ngeleza Hasan,Hamisa Omari,Maimuna , Haji Msaniwa na mcheza show wa kundi la Kitu Tigo Ilala

“ Hii ajali imepoteza watu 13 kati ya hao 12 wamefariki papo hapo na mmoja
amefariki akiwa anapatiwa matibabu Hospitalini.

"Ni ajali mbaya kutokea iliyohusisha magari matatu, ambapo waliokufa wote ni kutoka kwenye basi dogo la wasanii wa kikundi cha Five Stars na kusababisha majeruhu tisa kulazwa” alisema Mwamakula, akifafanua kuwa kati ya waliokufa 10 ni wanaume na watatu ni wanawake.

Amesema majeruhi tisa ambao wote ni wasanii waliolazwa katika Hospitali ya Mkoa wa
Morogoro ni pamoja na Mwanahawaa Ally( 55) kutoka Kundi la East African
Melody, ambaye alikuwa ni msanii mwalikwa, Susana Benedict(32), Zena Mohamed
(27), Samila Rajab (22)na Mwanahawa Hamisi (36)ambao wamelazwa wodi namba
tatu.

Kwa mujibu wa Kamanda huyo wa Kikosi cha Usalama Barabarani aliwataja
wasanii wengine waliolazwa katika Hospitali hiyo ni pamoja na Ally Juma
(25), Rajabu Kondo ( 25), Issa Hamis , Shaaban Hamis (41) na Msafiri Musa
(22).

Kwa mujibu wa Kamanda huyo wa Kikosi cha Usalama Barabarani Mkoa wa Morogoro, kuwa dereva huyo aliligonga lori hiyo wakati akijaribu kulikwepa Lori jingine lililokuwa likotokea mbele yake lenye namba T 530 BHY lenye tela T 182 BKB aina ya Scania ambapo katika harakati hizo basi hilo lililigonga Lori hiyo mbele pembezoni na kusababisha magari hayo kuanguka.

Alisema kuwa baada ya kuliparamia Lori hiyo , basi hilo liliyumba na kuhama uoande wake na kujibamiza kwenye Lori lililokuwa mbele yake ambalo halikuwa na mzingo kitendo kilichofanya paa la basi hilo kukatwa wa juu ambapo watu 12 waliokuwa ndani ya basi ndogo hilo kufariki dunia papo hapo na wengine saba kujeruhiwa vibaya .

Hata hivyo alisema , majeruhiwa mmoja kati ya saba alifariki dunia wakati alipokuwa akipatiwa matibabu katika Hospitali ya Mkoa wa Morogoro alipofikishwa kutoka eneo la tukio na kutambuliwa na ndugu zake kuwa ni Haji Mzaniwa ( 38), mwimbaji wa kikundi hicho.





Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 17 mpaka sasa

  1. MWENYEZI MUNGU AZILAZE ROHO ZA WAPENDWA WETU MAHALA PEMA PEPONI,PIA AWATIE NGUVU MAJERUHI WOTE.TUNAWAPA POLE FAMILIA ZA MAREHEMU.BWANA AMETOA BWANA AMETWAA,JINA LAKE LIBARIKIWE!!!

    ReplyDelete
  2. ajali ajali,ajali.kila siku ajali zinamaliza mamia ya watanzania,watzania nadhani hii ni chanagamoto kubwa,tujiulize tufanyeje kukomesha ajali hizi

    ReplyDelete
  3. Mungu azilaze mahara pema peponi marehemu wote

    ReplyDelete
  4. Tungependa kutanguliza pole zetu kwa wafiwa/ndugu/wafanya kazi wenzao wote, M.mungu awape wepesi katika kipindi hiki kigumuawalaze roho zao mahali pema peponi, awapunguzie adhabu za kabri, Amin.
    Napia pole ziwafikie wasanii ambao wapo hospital kwa matibabu, M.mungu awe nanyi na Inshallah m.mungu atawanyanyua na kuwapa nguvu katika kipindi hiki kigumu....Amin.
    TUKO PAMOJA KIHALI,DUA NA MALI.

    ReplyDelete
  5. Poleni wafiwa wote, poleni majeruhi.
    Kutokana na maelezo ya kamanda wa barabarani, dereva wa basi dogo ndio alikuwa mzembe.nahisi alikuwa amelewa.

