
WAZIRI wa Afya na Ustawi wa Jamii, Dk Haji Mponda amemtaka Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Isdori Shirima kuzuia haraka matibabu ya magonjwa sugu yanayoendeshwa na Mchungaji Mstaafu wa Kanisa la KKKT, Ambilikile Mwasapile katika Kijiji cha Samunge, Tarafa Sale, Loliondo.
Dk Mponda alisema hayo jana alipokuwa akijibu swali la waandishi wa habari baada ya kumaliza kuzindua matumizi ya Bajaji kwa ajili ya kusafirishia wagonjwa. Alisema amemwagiza Mkuu wa Mkoa wa Arusha kumzuia mchungaji huyo kuendelea na utoaji wa dawa mpaka serikali itakapojiridhisha na hali ya usalama pamoja na uwezo wa dawa hiyo.
“Kutokana na hali halisi ya usalama wa kiafya kwa sasa katika eneo hilo, kuna hatari ya kuwepo kwa milipuko ya magonjwa kwa kuwa idadi ya watu inazidi kuongezeka,” alisema Dk Mponda.
Zaidi nenda 'MWANANCHI'
Bofya Hapa
Zaidi nenda 'MWANANCHI'
Bofya Hapa
Tatizo hapa..Babu anafuta ajira za watu wengi..hivi kweli hii dawa kama inafanya kazi kwa mujibu wa waliotibiwa...utazipeleka wapi Asasi nyingi zilizotapakaa huko nchini eti zinasema zinasaidia walio na ukimwi kumbe hakuna kitu..TACAIDS na wengineo....si watu watakufa njaa?
ReplyDeleteWatafanya kila linalowezekana kuiua hiyo huduma ujue ya kwamba kuna mijitu kwenye nchi yetu imekalia ubinafsi na wala haijali maslahi wala uhai wa binadamu wenzao. Hapa serikali ambacho wangekifanya ni swala la kuchukua hatua za haraka kama vile wamepatwa na janga kama mafuriko..wasaidie kuwepo kwa barabara kwa haraka, waweke mahema, wachimbe vyoo... wapeleke huduma za maji hata kwa kutumia maboza..nk, watu wa Red Cross wawepo kule kutoa huduma.. huku huo uchunguzi wao uchwara ukiendelea..
Ankal, kitu kimoja tu ninawaomba wagonjwa wa kisukari [diabetes]wanaokwenda kumuona Babu Loliondo wasiache kupima sukari yao ya damu kila siku kwa kuwa hapa Arusha kumekwishatokea matatizo ya wagonjwa wa kisukari kuacha kutumia insulin baada ya kwenda Loliondo(hasa wale waliokwenda wiki nne zilizopita). Kwa mfano, mjomba wangu ana kisukari kwa zaidi ya miaka minane lakini ameidhibiti vizuri tu (kati ya 100 na 160). Kiasi cha wiki tatu zilizopita alikwenda kumuona Babu na kunywa hiyo dawa (kabla Loliondo hakujafurika watu). Aliporudi Arusha kwa siku tano za mwanzo alikuwa anajisikia vizuri sana na akaanza kula vyakula mwiko na kuacha kupima sukari (ana mashine ndogo inayoitwa GLUCOMETER ambayo hupima sukari kwa dakika moja tu). Wiki iliyopita, baada ya kunywa chai ya asubuhi, akaanza kujisikia vibaya. Tukam-rush hospitali ambako tukamweleza daktari kuwa mjomba ni diabetic. Alipopimwa sukari akakutwa na level zaidi ya 400 (zaidi ya 20 kwa kipimo kingine)!!!!! Sasa hivi mjomba amerudia dawa zake. Ninachosema ni kuwa watu waende kwa babu, lakini kama mtu ana kisukari asiache kupima kila siku (hasa masaa mawili baada ya kula). Mbarikiwe wote.
