Shehe Mkuu wa Tanzania, Mufti Shaaban bin Simba (pichani), amewataka Waislamu wote nchini kutoshiriki katika maandamano ya wanasiasa yanaoendelea nchini kwa vile yanalenga kuleta uvunjifu wa amani.

Mufti Simba ametoa agizo hilo alipozungumza na Baraza la Maulamaa lililowashirikisha mashehe na maimamu mbalimbali wa Tanzania katika Msikiti wa Farouk uliopo katika Makao Makuu ya Baraza Kuu la Waislamu wa Tanzania (BAKWATA), Kinondoni jijini Dar es Salaam.

Kwa habari kamili tembelea HABARI LEO
BOFYA HAPA

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 29 mpaka sasa

  1. tupe ufafanuzi mandamo ya kisiasa ama maandamano yasiyosimamiwa na si si emu?

    ReplyDelete
  2. SHEHE MKUU, ULIWASHAURI VIONGOZI WENZAKO WA KIDINI KUWA SIYO VIZURI KUJIINGIZA KTK MAMBO YA SIASA. SASA INAKUWAJE LEO UMESHINDWA KUFUATA USHAURI ULIOUTOA WEWE MWENYEWE? SASA KAMA UMESHINDWA KUTII USHAURI WAKO MWENYEWE INAKUWAJE UTUSHAURI SISI KUFUATA USHAURI WAKO ULIOKUSHINDA.WEWE NI KIONGOZI WA BAKWATA TU NA SIYO MSHAURI WANGU WA KISIASA.

    ReplyDelete
  3. JK akitoka 2015 akiingia Pinda then mtaruhusiwa kuandamana.

    ReplyDelete
  4. Usahihi:
    Kuna uwezekano wa kuwepo udini kwani wadini huwa hawako wazi. Hutumia vijisababu. Pia chama hiki kimelaumiwa udini kama Cuf walivyolaumiwa. Wadini woote huwa hawako wazi. Huyu mufti simwiti mdini kwani yuko wazi.

    Si Sahihi:
    Ni vibaya kukataza watu kutumia haki yao ya kulalama. Ila ikigundulika kwamba kuna udini wa sirisiri basi raia waepuke maandamano hayo hata kama ajenda ya wazi ni nzuri.

    ReplyDelete
  5. Bora kuwa muwazi kuliko kujidai hamna udini bongo wakati ndo tishio la imani mbeleni.

    Zamani wasuni na wakatoliki waliishi vizuri. Tangu hawa waporosti walivyoingia imekuwa fujo.

    Halafu tuanze kutatua matatizo ya imbalance za ajira serikalini.

    ReplyDelete
  6. I dont understand this country! kwenye katiba ibara fulani inasema maandamano ni haki ya kikatiba ya raia huru wa Tanzania, sasa mkuu wetu wa dini tena anatuchanginyi...sisi wa dini fulani maandamano marufuku, which is which! Nazidi kupagawa... Kwa tunaomuheshimu na kufurahia fikra huru za kizalendo tufanyeje????? Once again, njia panda. sasa wale wa mama mkubwa wao ruksa kushiriki maandamano ya fikra huru na kizalendo... huoni hapo tunaachwa? tunatengwa... KWELI INACHANGINYI!

    ReplyDelete
  7. Shida za Umeme, Rushwa, Wizi wa Mazi za Umma, Maji n.k hayo matatizo yanawapa Waislamu pia.

    Mufti anapowakataza kuandamana ni vizuri angewaeleza Waislamu njia nyingine za kupinga maovu hayo dhidi ya nchi yetu.

    ReplyDelete
  8. Itachukua karne milion nyingi kwa tanzania kuendelea katika nchi za afrika,hivi bila kuwa challenge hao mafisadi kutakuwa na mabadiliko kweli? mimi nashauri kwa maaskofu kuendelea kuubiri neneo la mungu kanisani na ma shekhe kuendelea kuubiri neno la mungu misikitini.mambo ya siasa na dini tusichanganye kabisa.