    ReplyDelete
  6. Ee Mwenyezi Mungu walaze maala pema peponi marehemu amen.
    na uwajaalie Afya waliojeruhiwa katika ajali uwape umri mrefu,
    uwajaalie imani wafiwa kazi yako aina makosa.
    sote tutarejea kwako mwenyezimungu amen.

    ReplyDelete
  7. pole kwa waliofikwa na matatizo mtangulizeni mungu atawapa faraja.

    ReplyDelete
  8. poleni wadau wooote,majeruhi na wafiwa katika kipnd hk kigum tulicho kuwa nacho kwa sasa .inasikitisha na kuumiza sn kwan bado vijana na tulikuwa tunawahitaji ila mungu amewahitaji zaidi ytu.tuwaombee zaidi kwan kaz yke haina makosa. mi hanifa wa chuchu fm znz

    ReplyDelete
  9. UWIIIIIIII,JAMANI UWIIIIII,SIJAAMINI ,MUNGU WANGU EEEE..WHY ?

    ReplyDelete
  10. Inna Lillahi Waiynna Illehi Llaju'un!EEe Poleni mno jamani wafiwa wote imenistua mno!Jamani hiyo ni kazi Ya Allah sisi sote tuko njiani tutafuata,lakini TZ kama mdau hapo juu sijui kwa nini usalama wa barabarani wasimamizi mnauzembea mpaka roho za watu zitoke ndo kidogo mtafuatilia,kama hilo gari bovu lililokuwa barabarani,kwa nini usalama barabarani msilitoe kabla magali hajaleta ajali kama hivi,,yaani barabara za TZ zimekuwa ni chinja chinja,,Mwenyezi Mungu atunusuru na matsunami,na yote mabaya TZ lakini,tuwe makini,barabarani ajali zitatumaliza....Mwenyezi Mungu awarehemu waliotangulia na waliko Hospital wote,awape Tahfif Insha'Allah,,EEEH poleni mno Mola Akupeni Subirah

    ReplyDelete
  11. MUNGU AWASAIDIE WAPATE NGUVU YA KUENDELEZA SHUGHULI YAANI MPANGO MZIMA WA TAARABU.NI HAYOO TU

    ReplyDelete
  12. innalillah lillah wa inna ilayhi raajiun.. hakika inasikitisha sana sana.. wenzetu wametangulia nasi nyuma yao.. M.mungu awalaze pema na awasameh makosa yao Amin

    ReplyDelete
  13. Duuuh! Kwa kweli ni msiba mzito kwa Tanzania na hasa wasanii wa Taarab. Yaani nimesikitika mno kusikia ajali ya gari imewamaliza. Nilipokuwa Tanzania, nilishuhudia mabasi ya mikoani yakienda kasi mnao hasas sehehemu ambazo madereva walijua hakuna wana usalama barabarani.

    Mungu alaze roho za waliokufa mahala pema mbinguni. AMEN.

    ReplyDelete
  14. poleni wafiwa. Tuweni makini na kusafiri wakati wa usiku ndugu zangu. you only live once. Kipigo kikubwa hiki.

    ReplyDelete
  15. Kwa kweli ni pigo kubwa sana kwa familia zao na wapenzi wa taarab. Poleni sana wafiwa. May their souls R.I.P. Kwa wale wengine ambao si wana 5 Stars waliofikwa na msiba huu poleni sana pia. Tunaomba Mwenyezi Mungu awaponye wale wote walio patwa na majeraha.

    ReplyDelete
  16. Jamani nimeingia kule global publishers nimelia sana, kuna picha za viungo vya binadamu sikutegemea kuona katika maisha yangu kweli nimeishiwa nguvu, kweli inatisha sana, poleni sana wafiwa na watanzania wote. Mungu azilaze roho za marehemu mahala pema, AMEN

    ReplyDelete
  17. tinaa n priscillaMarch 23, 2011

    inahuzunisha sana lakini yote ni mipango ya MUNGU. MUNGU azilaze roho za marehemu mahali pema peponi. AMEN.
    From tinaa and priscilla

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...