ReplyDeleteHivi kweli INVESTORS waliopoteza muda na pesa nyingi katika kutengeneza UKIMWI duniani....kweli watakubali kupigwa bao hivi hivi.......aloo huyu mchungaji itabidi apatiwe ulinzi.....
ReplyDeleteKwa uchunguzi gani wamaana wanaoweza kufanya? Maabara zenyewe ziko hali mbaya..!
ReplyDeleteHawana technology ya maana yakuweza ku analyse (in detail) huo mti, mpaka wakajuwa components zilizomo na how zina work aginst virus and other...! Sababu hizo maabara zimechoka, hazina vifaa.
Huwezi amini Tanzania Food and drugs authority (TFDA), hawana hata HPLC! Huko kwa mkemia mkuu, HPLC iliyopo imechoka,wataalam wakubahatisha (wanaenda course ya wiki moja,) wanajuwa ku analyse bangi, cocaine na heroin kwisha..hata Mass spectometry (MS) hawana.
Watajaribu kufanya Microbial Inhibition Test (MIT), which is not enough to tell! Hii ni preminary test tu.
They can tell nothing regarding chemistry and microbiology context kutoka kwa hiyo dawa.
Tutegemee majibu ya kisiasa zaidi, lakini sio ki science!
Wao wakubwa si wameshakunywa tayari ndio maana wanaanza kupiga mkwara babu apigwe stop ili waichunguze!!! Ninavyoelewa mie hata wakiamua kuichukua kuichunguza hawataona kitu sababu kama kweli babu anavyosema AMEOTESHWA NA MUNGU hiyo dawa basi kisayansi hawawezi kabsa kuona kitu! Hapo ni swala la IMANI ya mtu, kanywa kaona kapona.Pia huyu babu hajajitangaza kabsa ila ametangazwa na watu waliotibiwa kwake na kuona wamepona SO Serikali ifanye taratibu tu za kuboresha huko bs wakati wanafanya huo uchunguzi wao. Inawasumbua sana sababu ajira za baadhi ya watu zpo ICU.!!!
ReplyDeleteserikali ijali maslahi ya raia kuliko matume yao wanayounda kila siku!...kama watu wanatibiwa wamwache babu wa watu aendelee kutoa dozi...
ReplyDeleteSerikali ya wezi wanakimbilia kusimamisha dawa kwa wanyonge,babu anaomba 500 tu,itabidi tuandamane kama babu akizuiriwa kutoa dawa.
ReplyDeleteSerikali inchotakiwa kufanya ni kuweka huduma zinaotakiwa kwa mwanadamu kwa sababu umati ni mkubwa. Zaidi ya hapo wache wananchi wamue wenyewe.Mbona hizo huduma za matibabu ya kawaida mnashindwa kutoa kwa jamii. Kwa mfano mjamzito anapata mauti kwa kukosa huduma,hospitali hazina hawa hata ya kutuliza maumivu. =wagonjwa wanapata faraja kwa kumpata mtibabu .
ReplyDeletewewe Anonymous Thu Mar 10, 09:46:00 AM 2011 umeongea point sina la ziada na wewe uliefuatia ambaye babu yako amepata tatizo tena ni kweli watu wasiache dawa ghafla.
ReplyDeleteGoverment, wise choice.
ReplyDeletembona wao wenyewe walishakunywa kabla ya kuipima hiyo dawa? sasa ndo wanajidai inabidi ipimwe. haya mambo bwana..............
ReplyDeleteNaipongeza serikali kwa uamuzi iliochukuwa japo wamechelewa sana kufanya maamuzi hayo.Tutambue kuwa hayo ni maisha ya watu, dawa pekee haitoshi kuishabikia kama kuna side effectje?si jambo la maana san kuangalia?Dawa kam hizo mbona zipo kariakoo.Lakini ninachoangalia hapo ni uhakika gani babu anaowahakikishia watumiaji wa dawa hiyo.Kama ikitokea kuwa kuna madhara sijui nani atalaumiwa kama sio serikali? Bg up Gvmnt!!!!!!!