    ReplyDelete
  9. Kwa hiyo kama hoja ni UMEME, RUSHWA, WIZI WA MALI YA UMMA, MAJI nk ni hoja sahihi kama itapiganiwa na wasio Waislamu ( kwani sasa Waislamu wnazuiwa kufanya hivyo) , mafanikio yote yatakayotokana na wasio Waislam watengwe?
    Binafsi , namheshimu san Sheikh Mkuu, ana staha kubwa sana mbele ya jamii na pia hana pupa , siku zote ninapomsikiliza hasa kwenye Luninga, napata somo la uadilifu na staha toka kwake.
    Napata shida kuwa hoja hii ni yake binafsi au hata kama ni ya Kikao fulani cha Uongozi wa Waislamu ilijadiliwa akiwepo na kama alikubaliana.
    Angalizo langu kwa Waislamu wa Tanzania ni kuwa adui yetu ana dini zote anatakiwa kupambana nasi wenye dini zote. Tukimuacha ati tu kwa vile sisi ni wa upande huu hivyo tunamuunga mkono hata kama anatuumiza ni UPOFU.
    Ndiyo maana sasa hivi ipo HOJA kuu ya Katiba MPYA amabayo inatakiwa kuchangiwa nasi sote.
    Nachangia

    ReplyDelete
  10. Mkuu wetu wa dini unatuchanganya kwelikweli. Maandamano ndio sehemu ya kufikisha ujumbe kwa wanaotukandamiza (yaani serikali). Matokeo ya kuwaadabisha wanyonyaji hawa ni kuboreka kwa uchumi wa nchi ambao sote tutafaidi bila kujali huyu ni muislamu au mkristo. Sikushangai, pengine unatumiwa na wanasiasa ambao hawataki kuambiwa ukweli. Wanayozungumza chadema na cuf sio ukristo wala uislamu ni ukweli wa mambo ambayo sisiemu imeshindwa kuyafanyia kazi.

    ReplyDelete
  11. Mufti hapa nafikiri umeteleza kidogo!! Nafasi uliyonayo ni kubwa na inaheshimika sana katika jamii yetu.Hatutegemei kiongozi wetu kama wewe huanze kutenga kwa dini. Ni jambo la hatari sana!! Mimi binafsi nafikiri ingekuwa vyema ungewashauri watanzania wote wanaopenda amani kutojihusisha na mambo ya kuandamana.

    Tufundishe na kusisitiza kwa waumini wetu juu ya somo la utiifi kwa viongozi. Na viongozi wasisitizwe juu ya mapenzi kwa Mungu na wananchi pia!! Tusiwe wanafiki Mufti. Ikifika mahali watu wakakosa imani na viongozi wa dini hali itakuwa mbaya. Nyinyi viongozi wa dini ni kimbilio letu pale kazi za shetani zinapokuwa zimeshika kasi.

    Kitika kipindi hiki kigumu tusichome utambi na kuipa serikali wakati mgumu wa kuanza kuzima munkal wa kizazi hiki cha vijana wa sasa.......ambacho kwenda kanisani au msikitini ni issue.....Dini zimebakia katika majina yao tuu lakini mioyoni mwao hakuna kitu.

    Muheshimiwa Mufti Mungu akutie nguvu hili usimame katika mstari na nchi yetu hisiyumbe!!

    ReplyDelete
  12. Mufti tuambie ni njia gani tuitumie ili kupamabana na serikali isiyojali maslahi ya watu wake? Hapo tutaacha kuandamana. Angalia pengo kati ya matajiri na maskini linavyozidi kuwa kubwa ka sababu tu ya uongozi mbaya kuwaachia watu wachache watafune fedha za umma badala ya kufanyia shughuli za kimaendeleo. Mimi sijaona uvunjifu wowote wa amani kwa watu kuandamana. Ni serikali inayofanya kila njia ili amani ivunjike kusudi vyama vya siasa vionekane havifai. Pia kauli yako inazidi kvunja amani kwani inawagawa watanzania kwa misingi ya dini. Serikali ndio wavunjifu wa amani wa kwanza ndio maana wanakutumia wewe ili uwagawe watanzania. Ogopa dhambi. Wamejaribu kwa maaskofu wameshindwa kwani maaskofu wanaona serikali inavyochemka.

    ReplyDelete
  13. inafadhaisha sana....kauli uliyotoa inabeba uzito mkubwa sana mbele ya jamii.

    ila mufti hujatoa njia mbadala ya kuweza kufikisha ujumbe kwa serikali hasa wakati matatizo yanaonekana wazi na wanaojali ni wachache sana.

    kumbuka matatizo yote ndani ya hii nchi yanawapata watu wote kuanzia wasio na dini, waislam, wakristo nk hivyo basi unapotoa wito au onyo kama hilo ni vyema ukatoa na njia mbadala ya kukemea uovu huo na pia namna ya kufikisha madai ya msingi ya jamii yote mbele ya serikali kwa pamoja.

