Ankal,

napenda kutoa uhushuda wangu katika mjadala wa Loliondo ambao umekuwa ukivuma sana katika blog yetu kwa siku za hivi karibuni. Hongera sana kwa vijana wetu wakina, Magidd Mjengwa, mashaka john na bwana Mwilima. Hawa vijana wameongea mengi sana ya maana, na ninaungana nao katika hili, kwani hakuna cha tiba wala cha nini kwa babu. Wale wote waliojifanya wamepona, ndo wale wanaokufa

Kwanza, mimi ni muhathirika wa ukimwi. Niliomba ruksa ya dharura ofisini, nikafungasha, na kuondoka kwenda kwa babu. Nilipata kikombe changu baada ya siku nne tu. Kwa sasa nadhani inachukua zaidi ya wiki au mbili kumfikia babu. Yalioyonikuta loliondo, naogopa hata kuadisia; tulilala nje kwa kipindi chote. Nilishudia watu waliokuja na dripu toka hospitalini.

Kweri watu wamekata tamaa humu nchini. Baada ya kupata kikombe changu, nilirudi zangu DAR. Siku 12 zikapita nikawa situmii ARV’s , ghafla hali yangu ikawa mbaya sana ikabidi nikimbizwe hospitalini. Nilizirudia ARV zangu na sasa hali yangu imeimarika kiasi

Rafiki yangu, mwenye virusi vya ukimwi naye alienda kwa babu, karudi, na kuanza kutangaza kwamba kapona. Jana hali yake ikawa mbaya kweli, ikabidi tumpeleke hospitali ya amana. Ina maana wiki tatu aliamini amepona, kumbe ugonjwa ukawa unamtafuna zaidi. Nadiriki kusema wazi kwamba sidhani yupo hata mmoja aliyepona kwa babu. Kilichonishangaza zaidi ni hali niliyoikuta loliondo.

Nikiwa kwenye foleni, watu wanne wamefariki pale nikiwatazama, ila kuna mdada wa makamu alikata roho akisubiri muda wake wa kupata kikombe. Cha ajabu, ndugu zake badala ya kuurudisha mwili wake kwao Dodoma, walijifanya kuondoka naye na matokeo yake kumtupa njiani kama kilometa 20 toka hapo kwa babu.

Watu wengi wametupwa njiani, hasa pale ndugu wanaposhindwa na cha kufanya. Ili kuiokoa jamii dhidi ya magonjwa ya mlipuko huko loliondo na watu kutupwa kama wanyama polini, serikali inabidi iingilie kati, kwani hali ya loliondo ni mbaya zaidi na viombo vya habari vinatufichia ukweli...jamani, kuna kitu loliondo, kuna kitu kinafichwa.

aliyepima kabla ya, na kupata matokeo negative baada ya, ajitokeze. mimi sikuluka foleni, na nilikuwa na imani mpaka hali yangu inakuwa mbaya nilidhania nimepona ukimwi....

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 60 mpaka sasa

  1. Nimesoma shuhuda hizo ila wasiwasi wangu ni uchakachuaji. je nitaamini vipi kuwa hao wagonjwa wapo kweli? Kuna nini cha kunifanya niamini hayo? Inawezekana ikawa kweli au sio kweli. Ichube

    ReplyDelete
  2. Asante sana Mdau.

    Wenye kutafakari tulishasema kuwa Time Will Tell, na sasa the cocks are starting to come home to roost.

    Ningesema mengi, lakini niache hapa. Ushuhuda uliotolewa unatosha. Najua sasa watakuja watu wengi kujaribu kueleza vingine, utasikia - ohh, amani yako haba, mara ohh, umetumwa, mara ohh, mbona viongozi wa serikali wameenda...

    Eti mtu anasema, nimepiga kikombe na tangu siku hoyo situmii dawa - kwa hiyo nimepona. How unintelligent an argument is that guys?

    ReplyDelete
  3. Ndugu mtoa ushuhuda. Ungejitambulisha tukujue ingekuwa vizuri zaidi na ndipo ushuhuda wako ungeaminika kabisa. Hapa mtu yeyote anaweza kusema chochote iwe kweli au si kweli.
    Ankal natoa wazo... ushuhuda kama huu ni vema wauandikao wajitambulishe kama ushahidi wa kupona au kutopona la sivyo nani atamuelewa? Ukimwi ni ugonjwa au ukosefu wa kinga za kuzuia magonjwa?

    ReplyDelete
  4. Hiyo tunajua kwani taratibu za kisayansi hazikutumika kwenye dawa ya babu. Ila tunasubiri watu wenye busara kama wewe watokee maana tumezidiwa na wanafiki wakiwemo pia baadhi ya viongozi ambao wengine wana maPhD badala ya kuwa mfano mzuri kwa raia, wao ndio wanajionyesha unafiki wao kwa kunywa kikombe ili wananchi waje kuendelea kuwachagua kwenye uchaguzi ujao. Huyu babu ni mwongo hana kuoteshwa wala nini. Kaona kastaafu hana pesa aseme Mungu kampa dawa. Hii inanikumbusha tabia za Wagunya. Mgunya hatoi siri yake kama kafikwa na jambo baya, mpaka ma Mgunya mwengine limfike ndio atasema.

    ReplyDelete
  5. Hiyo post yako inaonyesha kwamba hukuwa na imani tangu mwanzo. After all ile dawa kama dawa haitibu ukimwi, ni imani, so uponaji haupo assured kwa kila mtu, hivyo si lazma upone ingawa wengine wanapona.Na ungekua kweli na imani ungekuwa na subira, coz kazi ya mungu hairakishwi, je kama ingehitaji kuchukua miezi mpaka upone!?? We umeshakurupuka tiyari!! Pole sana!

    ReplyDelete
  6. Mimi sikubaliani na ushuhuda wa jamaa huyu. Ili tukubaliane naye ni lazima ajitambulishe na kusema jina lake, kutoa ushuhuda pasipo jitaja jina tutaamini vipi? Kikombe cha Babu kina TIBU acheni kejeli zenu Mimi nina Mtu namjua alikuwa na Cancer na sasa ameshapona kabisa na hapo ndo nimeamini. Nadhani ili ukubali ni lazima uone ushuhuda wa kweli si huu wa kuchakachua. Kingine haiwezekani hata kidogo Ndugu afiwe na nduguye alafu amtupe kama mzoga hilo haliwezekani kabisa. Na kama lipo tungeshasikia tayari unajua jinsi binadamu anavyotoa harufu ndugu yangu? Hayo si ya kweli na omba radhi kwa shuhuda za UONGO.

    ReplyDelete
  7. Yaani Viongozi wa tanzania niwauaji wamempa huyu babu jina sasa ameuwa wengi na magazeti yalimpamba sasa watu watakufa na magonjwa yatakuwa mengi sana huyu babu anatakiwa kupelekwa mahakamani na wanasayansi watoe ushahidi wa hii dawa sababu inchi inaendelea kuelekea pabaya sana!Nafikiri Serikali ijuuzulu kwa hili sbb mpaka leo wanaendelea kumpa huyu babu nguvu zakuuwa!