ReplyDeletetusikimbilie kulaumu serikali jamani twende na wakati,dunia ya leo sio ya kukulupuka na vitu kama hivyo vinavyo husu maisha ya watu!
Naipongeza serikali kwa uamuzi iliochukuwa japo wamechelewa sana kufanya maamuzi hayo.Tutambue kuwa hayo ni maisha ya watu, dawa pekee haitoshi kuishabikia kama kuna side effectje?si jambo la maana san kuangalia?Dawa kam hizo mbona zipo kariakoo.Lakini ninachoangalia hapo ni uhakika gani babu anaowahakikishia watumiaji wa dawa hiyo.Kama ikitokea kuwa kuna madhara sijui nani atalaumiwa kama sio serikali? Bg up Gvmnt!!!!!!!
ReplyDeletetusikimbilie kulaumu serikali jamani twende na wakati,dunia ya leo sio ya kukulupuka na vitu kama hivyo vinavyo husu maisha ya watu!
wamwache huyo babu aeendelee kutoa hiyo dawa, tusidharau maoni ya mungu..kama watu wamekunywa na wanapona haina haja ya kuwapiga stop. mbona tunapita njiani vibao vya waganga wa kienyeji vimejaa nani ameenda kuchunguza hizo dawa wanazotumia?mbona TFDA hawajapelekwa huko?au angejiita mganga wa kienyeji ndo asingechunguzwa? imefika mahali serikali iwaache watu watumie utashi wao wenyewe manake kama watu wanaamini katika huo uponyaji waache waende kwa babu wakapate kikombe cha kufanya wawaboreshee miundombinu
ReplyDeleteKwanza babu atakukwa ameokoa ama amepunguza matumizi ya mamilioni ya shilingi ambazo serikali inatumia kuagiza madawa kutoka nje kila siku, Hususan za magonjwa hayo sugu, Lakini kwa vile ni ulaji wa watu wachache wasiokuwa na hata chembe ya huruma kwa watanzania walio maskini, watakuwa wanaona jinsi hali zao zitakavyoyumba kwa kukosa ulaji..Hapo hapo wenyewe wameshawahi huko na kujipatia dawa..TUTAANDAMANA TU HATA IWEJE IWAPO WATAZUIA MOJAKWAMOJA KUPATA HUDUMA HIYO YA UZIMA.
ReplyDeleteSerikali? hakuna serikali Tanzania. Kuna watu tu wamejazana ofisini na mafaili mezani. Hakuna anayejua majukumu yake. Waziri anampa taarifa mkuu wa mkoa kupitia waandishi wa habari halafu unasema serikali ipo? hajui hata jukumu lake kama waziri ni nini au nani anahusika na jambo fulani. ndio maaana jambo kama hili linawea kuchukua mwezi kusikia tamko kwa sababu watu hawajui majukumu yao ofisini. Huu ni mzigo kwa Taifa kuwa na viongozi wasiojua majukumu yao ni yapi na nani wafanye naye kazi. Sasa waziri unasema unasitisha huduma then whats next? husemi mmekaa kikao lini na kuamua mtafanya nini ila unapiga tu stop kwa sababu umevaa suruali. Hivi vizee vya enzi za ukoloni vistaafu sasa muachie watu waliosoma wakaelimika waendeshe nchi. Tazama TRA baada ya kuanzisha chuo chao na kuajiri wasomi. Past 10 years husikii wakitajwa gazetin au redioni, mambo swaafi kwenye ofisi zao.
ReplyDeleteNakubaliana 100% na wadau wote hapo juu. Hii habari ya serikali imenisikitisha sana. Mbona hawajazuia mganga yeyote wa kienyeji kutoa huduma zake?? Hapo ni ubinafsi, uroho, na ubabe tu.