    Pia unapowakataza waislam kujiunga katika maandamano unakua umekiuka haki ya msingi ya kikatiba ya kila mwananchi kwani hawajavunja sheria yoyote,,,pili unakua wewe ndie unaesababisha utengano katika jamii kwani kwani unaonesha kua waislam wao wameridhika na hali halisi ya Tanzania ya leo isiyo na matumaini ya kesho wala kwa vizazi vijavyo.

    Mwisho napenda kukujulisha kua hata wakikutii na kutoshiri basi wengine tutashiriki sana hadi hali itakapo kua nzuri kwa kila mtanzania wa sasa na badae after sisi.

    nawakilisha mawazo yangu.

    ReplyDelete
  14. YAHHEEEE!

    Mbona mufti upo ndotoni!! hii ni karne nyingine atii.

    Jiahidi kurekebisha kauli yako hiyoo! Sbb ujatutendea haki vijana wa leo.

    Wanasema nchi itajengwa na vijana wa leo, Je tusipo shiriki tutafanya nini? Ama tukae na nyie wazee vibarazani kupata GAHAWA!!! Je tutawaeleza nini kizazi kijacho?

    Mufti rekebisha maneno yako, atutaki kuwa wazembe!

    ReplyDelete
  15. "Mufti amewataka waislamu wote nchini kutoshiriki katika maandamano ya wanasiasa yanayoendelea nchini kwa vile yanalenga kuleta uvunjifu wa amani". Huo ndio ushauri wa mufti. Sasa kama katiba ya nchi inasema raia wanahaki ya kuandamana kwa kuvunja amani basi mufti atakuwa amekosea, lakini kama katiba hasemi hivyo basi ushauri wa mufti ni sasa. Siasa ni mambo ya kigeugeu leo kabaila mbaya kesho kabaila ni mwekezaji! Jana nchi yetu ni ya wakulima kesho wamanjinga nao pia wanaleta maendeleo. Kulikuwa na wakati watu wanakamatwa kwa sheria ya uzururaji! Leo kila mtu anahaki za binadamu.

    ReplyDelete
  16. NAOMBA BWANA MICHUZI UMPELEKEE MUFTI HIZI COMMENTS AZISOME ILI ZIMSAIDIE KUENGEZA MAWAZO MAZURI!!!

    WATU WASIANDAMANE KUPINGA UOVU????. TANGU NIKUMBUKE SIJAWAHI KUMSIKIA YEYE KAMA KIONGOZI AMEPINGA UOVU NI PAMOJA NA RUSHWA, DHULMA ZILIZOZAGAA NCHININI. SASA IWEJE UWAKATAZE WATU WASIFUATILIE HAKI ZAOOO.??? MUFTI HAPA UMETELEZA TENA SANA. KISINGIZIO NIKUEPUKANA VURUGU AU KUCHANGANYA SIASA NA DINI.

    ReplyDelete
  17. Waswahili tuna mambo, Mufti hajakurupuka! katoa somo la kujihadhari na maandamano ya baadhi ya wanasiasa ambayo malengo yake ni uvunjifu wa amani,kaongea na waislam mlitaka awahamasishe kufanya yasiyopendezewa na Mwenyezi Mungu, au akaongelee kanisani wakati yeye ni kiongozi wa Waislam, tumieni busara jamani tuiepushe nchi yetu na vurugu zisizo stahili! yatakayotokea mtamkumbuka huyohuyo Mufti.

    ReplyDelete
  18. Jamani ndugu zangu watanzania ni nani kasema kuna vurugu? Hizo vurugu wanaleta hao wasiotaka kuambiwa ukweli (SSM). Sisi waislamu tutamtii mufti wetu je hiyo ndiyo njia ya kuepusha vurugu? waislamu kutoshiriki maandamano si njia ya kuzuia vurugu. Naomba niwaulize swali, hiyo vurugu mnayoisema itakuwa kati ya nani na nani? Kama ni CCM na Chadema, ndani ya vyama hivyo kuna waislamu na kama ni CCM na CUF nadani ya vyama hivyo kuna waislamu na kama ni Chadema na CUF bado ndani ya vyama hivyo kuna waislamu. Kwa hiyo kuzuia waislamu kuandamana sio njia ya kuzuia vurugu. Tafuteni chanzo cha maandamano ndipo mtaweza kuzuia hizo vurugu mnazosema. Ebo tutumieni akili japo kidgo.