    ReplyDelete
  8. Jamani mboha tupo njia panda sasa hatujui twende wapi ukuzingatia wauza vikombe wamekua wengi sana sasa me naona ni bora kila anae toa ushuhuda ajitambulishe kama mtoa waoni wa kwanza alivosema ili tuwe na uhakika na ushuhuda tunaopewa kwani wengine wana chiki binafsi na hawapendi wenzao kupona

    ebu we mtu ulietoa ushuhuda kama ni kweli jitambulishe kwa jamii kila mtu akujue na uwe muwazi kusema ukweli kwamba hujapona

    uwazi wako utaokoa wengi sana ambao wata penda kwenda huko loliondo....

    ReplyDelete
  9. Wote wanosema hawajapona hawakuambiwa waache dawa za Hospital on the sport.

    ReplyDelete
  10. Wewe usitukatishe tamaa unasema umerudia kutumia ARV zako mbona hujasema umepima na kuona kama virus vimeisha ama la! unalo hilo sisi tutakwenda tuu na sasa hivi foleni imepungua lazima twende. Kama jasiri tuma na picha yako tukuone na utueleze unafanya ofisi gani tukutafute usizidi kuchafua afya za wenzako!!! kwenda kule! Dawa hii ingekuwa imetoka ULAYA kama hizo ARV ungesema unapata nafuu!

    ReplyDelete
  11. THANK YOU!!! Asante sana kwa kutoa ushuhuda wako watu wengi wanaogopa kuikosoa Loliondo kwa vile imehusishwa na neno la mungu. Natumaini ushuhuda huu utaokoa maisha ya wachache ambao labda wanafikiria kwenda huko au wamekunywa kikombe na kuacha kutumia dawa zao. LOLIONDO sio kabisa!!! wagonjwa waendelee kunywa dawa zao kama kawaida.

    ReplyDelete
  12. Unahaki ya kutoa maoni yako...but no reseach no right to speak..,have you done a reseach ili uone ni watu wangapi wamekunywa na kupona?...do you think...watu wooote wale kwenye..foleni ya kwenda kwa babu...wamekurupuka?..trust me,% kubwa ya watu wanaoenda huko wanaenda baada ya kupata shuhuda "aminifu" za waliopona, naziita aminifu kwa vipi?...ni pale unashuhudiwa na mtu unaemfahamu na unafahamu ugonjwa wake..na sasa unaona amepona...ile dawa sio panado unanunua shop then unameza unapona...,unahitaji kuwa na imani thabiti juu ya kazi ya mungu katika uponyaji huo.sio...kusema tu mi ninaimani....while unasikilizia uone kama unapona au vipi!,....hivi wewe unadhani mtu anaweza toka all the way hadi loliondo akiigiza kama yupo hoi, anywe dawa afu ajifanye kapona?...kwa wale ambao tumeshuhudia wakipona hapohapo?.Hata hao viongozi wanaozidi kwenda ni ababu ya kupata shuhuda aminifu ndo mana wanazidi kwenda...Mwisho mimi nadhani hukuamini kupona tangu mwanzo ndo maana umekua mwepesi wa kulalamika...au ndio nguvu ya shetani kutaka kujiinua na kupinga kaziya mungu..amekuchagua wewe kuwa njia yake ya kujiinua..Pole kwa kutopona..lakina naamina ukijirudi na kuamini Mungu anaweza tenda jambo kwako utapona bila hata ya kuongeza kikombe...!

    ReplyDelete
  13. Yani usikatishe watu tamaaaa wewe jitambulishe kwa jina, na pia nikwambie ujue watu wanapeleka wagonjwa wakiwa na dripu kwanini wawapeleke???? hilo ni kosa na babu alishasema watu wasitolewe mahospitalini watu hawasikii babu ye afanye nini kama nyie wananchi hamsikiiii jaman ye aliwatuma mkawatoe wgonjwa mahospitalini wengi wakiwa wapo hoi??????? tena msimlaumu huyu babu kabisa uzembe ni wetu unampeleka mtu hoi barabara ilivyo mbaya we unategemea upate matokeo gani????? so wewe mdau sikubaliani na wewe kwanza unaonekana ni mwongo wala huumwi sema jina tujue.

    ReplyDelete
  14. asante kwa ushuhuda. mie nakuamini 100%. wanaodai ni imani wanazidi ku-confirm kuwa kikombe hakina kitu, ni uzushi tu. wajinga ndio waliwao. kwa hiyo wajinga muendelee kwenda loliondo.

    ReplyDelete
  15. Kwani ukishalijua jina la huyu "shuhuda" litakusaidia nini. Wewe kama humuamini ni wewe ila "when things fall apart" then usiseme hukuambiwa au hukuonywa. The truth is out, no one will force you to believe it.

    ReplyDelete
  16. Mwenye kusikia na asikie. Mdau ametoa ushuhuda wake. Hakuna haja ya kupinga, kwani mdau nia yake ni kutoa ukweli wake. Kama unaamini sawa pia, lakini mapaka sasa Hajajitokeza mtu yeyote aliyepona akashuhudia. Ni watu tofauti na waathirika ndiyoo wamekuwa wakiwashuhudia.

    ReplyDelete
  17. teh teh teh teeeh....! WABONGO BWANA....!!! yaaaah mnapenda sana vitu simple simple tuuuu teh teh teh.....! unajua mimi mpaka sasa almost two monthes naishangaaa viongozi wetu wakibongo wanashindwa kutoa tamko lolote kuhusiana na LOLIONDO, try to imagine kwa wastani WATU 7 wanakufa kila siku na kutelekezwa huko kisa dawa ambayo NO ONE HAS PROVIED IT SCIENTIFICALLY....hebu jamani tuamkeni tuwe profesional citizens...teh teh ....kirahisi rahis tuuu unapona eeeh, any way lakini mimi sijui ila UKWELI UTAJULIKANA....

    jamani WIZARA YA AFYA, TBS, TFDA, SEKRETARIET YA MKOA WA ARUSHA nalo hili linasubiri mpaka PINDA AU KIKWETE alitoleee tamko..... jaman jaman jaman jaman jaman......

    ReplyDelete
  18. Unajua kama ni mtu mwenye maarifa yako kichwani (intelligence), huwezi kuwa mjinga kukurupuka na kuamini. Na maarifa ujengwa kwa elimu ya duniani na maandiko ya Mungu. Uliposoma kuwa kutakuja manabii wa uongo ndiyo hawa sasa, shetani na wafuasi wake wanakuja kama malaika kwa kivuli cha dini unayoiamini. Neno la Mungu halimponyi mtu kwa masharti isipokuwa kazi ya shetani. Nimeshuhudia jana star tv, yule mama wa Tabora anahojiwa na waandishi wa habari huku akiwa amevaa rosary na bado akapandisha pepo mchafu live! Serikali inaogopa kuzuia kwa kuwa wengi wa viongozi ni waathirika pia japo hawajataka kujitangaza. Kwa kikombe kile jua kuwa unamkana Mungu muumba na kusaini kwa shetani, na kinachofanyika ni mazingaombwe, kama vile nakutengezea noti za pesa kwa vipande vya magazeti na baada ya muda hizo noti si noti tena!