ReplyDeleteHobidin nakubaliana na wewe na mie pia nampongeza waziri wetu wa afya kwa hatua aliyoichukua. Nilipigwa na butwaa baada ya kuona habari ya babu kwenye blog yetu ya michuzi ambayo inafanya kazi kubwa sana ya kuunganisha watu kutoka pembe nyingi za dunia. Hii ni karne ya 20 na siamini kwamba bado mtu anatokea na kusema ameonyeshwa dawa. Madawa yanayotengenezwa yanachukua mpaka miaka 15-20 ili kufanyiwa uchunguzi na kuweza kupitishwa ili binadamu waweze kutumia. Zamani dawa hazikufanyiwa uchunguzi kwa jinsi ilivyotakiwa na binadamu walipotumia zilileta madhara makubwa sana. Vilevile naelewa kuwa ni vigumu kuelewa sababu za waziri wetu kusitisha utolewaji wa dawa ya "babu" kwa kuwa wengi wetu hatuelewi sheria za kufuata wakati wa uchunguzi wetu kutokana kwamba hizo sio fani zetu. Ninaamini kuna wasomi hata wawili watatu serikalini na kipindi hiki inabidi tutumie elimu zao katika kutusaidia wote tufikie kwenye uamuzi utaotupa faida wote. Hivyo, naipongeza serikali kwa hatua hii muhimu ya kuweza kujali wananchi wake. Tunaweza tusikubaliane kwenye maoni kwa kuwa kila mtu anayake lakini inapohitajika utaaalam ni vizuri kuamini kuwa kuna kitu kitafanyika na tusikilize. Tusiposikilaza ndiyo mambo mengi yanatukuta na tunashindwa kuelewa ni nini kimesibu. yangu ni hayo tu
ReplyDeleteKarne ya 20 ndio haina miujiza na mungu kalala?
ReplyDeleteUnless huna imani yoyote na ni mwanasayansi then ongea
Otherwise hakuna point-imani itabaki kuwa imani na science itabaki kuwa science milele.
mchungaji maganga muaguzi
ReplyDeleteserikali ya kiislamu imemzuia mchungaji uaguzi
ReplyDeleteHuyo waziri angeacha roho mbaya, hivi kweli Tanzania inafurahi kuwa na idadi kubwa ya wagonjwa wa ukimwi au ndo wizara ya afya inaona ni sifa.Babu waponyeshe hao wanahaki ya kuishi kama wengine.Hii yote tamaa ya pesa eti AIDS control programme mtaji contro wenye,hadi kichefu chefu.
ReplyDeleteNadhani nyinyi wote mnaopinga hatua ya serikali hamjui mnaongea nini na wala hamjafika huko. Hapa Arusha na Moshi watu wengi waliokwenda kwa huyo babu na kuacha kutumia dawa zao za BP na sukari wamejikuta wakikimbizwa hospitali wakiwa mahtuti kabisa.
ReplyDeleteOnly in poor Africa do you have so many superstitious folks flocking in their thousands to go for a bogus "miracle" treatment. Tuko karne ya 21 SI karne ya 19 jamani.
ReplyDeleteSafi sana. mtoto wa dada yangu ana kifafa amekwenda Loliondo, kurudi A-town kifafa kimezidi kwa kuwa kaacha kutumia dawa zake.
ReplyDeleteJamanitofaiutisheni 'Miracle' , 'Sience' and Magical' anachofanya babu ni miracles na sio sciece wala magics.. Kila mtu ana uhuru wa kuchagua.
ReplyDeleteJamanitofaiutisheni 'Miracle' , 'Sience' and Magical' anachofanya babu ni miracles na sio sciece wala magics.. Kila mtu ana uhuru wa kuchagua.
ReplyDeleteBABA IMANI NA MIUJIZA HAZIHITAJI MAABARA, KWANZA HAWA VIGOGO WASHAKUNYWA DAWA THEN WANADAI WANATAKA ICHUNGUZWE KWANZA..MBONA HATA NANIHII ASHAPIGA DAWA SANA???
ReplyDelete