    ReplyDelete
  19. Kwa vile tunaamini maandamano ni kwa ajili ya kufikisha ujumbe basi sie waislamu hatutaandamana kwa kumtii kiongozi wetu lakini ujumbe wetu tutawapa hao watakaoandamana.

    ReplyDelete
  20. CAG amekagua mahesabu na kugundua pesa zimeliwa au hazijulikani zilikokwenda na aliepewa dhamana kwenye matumizi ya hizo pesa anajulikana, kuna haja gani ya kuwaita takukuru halafu baadae afikishwe mahakamani? Kwa nini asilipe gharama na kufungwa moja kwa moja? Matokeo yake kesi inachukua miaka 10 na ikimalizika muhusika anonekana hana hatia. Hao Takukuru na mahakama ndio CAG? Je haya ndiyo mufti na wengine mnataka tuendelee nayo? Tumechoka!!!!! Maandamano ni halali ya kila mtu

    ReplyDelete
  21. Kuna mtu aliwahi kutoa wazo kwamba kama serikali inakataa watu kuandamana basi tuchapishe T-shirt zenye ujumbe tunaotaka kuufikishia kwa serikali halafu watu wavae hizo tshirt mitaani. Nafikiri hili ni wazo zuri sana. Linatakiwa liingizwe kwenye katiba mpya kama njia mbadala ya kufikisha ujumbe.

    ReplyDelete
  22. Wewe mbona unaongea pointless? Huko misri, tunisia na libya hawana dini? tena ni waislamu wazuri kuliko sisi. Mwenye dhambi ni yule anayeona anaibiwa halafu anamuacha mwizi aendelee kumwibia. Hakuna mtu atakayeiondoa serikali madarakani ila lazima wajue wanatunedea ndivyo sivyo. Haya tuambie ni njia gani nyingine tutumie ili tusiendelee kunyonywa? bunge ndio hilo linajipangia mishahara mikubwa.

    ReplyDelete
  23. Mufti angeshauri Watanzania wote wasijihusishe na hayo maandamano. Hivi kwa kuwashauri Waislamu peke yao ina maana Mufti hajali usalama wa waumini wa dini nyingine?

    ReplyDelete
  24. MkandamizajiMarch 24, 2011

    Ukisoma article utakuta haya:

    Aidha, amesema, hivi sasa Rais Jakaya Kikwete anaandamwa kutokana na imani ya dini yake huku waumini na viongozi wa Kiislamu wakibaki kimya bila ya kuyazungumzia masuala yanayojitokeza likiwemo hilo.

    Amesema, tofauti na uongozi wa marais wanaokuwa na imani ya Kiislamu, marais wanaokuwa na imani ya Kikristo huwa hawaandamwi kiasi hicho na hivyo kuleta tafsiri kuwa imani ya dini ndiyo chanzo cha yote yanayofanywa rais aandamwe.

    “Misikiti iungurume na wala isikae kimya, ukimya ufe na yalaani mabaya yote hayo pamoja na dini ya Kiislamu kufanywa tabaka la chini, tuamke na tushikamane kwa pamoja” alisema Mufti Simba.

    ..........................................

    Sasa jamani kweli tunaelekea huku? wafuasi tuwe makini na maneno yanayosemwa na viongozi wetu wa kidini hawa!

    ReplyDelete
  25. Sheikh shikamoo! Hujaenda Loliondo hicho kisukari? Uschelewe bado tunakuhitaji na nafasi ndio hiyo!

    ReplyDelete
  26. Hata siku moja hatozungumzia waislamu kususia ya CCM! ni Ubaguzi tuu huu.

    ReplyDelete
  27. FUCK YOU ULIYEBANA COMMENT YANGU

    ReplyDelete
  28. Nadhani tatizo siyo dini, yani tumesahau sisi watanzania ni wavivu kupindukia, hatujali tunachokifanya, tunataka pesa ya haraka tu, angalia wewe unaetumia computer kazini kkuingia kwenye internet na kufanya shunguli zako, badala ya kuchapa kazi, watu folleni mlangoni kwako huwapi huduma, lakini undani upo kwenye internet unasoma uzembe. Dini haina uhusino na kutokupata huduma bora za afya, umeme, maji salama, kionozi kutojali wannchi wake. Tunachopigania nai huduma safi, uhuru wa kukosowa viongozi wetu, elikwa vijan bila matabaka. Udini unahusiano gani na jiji la Dar kukosa maji, au sukari kupanda bei, au wannchi kulalamika?

    ReplyDelete
  29. Wewe mbona umepata muda wa kuandika hii, acha unafiki.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...