    ReplyDelete
  19. POLE SANA ENDELEA KUMUOMBA MUNGU NA FUATA SHERIA ZAKE UTAPONA. Anony wa 4th Apr 12;15pm nakubaliana na wewe. Ya mungu mpe mungu na ya kaisari mwachie kaisari. Usimjaribu mungu, kama unaomba uponyaji omba nawe utapewa. Usiombe huku unaruhusu doubt moyoni that doesnt work. SWALI JE WOTE WALIOKWENDA WAMEKURUPUKA? KAA CHINI UFIKIRI MTU MZIMA HASHURUTISHWI.

    ReplyDelete
  20. LOLIONDO JUU!!!JUU ZAIDI!!!!HAACHI KWENDA MTU KULE...TUTAENDA MPAKA MWISHO!!!!

    ReplyDelete
  21. Wewe unayequote Maandiko kuwa *Ya Mu... mpe Mu... na ya Kaisari mwachie Kaisari*. Hata wenye dini yao kwa miaka elfu mbili hawachukulii maandiko so literaly.

    Can you be more Catholic than the Pope?

    ReplyDelete
  22. Huu uongo wa Loliondo ni kama nyama ya kitimoto, inayojipika na mafuta yake yenyewe.

    Mtu anapoamua kwenda Loliondo anakuwa ni kama kajitangaza hali yake tete. Sasa anaporudi, ni lazima aseme amepona, ili kuepuka unyanyapaa. Na ndiyo maana watu waliotoka huko wako tayari kuapa kuwa wamepona, lakini ukiwaambia wakapime wanakataa.

    ReplyDelete
  23. USHUHUDA

    Sasa kwani akitoa jina ndo inakuwaje? Anaweza akaandika jina kama Mickey Mouse, John Rashid, Maria Jackson, Juma Bakari au hata Babu Babu sasa ndo ndo inakamilisha vipi ushuhuda!!!!

    ReplyDelete
  24. Nashukulu kwa maoni ya wote mlio tangulia kwa kweli serikali inafatilia swala la kwa babu na inawagonjwa kiasi fulani ambao wamepewa hiyo dawa kwa chini ya wizara ya afya ili wawe wanafanyiwa uchunguzi kila baada ya muda ,licha ya serikali kuiyangalia hiyo dawa kusema kwamba haina madhala kwa mwana adam kwa hiyo tuwache sreikali na juhudi zake na pia kwani ndugu zangu duniani hakuna dawa za miti shamba ambazo zinaponyesha magonjwa mbali mbali ukiondoa huo ukimwi na sukari n.k?lazima tuwe na subira na pia tuwe na imani,mfano kama ugonjwa wa kimeo kwa watoto kuna tiba chungumzima za aina tofauti na watu wanapona kwa tiba hizo na wala hamna malalamiko,tuwe na subira hakuna lenye mwanzo likakosa mwisho,asanteni

    ReplyDelete
  25. Huyu mtu anataka watu wachangie hoja yake tu ili ajipe sifa na yeye ametoa hoja. Embu tupite tuu tumuache aende zake. Hana la maana na kama anaukimwi kweli mwacheni akajichimbie tu maana ameshakata tamaa

    ReplyDelete
  26. Jamani mtoa ushuhuda ameeleza hali yake. Na hii ndio maana ya ushuhuda. Kisha ametoa rai (ombi) kwa mgonjwa mwenzake aliyetibiwa kisha akapona. Ajitokeze na asimulie yalio moyoni kama yeye alivyoeleza. Huku akiwa ametolea mfano wa mgonjwa mwenzake anayemjua na aliye nali kama yake na wote wametumia KIKOMBE na hali yao ilivyo kwa sasa (HAWAJAPONA!). Kwa lugha rahisi akijichukulia yeye na huyo mwenzake akaona atoe matokeo ya utafiti wake wa mwanzo (preliminary results) kwa wadau tujadili. Lakini la kushangaza ni kumtolea maneno ambayo si mazuri ukizingatia ni mgonjwa.
    Pia katika utafiti wake anahitaji kulinganisha matokeo (validation) kwa wale waliopona, lakini hapa hakuna hata mmoja aliyejitokeza kusema yeye ametibiwa na amepona. Badala yake either ni kuamini/kuhisi kuwa dawa inaponya au kuambiwa bila uthibitisho wowote. Je tumwamini nani: aliyeambiwa au aliyemginjwa na akatibiwa? Binafsi naungana na mtoa maada kutaka kujua zaidi hasa kwa kupata ushuhuda wa mtu binafisi yaliomkuta. Kigezo cha wengi kwenda na kunywa si kigezo cha kupima uponyaji wake bali inategemea mabo mengi pamoja na matangazo (publicity) kwa jamii na walivyoipokea (diffusion)

    ReplyDelete
  27. Kweli Mdau mimi kuanzia namna umeandika na unavyoexpress you dont sound kama Muathirika.Imani si kitu kidogo,Kwanza Babu kasema waathirika wakae mda gani baada ya kunywa dawa ndo wapime?Ungekua na imani thabiti i tell you unge buy time mpaka watu ndo wangekushtua bwana.
    What i believe kuna wengi sana ambao hawatapona,hii ni kazi ya Mungu inahitaji kuanzia wiwo wa mgonjwa.
    Halafu sikuamini ulivyosema kuna watu wametupa ndugu zao,je Hao ndugu waliompeleka wanavyorudi makwao hawaulizi mgonjwa yuko wapi?
    Ulishindwa kabisa kupiga picha hata ya simu ama kuripoti sehemu yoyote juu ya hiyo maiti?
    Usimwaribie babu bwana,mdau mmoja kasema tujiulize watu wanaenda kufanya nini,Jibu ni kwamba kweli kuna wanao pona.

    ReplyDelete
  28. Common mwananchiApril 04, 2011

    Kumshutumu babu au kumpeleka mahakamani itakuwa sio kumtendea haki. Yeye anasema hajaweka bango la kuita mtu na kama unaenda kwa kikombe shart moja wapo ni uwe na imani, ambayo inataofuatiana kati ya mtu na mtu na ni ngumu kuipima (quantify).

    Kwahiyo, tulishashauri tangu mwanzo, mtu kabla ya kwenda ajiridhishe na dawa yenyewe kwa maana ameona mtu aliyekuwa mgonjwa, kisha akapata kikombe na akapona, tena iwe imethibitishwa na vituo vya afya vinavyotambulika, basi ajenge imani yake hapo na aende. Lakini kama mtu alienda bila kujiridhisha lakini ana imani au hana, hayo yote yalikuwa ni majaribio (Trials) na alienda kwa faida au hasara yake mwenyewe na anapaswa aridhike na matokeo utakayopata (kupona au kutopona).

    Sana sana ukimuuliza babu atakuambia hivyo hivyo, sikukuita (sina bango) na dawa yangu haina shida, tatizo wewe haukuwa na "imani ya kutosha", sasa tunapimaje imani ya kutosha hilo nalo ni swali. Nilishawahi kuandika kwamba, inabidi mtu ajiulize maswali ya kutosha kabla ya kwenda kwa babu na sio baada ya kurudi. Matokeo yake ni haya tunayoyaona sasa ya kumponda babu na dawa yake baada ya kunywa. Je alikuita???

    Kuhusu serikali, kwa upande mmoja inafurahia hali hiyo lakini kwa upande mwingine ndo imechanganyikiwa kuliko hata wananchi wake. Inafurahi maana sasa mambo ni shwari, hatusikii Dowans, Richmond, maisha magumu au maandamano ya Chadema sababu watu wako au wanaenda Loliondo. Na kwa kufurahia hilo, imeamua Kujenga barabara nzuri ili watanzania wote waende huko na waiache serikali ipumue kutokana na kashfa kibao zinazoikabili. Lakini, imechanganyikiwa kwa maana wale wote waliotakiwa au wanaotakiwa kutoa maamuzi magumu na sahihi kuhusu Loliondo na dawa za aina hii zinazoibuka kila siku, nao wameenda au wanaenda au wanatamani kwenda huko. Kwa hiyo serikali imebaki na kigugumizi. Hii ni hatari maana yeyote atakayeibuka, kama wanavyoibuka sasa kila kona ya nchi, na kwa kwa stahili ile ile ya vikombe vya kuoteshwa, inabidi serikali isimguse, impe ulinzi na viongozi waende kunywa. Kwa bahati mbaya akatokea mtu ameoteshwa kikombe kinachodhuru na kwa kuzingatia watanzania hawapendi kujiuliza maswali magumu kabla, nahisi itakuwa ni balaa kubwa na serikali itakuwa imeshindwa kulinda watu wake wasidhurike. Watu wa aina ya mdau wa ushuhuda hawatapata hata huo muda wa kumponda kikombe, watakukwa wameshadhurika.

    Nimalizie kwa kusema, Mdau wa ushuhuda (na wengine kama mmpo), Loliondo ulienda mwenyewe kwa faida na hasara yako mwenyewe, tena bila kujiuliza maswali magumu, hivyo kubali matokeo na maisha yaende kama kawaida. Ambao hamjaenda lakini mna mpango wa kwenda, pimeni kwanza wenyewe matokeo, kutoka kwa wale wote waliopata kikombe (sio huyu pekee). Na mjue mnaenda kwa faida au hasara zenu wenyewe na mridhike na matokeo vile vile. Mkipona mshukuru Mungu, usipopona pia mshukuru Mungu.

    Naomba kuwakilisha

    ReplyDelete
  29. WEWE ULIYE SEMA BABU NI MUONGO NI MNAFIKI KWANZA UKINYWA ARV'S NDIO HUFI MBONA MNAKUNYWA NA MNAKUFA VILEVILE NA DAWA YEYOTE SIO WATU WOTE WAKINYWA BASI WATAPONA SIO KWELI UNAWEZA KUNYWA DAWA HII USIPONE NA MWENZIO AKINYWA ANAPONA MNAFIKI MKUBWA WEWE NA UKIMWI WAKO MWENYE IMANI YAKE MWACHE AENDE NA ASIYE NA IMANI ASIENDEE, ILA KWA UCHUNGUZI WANGU WANAOTANGAZA BABU NI MUONGO ASILIMIA KUBWA NI WATU WA UPANDE WA PILI WA SHILINGI INAWAUMA KUSIKIA BABU AMEOTESHWA NA ANATIBU MBONA YULE KIJANA WA MBY HAWAMZUNGUMZII KWA SBB NI WAO NA NI MGANGA WA JADI.
    MWACHENI BABU AWABATIZE MTAKOMA MWAKA HUU.

    ReplyDelete
  30. Mbona una haraka hivyo? Serikali kupitia MUHIMBILI, TFDA n.k wanafuatilia kikundi cha watu waliopata kikombe kuona manufaa ya dawa ya Babu. Zoezi hili la serikali kisanyansi haliwezi kufanywa chini ya miezi 12 ili kutoa tamko rasmi la kiserikali.

    Pia kumbuka kuna watu wanapewa ARV hazifanyi kazi mpaka wabadilishiwe aina nyingine ya ARV. Pia kuna watu wanatumia Chloroquine haiwaponyeshi malaria labda kwinini ndio watapona malaria.

    Hivyo mdau inawezekana wewe ukawa 'resistant' kwa kikombe cha dawa ya Babu kama kwa wale wengine ambao ARV ya aina 'A' haifanyi kazi labda ARV ya aina 'B" ndiyo inafanya kazi ktk miili yao.

    Hivyo kwa kipindi hiki ni mapema mno kutoa tamko kuwa dawa ya Babu haifanyi kazi, bado wanasanyansi, wanakemia na madaktari wa taasisi za Tanzania wanafuatiliakwa karibu hali za wenzio wengine waliopata kikombe.

    Mugariga a.k.a dawa ya pia naweza sema ni aina ya 'ARV' yaani inautua mwili kuweza kupambana na maradhi mwilini kama ilivyo ARV za HIV ambazo huusaidia kinga za mwili za CD4 kutokuwa chini ya 250 ili kupambana na magonjwa nyemelezi. Dawa ya Babu + imani ifanya mwili kufuta magonjwa sugu aliyoyataja mwilini kwa kutumia 'mwili wako wenyewe na akili yako'

    Pia kumbuka hao waliofariki kwa HIV baada ya kikombe pengine walikuwa na magonjwa nyemelezi kama kaswende ya ubongo,ini kuharibika, hepattitis B au C, TB n.k ambayo hayapo ktk listi ya magonjwa yanayoponyeshwa na kikombe au siku zao zilifika. Maana malaria huua na kila aliyezaliwa hata kama haumwi lazima kuna siku 'atarudi kwa udongo'
    Mshauri
    Wa-Maisha

    ReplyDelete
  31. MTAKUFA SANA WABONGO, SIKUAMINI NILIPOSIKIA KUWA HATA VIONGOZI WA TANZANIA TULIOWACHAGUA KWA KUDHANI KUWA NI WATU SMART, WAMEAMUA KWENDA KWA BABU KUPATA KIKOMBE......WHAT A SHAME...JUST A COMMON SENSE, HIVI KWELI MNAAMINI KUWA KIKOMBE KIMOJA CHA BABU KINAPONYESHA UKIMWI AU KISUKARI?...I DONT THINK SO.

    ReplyDelete
  32. Anayetoa ushuhuda huanza kwa kujitambulisha wewe nani.

    ReplyDelete
  33. elimu duni na viongozi uuzo mtupu , kazi hipo hapo.
    Dunia ya leo watu bado mnaamini mambo kama hayo,
    Imani hipi hiyo?kikombe ki1 magonjwa 5.poleni!
    Ndio maana wakoloni walitutawala kiulaini kwa kututangazia dini.

    Stop AIDS ,serikali,vyombo vyo habari waambieni wananchi ukweli.

    ReplyDelete
  34. Bwana weee kama ujapona hiyo ni juu yako, usilete hapa mashauli yako, jiokoe nafsi yako mwenyewe, unadhani hata kwenye maafa wote wanangamia, basi kwa tarifa yako wapo wanopona pia, utapona kwa kadli ya imani yako, hata hapo ulipo, ukiacha maovu yako yote na kumwelekea mungu utapona, sio mpaka upate kikombe cha babu, kwani hizo dawa unazokunywa, si imani tu, imekuelekezea huko kwamba zitakusaidia ukinywa, usipokua na imani nazo, nazo hazifanyi kazi, au kwa vile mzungu amekwambia amekukuakikishia kwenye maabara ndio wapata imani, hayaa weee.

    ReplyDelete
  35. Wewe Mjengwa naona ni mtu ambaye ni very contravesial. Unaposema kuwa serikali inashabikia tiba ya Loliondo sio kweli. Unategemea kama serikali wangefanya nini kufuatia suala kama hilo? Wangepiga marufuku watu kwenda Loliondo wakati wanaenda kwa ridhaa yao? Utakumbuka pale mwanzoni waziri wa Afya alijaribu kugusia suala hilo nchi nzima ilimshambulia. Maelfu na maelfu ya watu wanaenda Loliondo na wanajipa imani kwamba wanapata nafuu au kupona kabisa maradhi yanayowasibu. Hata kama kupona huko hakutokei kwa 100% among the people wanaokunywa hiyo dawa lakini hiyo percent whatever small or big inatosha. Cha muhimu hapa ni pale ambapo dawa ilipimwa na kuonekana kwamba haina madhara (sumu) kwa watumiaji. Kuhusu kuendelea kutumia dawa za hospitali kama ARVs, Insulin, n.k. serikali ilishawaambia watu wote wanaotumia dawa ya babu wasiache kuendelea na dozi zao za hospitali. Kwa maana hiyo dawa ya babu iwe kama complimentary tu na si vinginevyo. Kwa kuwa miongoni mwa hao wanaotumia dawa ya babu wengine wanaacha kuendelea na dozi zao za awali basi hilo ni jambo jingine. Lakini suala la kutahadharishwa kutoacha dozi hizo lilishatolewa ufafanuzi kabla. Hata wataalamu wa Wizara ya Afya na watu wa TFDA pia walisema kitu hicho kwamba kwa sasa wataifanyia majaribio mpaka itakapothibithika kuwa inatibu hayo magonjwa sugu yaliyotajwa na Babu (UKIMWI, BP, Kisukari, cancer na n.k. Kwa hiyo tusiwe tu wa kurusha makombora ya lawama. Hao viongozi wa serikali wanaoenda huko wanaenda as individuals na sio kama mawaziri au wabunge au wamkuu wa mikoa kwenye official visit. Maana ugonjwa hauna cha waziri unampata individual. Tusikimbilie kulaumu. Je kama wewe Mjengwa ungekuwa Rais leo ungelipiga maruku dawa ya Babu? Nchi nzima iandamane halafu ndiyo ujue kuwa sio sahihi. Kwa muda mrefu watu wengi tu huenda kwenye tiba mbali mbali za hospital na kienyeji pasipo kubughudhiwa. Iweje leo la Loliondo liwe issue!!!!!! Hilo suala la UNO na siku ya UKIMWI duniani wala halina uhusiano na mambo ya ndani ya nchi kama hili suala la Loliondo. Wafanye tu hizo sherehe na sisi tunaendelea na kikombe chetu. Kwanza mimi naona ni mkakati mzuri tu wa kupambana na UKIMWI kwa alternative treatment psychologically!!

    Mdau

    ReplyDelete
  36. Unapochangia zingatia maadili na uwe na ustaarabu ndani yake hasa wewe uliyechangia mada saa 03.00pm, kuamini ama kuto amini ni suala la mmojammoja si kama wote unaowaita wa upande wa pili wa shilingi, kwani hata hao nao wamo kwenye foleni na wengine wameshapata huku wakibaki na imani zao kubatiza pia ni suala la mtu mmojammoja wala usitegemee utabatiza wote mbona wapo wengi tu wenye kusilimishwa makundi kwa makundi nao utawaambiaje usilazimishe imani aliyetoa ushuhuda ndio mweneye siri ya ushuhuda wake aliamini ama hakuamini ameathirika ama katumwa usichanganye mada kama haukuelewa uliza

    ReplyDelete
  37. Kila mtu aamini anvyoamini, kumsemea mwenzio ni DHAMBI. Mtu alishaenda hajaenda nani kamuomba mwenzake nauli au hela ya kula? Kupona unapona mwenyewe, kufa unakufa mwenyewe, Mwwacheni babu afanye kazi yake hakuna akulazimishaye kwenda. "BABU ANAPONYA NA WENGI WANAPONA HAJATANGAZA POPOTE KUWAITA MKANYWE KIKOMBE" huenda mnopinga hata hampajui loliondo na hamna mpango wa kwenda.

    Mnawadanganya wenzenu wasipone. Kila mtu aende kwa imani yake.

    ReplyDelete
  38. Jamani, kila mtu ana imani yake. Hata dawa za hospitali zinahitaji imani. Hata kumuona daktari tu kunatosha kumponya mtu kama ana imani naye. Mimi nimekwenda Loliondo na wenzangu saba. Lengo langu lilikuwa kumpeleka Mama yangu mzazi aliyekuwa anasumbuliwa na rheumatism kwa takriban miaka 25. Katika wale wenzangu tuliokodisha gari pamoja, wawili walikuwa ni severe diabetic wa kujichoma insulin, mmoja cancer ya damu, mwingine pressure kali sana na alitolewa hospitali siku mbili zilizotangulia, mtoto wa miaka miwili na nusu aliyekuwa na tundu kwenye moyo, na binti wa miaka 18 aliyekuwa na uvimbe kichwani na alishafanyiwa operation India mara tatu bila mafanikio kwani bado alikuwa na severe headache pamoja na convulsions za mara kwa mara. Namshukuru Mungu kwani tangu tumerudi hii ni wiki ya tatu na Mama yangu amepona kabisa, yule mwenye cancer amekwenda kupima na ameonekana hana dalili za cancer (infact madaktari wake wameshangazwa sana kiasi cha kuamua kurudia vipimo baada ya mwezi mmoja), wale wa kisukari wanaendelea vizuri na wameacha kuchoma insulin na wanakula vyakula vya kawaida, yule mtoto mwenye tundu moyoni anaendelea vizuri sana na tundu limeziba, yule mama wa pressure, anasema hajapata tena pressure na yule binti wa kichwa, hajaumwa tena na kichwa na wala hajapata tena convulsions. Infact, ameanza shule leo baada ya kuacha kwa miaka mitatu. Nina shuhuda za ndugu na marafiki wengi waliopona kwa dawa ya Babu na ambao walitupa msukumo na sisi kwenda kule. Kama kuna ambaye hakupona ni bahati mbaya tu, kama jinsi ambavyo hata hospital hawaponi wote. Lakini kwa asilimia kubwa dawa ya Babu inaponyesha. TUNAMSHUKURU MUNGU.

    ReplyDelete
  39. Nadhani wa kumlaumu hapa ni ndugu wa wangojwa wanaopeleka wagonjwa mahututi kwa babu na wala si babu. Pili babu mwenyewe ameshatoa ushauri zaidi ya mara moja kuwa watu wasiache dawa za hospitali mara moja but it seems as always wabongo wengi hawako makini kusikiliza au kusoma kwa makini. Kila kitu watu wanataka chap chap; utajiri, elimu, uendeshaji wa magari etc na unaweza kuona matokeo yake. Kuna watu wamepona na wanafahamika bwana.

    ReplyDelete
  40. Kweli huyu mdau Shuhuda ni 'miti-shamba-resistant' kwa dawa ya miti-shamba ya Babu wa Loliondo. Kwani imani ni kumshukuru muumba ambaye ametoa mmea huu wa tiba ya Loliondo kwa binadamu. Pia watu huwa 'drug resistant' kwa madawa ya kizungu na hivyo kutopona magonjwa yao kama ripoti hii chini:

    Diseases that we have always taken for granted because there was an easy cure may not be ignored any longer.

    Good examples are malaria, tuberculosis or even gonorrhoea which for many years could be completely cured with cheap medicine.

    This is no longer the case since many disease-causing organisms have mutated and now tolerate or live with these poisons.

    For example, drug resistance to tuberculosis has seen the cost of treating emerging strains jump to over Sh1.3 billion from just a few hundred shillings.

    Already, malaria parasites resistant to the new and very effective drugs called artemisinins are emerging while replacement for this treatment is still years away.

    Resistance is also emerging in the treatment of HIV, a factor that could greatly complicate the lives of more than one million infected Kenyans.

    This Thursday, while observing World Health Day, Kenyans should reflect on the increasing loss of previously powerful anti-microbials.

    Paradoxically, this is happening when global attention in medical research has turned to the more lucrative market for chronic diseases, having decided the fight against most germs had been won.

    This state of affairs has been accelerated by misuse and irrational use of medicines.

    At the individual level, there has been an increasing incidence of self-medication and even poor adherence to medical instructions.

    Any time an individual overuses, underuses or misuses medicine, he or she is contributing to the problem.

    There is a strong case for everybody, including policy-makers, regulatory authorities, the drug industry, the public and individuals to consciously safeguard today’s drug for future use.

    http://www.nation.co.ke/oped/Editorial/Resistance+to+drugs+an+issue+of+great+concern++/-/440804/1138040/-/n08wqk/-/index.html

    ReplyDelete
  41. HII INAONYESHA NI JINSI GANI SERIKALI YA TANZANIA ILIVYOSHINDWA KUFANYA KAZI KWA WANANCHI WAKE! ILA SERIKALI ITAPATA AIBU KUBWA SANA MUDA SIO MREFU! NA VIONGOZI WANAO PIGIA DEBE HUU MTI SHAMBA WATAPATA AIBU KUBWA SANA KWANI WATU WENGI WATAKUFA KWA KUACHA KUTUMIA DAWA WALIZOPEWA NA WATAALAM WA AFYA. WATAALAM WENGI WAMENYAMAZA KIMYA KWANI HAWATAKI MALUMBANO NA VIONGOZI WA SERIKALI KWANI WANATETEA SANA KIKOMBE CHA BABU KWA KUTAKA KUSAVE BUDGET YA WIZARA YA AFYA. WANANCHI MNATAKIWA KUFUNGUKA MACHO YA KIROHO NA KUFIKIRIA KWA MAKINI SANA A(DIG DEEPER) HIKI KIKOMBE KITAKUJA KUANGAMIZA WALIO WENGI TANZANIA! NINAWASHAURI WAGONJWA WOTE WAENDELEE KUWAONA MADAKTARI WAO NA KUENDELEA NA DOSE ZAO KAMA KAWAIDA HATA KAMA WAMESHAKUNYWA KIKOMBE CHA BABU KWANI USHUHUDA UNAONYESHA KWAMBA WATU WENGI WALIOACHA KUTUMIA DAWA ZAO HASA WAGONJWA WALIOATHIRIKA NA HIV WENGI WANAKUFA, KILA SIKU WANAZIKWA NA WENGI HALI ZAO ZINAENDELEA KUWA MBAYA ZAIDI.
    MASIKI TANZANIA IMEPIGWA UBUMBUWAZI NA VIONGOZI WA SERIKALI WAMETEKWA INTELIGENSIA YAO WAMEPUMBAZWA NA KUJIINGIZA KATIKA IMANI ZA KALE.
    INABIDI KUWA MAKINI HIZI NI NYAKATI ZA MWISHO YESU ALISEMA NYAKATI HIZO WATATOKEA MANABII WA UONGO, NA KUTAKUWA NA MIUJIZA IKITENDEKA SEHEMU MBALIMBALI NA UKISIKIA HAYA YANATOKEA WEWE USIKIMBILIE HUKO! NAONA SASA WATU WANAKIMBILIA LOLIONDO! TANZANIA INAPOTEA NA KUANGAMIA TUTAPOTEZA VIZAZI MUHIMU SANA TUSIPOFUNGUA MACHO YETU YA KIROHO.
    MUNGU IBARIKI TANZANIA.
    NI MIMI MDAU WA DAMU USA

    ReplyDelete
  42. ukisikiliza wanaotoa ushuhuda utagundua kuwa wapo wanaopona na wasiopona. lakini wanaopona ni wengi zaidi.
    kila dawa inayogunduliwa huwa inaponyesha kwa % kadhaa tu na pia inategemea zaidi imani ya mtu kwa dawa ile.
    kama mtu hujapona usikatishe tamaa wenzako.

    ReplyDelete
  43. Babu ni mjasiria mali tu. Km sharti la dawa ni lazima mtu awe na imani kwanini babu hawachagui wenye imani peke yao ndo akawapa dawa anawapa hata waislamu. Ukweli nikwamba babu ni muongo na anachojali ni pesa tu. Hakutumwa na Mungu wala Kulungu. Pia linachonisikitisha zaidi ni kwamba hii issue imenipa picha kwamba sie wabongo vichwa vyetu vimeoza sana na sio siri na mm ntaanzisha biashara yangu najua sitakosa vichwa km wajinga wapo wengi namna hii..Upuuzi mtupu na aibu kubwa kwetu wabongo. Eti mpaka uwe na imani ndo upone.sasa kwa nini anauza kwa watu wote na kipimo cha imani kitakuwa kipi acheni ujinga;hapa issue sio udini bali issue ni maslahi na afya za watu msitetee tu kwasababu babu ni wakanisa lako au kabila lako. Nyote mnaomshabikia babu na kumpigia debe mnashare zenu ktk madhambi ya kuuwa watu lifikirieni na hilo pia.

    ReplyDelete
  44. MH MNAOBEZA BABU KWANZA KABISA BABU HAJAMUITA MTU, WATU MNAENDA WENYEWE, PIA MUMELOGWA NA WESTERNERS, YANI MTU AKILA PANADOL BASI ANATUMIA AKILI AKINYWA MITI SHAMBA BASI NI MJINGA HATUMII AKILI, SAYANSI NI NINI KWANI? ACHENI ULIMBUKENI NA KUWA NA MAMAZO YA KUTOPENDA KUENDELEZA VYA KWENU! SO IKITOKEA MAREKANI MSINGETUKANA SIO? HIYO NDO TIBA YA ASILI YA AFRICA AN IT WORKED FOR SO MANY AND IS STILL WORKING PERIOD, KAMA HUUMWI HUNA HAKI YA KUSEMA, NA HUJAUMWA THATS WHY!

    ReplyDelete
  45. asante mdau uliotoa maelezo apr 04,03.59.00 pm tunashukulu kwa ushuhuda wako lakini swala la wengi lipo pale pale kama ungejitambulisha na pia hospital ambazo hao wagonjwa walizokuwa wanatibiwa na uthibitisho wa vipimo vyao hao wagonjwa kutoka madaktali wao hapo inakuwa rahisi mtu kukufaham vizuri hivi ulivyozungumza ni vizuri sana lakini bado pale pale kitambaa cha macho hatuoni mbele,muhimu tuwache wizara hili jambo litatoa wazi maelezo yake itapofikia wakati wake maana humu tunaumizana vichwa tu tunapotaka kuelimishana tuweke wazi kila kitu ili tuwe waaminifu kwa kila upande,mimi naomba tujitahidi tuweke maelezo yaliyo wazi kabisa,mdau istanbul,turkey

    ReplyDelete
  46. Imani ni psychological issue na Maradhi ni Physiological issue..SASA NYIE WADANGANYIKA MTAAMINI VIPI KUWA IMANI YAKO ITAKUPONYA? MIE NASHINDWA KUELEWA KABISA KWA NINI WATU WAMEUVAA UJINGA KAMA NGOZI WAKATI DUNIA YA SASA KILA JAMBO LIKO WAZI.

    ReplyDelete
  47. Wengine wamepata magonjwa kwa sababu ya laana. Sasa kama mtu alibaka wanawake akalaaniwa. Au alikuwa anafanya ushoga na laana ikampata unatarajia huyu awe na imani?

    Atakuwa na imani tu kama atatubu maovu yake. Mtu yeyote aliyefanya maovu na akapata laana huyu asipotubu dhambi zake na kuacha dhambi atakufa tu.

    Kuna wengine Wanakwenda kunywa kikombe ili wakipona waendelee na matendo ya ki haramia. Hao hawatapona na tutaendelea kuwasikia hapa mkijitokeza. WENGINE WANGA/WACHAWI WAMESHAROGA WATU NA KULA NYAMA ZA WATU SASA MUNGU KAWAHUKUMU KWA KUWAPIGA NA MAGONJWA. TUBUNI JAMANI TUBUNI ACHENI VISINGIZIO. Wengine wamedhulumu vitu vya watu. NA WENGINE MUDA WAO WA KUFA UMESHAFIKA. TUKUMBUSHANE!!!

    Lakini mwenye Imani lazima apone. Imani inaanzia kutubu na kuacha maovu

    ReplyDelete
  48. Thank you Thank you kwa huyu alietoa ushuhuda wa watu waliopona. Mimi ningependa kutoa reminders chache tu kwa wote:

    1) Babu hajamlazimisha mtu yeyote aende kwake; Go with your OWN FAITH, and partake the cup at your own risk.
    2) If the dawa did not work for you, it is NOT a guarantee that it will not work for everyone!
    3) Everyone has a right to give their own testimony on this website; this is a free blog that encourages communication. Usiwe quick to judge someone's view just because it is different from yours!
    4) Trust in the Lord your God! Just because a Government official went to Loliondo and reported it, doesn't mean all of a sudden he is the 'measuring stick' for success or a cure! A govt. official is a Human Being like you! But that which is a miracle is just that! Oh ye of little faith!
    5) Miracles do happen! Pray for Babu that he continues to cure those with icurable diseases, and Thank God for this one of a kind miracle! AMEN!

    ReplyDelete
  49. Halafu inaonekana kuna watu wanaotamani hii dawa isifanye kazi. Ila nawapa pole manake waliopona na tunawafahamu ni wengi sana. Sasa huwezi kutuambia tunaowafahamu na wale wenyewe waliopona tukubaliane na wewe. eti tuseme ni kisaikolojia tu.

    halafu wale wanaopinga wana maslahi fulani. Kwenda Loliondo tunaenda kwa nauli zetu hakuna anayetulipia hapa. Tuacheni tuende. La mwisho naomba niulize mbona wanaopinga wana uchungu sana! kwani watu wakipona nyie mnateseka kivipi?

    Kama watu wangekuwa hawaponi wangeshaacha kwenda Loliondo. Nyie wapinzani wa Mchungaji mshindwe sana

    ReplyDelete
  50. Hata ukipata jina na picha iweje? kwani amekutaka? mbona tuna shindwa kuheshimiyana? kila mmmoja anatoa ushuhuda wake mbona wale waliomfagilia babu hatuja washambulia? ama kweli wabongo bado tuko nyuma sana hatuna hata hekima ya kukubali kwamba mshuhuda ameamua kutoa ushuhuda wake kwa nia njema? TUMEKWISHA. ebu tumieni akili mliopewa na Mungu jamani. Na muwache kunyanyapaa, yawezekana huyu unaemnyanyapaa ni ndugu yako. Tulia kwanza uwaze kisha tumia busara unapo toa maoni.

    ReplyDelete
  51. Watu wengine huwa wanafiki na wabinafsi. Huyu aliyetoa ushuuda yeye hakupona kwasababu alienda kumpima babu kwamba sio mkweli. Sasa ujumbe wangu ni hivi wewe haukupona kwasababu ulienda kwa lengho la kumzalilisha babu na ndio maana ukatanga hata kwenye mtadoa wetu wa jamaii nakushauri uwe makini mungu atakukomesha. Naomba ndugu zangu wote wenye imani na babu waende na wale wasio na imani wasipoteze mda wao kwenda kwa babu maana hawatapona

    ReplyDelete
  52. Watu wanamahasira kweli na huyu mtu ..Jamani kama umekunywa na unaamini basi kaa kimya yeye anaeleza aliyoyaona huko. Alikwenda na kupoteza 4 days na gharama za watu kwenda huko...Hamtaki kusikia the other side of the story kwa nini? Kwani ni uongo kuwa watu hawajafa huko na wengi wanazidiwa. Kwani ni uongo huo. Ngoja mtakavyoona tunaongeza kuwa pita wanigeria kwa maambukizo ya Ukimwi...

    Serikali isipowaelimisha watu hii rate ya ukimwi uliyoo itaingezea mara 100. Labda serikali inaona tuko too many sasa inaona hii itapunguza people

    ReplyDelete
  53. USHAURI

    KWA USHUUDA WA HUYO MTU HAPO MIMI SIONI KOSA LA BABU LOLIONDO LIPO WAPI
    JE ANGETUAMBIA KUWA BABU ALIMWAMBIA KUWA AACHE KUTUMIA ARV
    yeye kaenda kunywa kikombe na wala hakuambiwa aache kutumia arv pia tujuwe kupona na kikombe ni linataka pia imani na si kwenda tu kunywa
    pia yaonyesha mwana ushuuda alikuwa anamjaribumungu na si kuwa na imani
    loliondo goes on babu juuu
    fitina ziachwe babu hakusema kuwa kila atayekunywa atapona so ushuuda wako hauwezi kuharibukazi ya mungu kwasababu hukuambiwa uache arv
    pia swala la watu kufa njiani kwa kukosa huduma si kosa la babu na wala halihusianina mchungaji masapile hata pia suala la hudumambovu halisuiani chochote na mchungaji so malalamiko ya huduma mbovu peleke ccm au kwa kikwete kwani wao ndio wahusika kwa hudumakwa jamii

    ReplyDelete
  54. Watu wanamahasira kweli na hwataki kuambiwa ukweli kwa vile wanataka hii dawa iwe kweli...trust me thanks god for this person who is willing to point out the truth.

    hii dawa ingekua ya kunywa mara tatu nne ninge weka chembe ya imani yangu kuwa itaponyesha japo ugonjwa mmoja lakini magonjwa haya yote? ni kuwa ameona kila mmtu anaumwa. ni kama waread mikono wote wanaenda kwa mapenzi, money, and happiness kwa vile hivyo nimepungua kwa kila mtu...

    ReplyDelete
  55. Babu huyu mimi naona anatuzongua tu kipimo cha imani kipo wapi hapo. haya endeleeni tu kuamini uchawi, mazingaombwe na utapeli wa kutajirisha wengine. Halafu wagonjwa weeeeeeeengi kweli Tanzania hii wengine wanakunywa kikombe wapate utajiri si uchuro huu, Inaudhi saaana kuishi na kuongozwa na viongozi majuha kwani nawe unakuwa juha

    ReplyDelete
  56. Khah! wabongo macomedian sana. Nimesoma comments zote za wenye kupinga kikombe na wenye kukipenda lakini huyo aliyesema kuwa serikali imeona tuko wengi sana hivyo hii ni njia mojawapo ya kutupunguza imevivunja mbavu mpaka nimetaka kujikojolea jamani. Duh bongo hamna earthquakes, hurricanes, cyclones wala tsunami ila hii sasa ni tsunami yetu. Ehhhh Mungu turehemu wote. Wenye kuweza kuona na waone.

    ReplyDelete
  57. Nyie mnaosema ati kama haiponyeshi mbona watu wengi wanakwenda tu? Fungueni macho hivi umeshaisikia ile habari ya the Jonestown massacre? Kama hujasikia google hiyo story na usome utaelewa. Watu wakunywa sumu na kufa under the name of God. Unataka kuniambia watu 900 wote naoa walikua hawajui sumu itawaua? That tells all the psychological impact of the mind control techniques. Sasa usizanie kwenda watu wengi ndio sababu au uthibiitisho kuwa hiyo dawa inaponyesha. Psyclogy crowd hiyo tu the power of situational and social influences...

    Imani ipo mahali popote lakini kuna magonjwa ambayo hata wanaofanyaga research na dawa zao wanawapa nusu ya group real meds na kundi lingine fake meds. Na wanaweza wakapona wote waliokunywa dawa na wasiokunywa. Hayo magonjwa hayahitaji tiba...BP, kisukari unaweza kucontrol hata bila ya dawa ni life style changes tu na mavyakula yetu tunayokula kila siku ndio yanatuengezea hayo magonjwa. Hivyo hao wanaosema sijui watu walikua wana BP, kisukari wamepoa I won't listen to those..That is a very little price to pay from all the people died so far just waiting to see MR BABU. Huyo anayesema mtu alikua ana cancer na amepona...Please tuonyeshe reports za before and after kutoka kwa DR. Na wenye ukimwi vile vile wakae week 6 waende wakachukue vipimo. Hiyo dawa kama ni very powerful mti shamba unaweza ukavificha virusi hivyo visionekane kumbe vipo tu. Nenda kapime baada ya week sita. Tusiambiane tu kwa kuona mtu anatembea vizuri leo..Imani inaponyesha kwa muda...Na hata madacktari wa ukimwi huku niliko wanawaambia wagonjwa wao attitude yako ndio itakufanya ukae sana. Hata hizo dawa wanawapa lakini kama wewe ni mtu wakuwa depress all the time hutasurvive. Wenye kusema huyu hana imani basi wenye imani tuleteeni evidence hapa. Kila mtu ni mimi rafiki yangu, sijui jirani blalablala Mbona hamna anayesema mimi ni mfano hai...TB imekwisha, Sasa hivi nipo HIV-


    Ndio ile tukiwa wadogo tuliambia kuna mwanaume kazaa. Watu walienda hospital wengi kumwangalia lakini hakuna aliyekuja akasema kweli nimemwona ni kila mtu yeah nimeambia...nimeambiwa....hakuna cha kuambiana hapa yeah save others kwa kutoa vipimo vyako hapa tuone..sio kukaa kimya na kusemea fulani fulani.

    ReplyDelete
  58. HUYO JAMAA NI MUONGO AMETAKA KUUZA SURA

    ReplyDelete
  59. Jamani poleni kwa yote.

    Mimi nina ndugu zangu wawili ( dada na kaka) sote kwa pamoja (3) tuna shida ya kisukari. Na wote tulienda kwa Babu. Dada alikuwa haoni tena na ilikuwa apelekwe KCMC ili akwanguliwe macho yake maana hata miwani ilikuwa haisaidii tena. Sasa hivi hahitaji hata hiyo miwani na amerudi kazini. Ni mwalimu anafundisha shule ya msingi Makumira waweza kuja kuhakikisha mwenyewe. Kaka wakati tunaenda, yeye sukari ilikuwa 25. sasa hivi (wiki 2 baadaye) sukari iko 6.5! Frequency ya kukojoa haipo tena kabisa. Ukitaka kuhakikisha, waweza kumtembelea anafanya kazi idara ya maji Muleba. Mie ambaye nimekuwa na sukari kwa muda mrefu zaidi yao ndiye bado nasuasua ila cha ajabu ni kwamba ganzi miguuni, kukojoa ovyo, uchovu na loss of concentration vimeisha kabisha. Nasubiri kupona kabisa. Ila sijaacha kutumia dawa maana aliniambia nisiache mpaka nitakapoona nimepona kabisa.

    ReplyDelete
  60. Kumbe watu wanapenda kusikia positive tu kuhusu babu ....?

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...