Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 11 mpaka sasa

  1. AMA KWELI ASILI HAIPOTEI!!!! HIZI KWELI ZIMERUDI ENZI YA KINJEKETILE NGWALI (NI HISTORIA TU IMEJIRUDIA HATUSHANGAI SANA )

    ReplyDelete
  2. Teh..Teh...Teh.......
    Eee Mugnu utusaidie. Tuepushe na hao wahubiri wa uongo na wanatumia jina la YEsu kama kigezo.

    ReplyDelete
  3. Haya mnayoyaona ni matunda ya makanisa yanayoibuka kila siku bila kuwa na mfumo wa kudhibiti kwasababu kila mtu anatumia kanisa kwa faida yake. ukianzia Vatican ambapo hujasikia Papa akisema kaoteshwa na Mungu. kuna makanisa yaliyoanza Nigeria ambako yametegemea zaidi katika kunufaisha wahubiri kimaisha kwa kuwadhulumu waumini kwa njia la hila na kutumia jima la YESU. Wanajua waafrika rahisi kuamini wakiambiwa tu kwa jina la YESU basi hakuna maswali. na hii sio wananchi walalahoi mpaka viongozi wetu nao wamo katika kufuata ili mradi jina la YESU limetajwa.

    hata ukiibuka na ukatili ukitumia jina la YESU watu watafuata. hii si ya leo tu bali historia inaonyesha haya mambo yameanza zamani zama za ujinga. yaliachwa ulaya baada ya mapinduzi ya kisayansi yalipotokea. kwa waafrika bado tuko kwenye zama zile za ujinga kwasababu japo sayansi ipo lakini hatuielewi.

    Swali dogo tu nataka kuuliza huyo aliyesema katokewa na YESU ama BIKIRA MARIA alizungumza lugha gani na alikuwa na anafanana vipi na unahakika gani kwamba ni huyo unaemdhania wakati hujapata kumuona maana mpaka leo wazungu waliondika historia hawana picha ya yesu. yule anayetumiwa ni MZUNGU wa west europe wakati YESU alikuwa Myahudi na wayahudi wana umbo tofauti na yesu anayetumiwa katika picha.

    pili ni matunda ya ukweli kwamba wabongo karibu asilimia mia wanaamini ushirikina zaidi na hiyo si kwa walala hoi bali mpaka viongozi tena wa ngazi zote.

    Tatu ni ukweli kwamba bongo hakuna wasomi wa nyanja ya sayansi kama wapo basi ni wale wa kukariri na sio wa kutumia fikra zao wenyewe kufikiri na kutenda yaliokatika elimu ya sayansi. hii inahakikiwa na kutokuwa ama uchache wa uchapishaji wa matokeo ya uchunguzi wa kisayansi katika majarida ya dunia. wasomi wetu ni kukariri ya watu walikaa na kukuna vichwa halafu wakafaulu mitihani ambayo imepitwa na wakati. ndio maana sauti zao hasikiki hasa wakati masuala kama haya yanapoibuka. nao pia wanaweza kuwa wanazuiwa na ile sababu ya kwanza na ya pili.

    ReplyDelete
  4. He sisi Watanzania bwana. Tulishaenda vitani tukiamini kuwa risasi za Mjerumani zitageuka maji. Hakuna jipya hapo. Lakini inasikitisha sana.

    ReplyDelete
  5. 200-2010 was the Bongo flava decade
    2011+ is the "vikombe" decade (Age of vikombes)
    Subirini 2020 muone wengine wataokuja na usanii mpya.

    ReplyDelete
  6. HAPA MIE SIONI CHA AJABU ILA NI KWAMBA BAADA YA BABU KUVUTIA MACHO NA MASIKIO YA WATU NDIPO VYOMBO VYA HABARI VIMEKUWA VIKISHIKILIA BANGO HILI SWALA...
    KABLA YA BABU HAWA WATU WALIKUWEPO WENGI TU TENA WENGI SANA LAKINI KWA KUWA HAWAKUFATILIWA NA VYOMBO VYA HABARI HAKUNA ALIYEKUWA AKIJUA... VYOMBO VYA HABARI NI MUHIMU SANA KATIKA KUELIMISHA ILA WATOA HABARI WENYEWE WANAPOZITANGAZA HIZI HABARI WANAKUWA NA MTAZAMO FULANI AMBAO KILA MSOMAJI ANAUPOKEA KWA UTOFAUTI KUTOKANA NA MAZINGIRA ALIPO, ELIMU, IMANI YAKE KIDINI NA HATA HALI YAKE KIAFYA.
    JE MTAKUBALIANA NA MIMI KWAMBA HAO WAGANGA WA JADI NA WAPIGA RAMLI WALIKUWEPO WENGI TU SIKU ZOTE NA SI TANZANIA PEKEE BALI MAHALI PENGI DUNIANI? ILA KWA KUWA HABARI ZA BABU ZIMEUZIKA SANA MAGAZETINI NA KWENYE TV NA REDIO BASI VYOMBO VYA HABARI VINAZIFUATILIA KWA KARIBU HADI SASA WATANZANIA WOOTE WAMESHASAHAU HATA WAKINA DOWANS NA WENGINEO.

    IMEFIKIA WAKATI SASA MIJADALA HII IFIKE MWISHO WATU WAFIKIRIE MAMBO MENGINE!!!!!

    ReplyDelete
  7. kazi ipo dah...

    ReplyDelete
  8. MSITUDANGAYNE BWANA, HAWA WOTE NI WAFUASI WA nabii Yohana Mashaka ANAJIFANYA MTAKATIFU KUMBE ANATUMIA MIGONGO YETU KUANZISHA MADHEHEBU YA WAKINA BABU KILA KONA. INOGILE, MBEYA, MABABU NA BADO SANA

    ReplyDelete
  9. Everything that sounds too good to be true is not true

    ReplyDelete
  10. mtajiju nyie wenye imani thabiti sasa mchague nyie tone la maji kikombe kimoja kwa babu au vitatu itunduma hehehehehe mi sina imani thats y ninawaambia nyie ninayemwamini anitosha

    ReplyDelete
  11. Common mwananchiApril 07, 2011

    Tumeshaandika sana lakini wapi. Ni kwamba, tutaendelea kuona vikombe vipya kila siku mpaka pale watu wenyewe watakapoamua kwamba sasa imetosha au yatakapojitokeza madhara. Kwa sasa, swala hili lipo kwa namna mbili kuu; kwanza ni mtu kuoteshwa na pili kupata mamia ya wanywaji wa kikombe. Alipooteshwa Babu ilichukua muda kwa watu kufurika kupata "Ze Original Kikombe" kutokana na kusambaa taratibu kwa habari na "shuhuda".

    Lakini tofauti na "Ze orijinal kikombe", vikombe hivi vipya vinapata mamia ya wafuasi kwa haraka ya ajabu tena bila kujiuliza maswali wala "shuhuda". Yaani sasa kwa watu wengi sasa, INATOSHA TU kuwaambia nimeoteshwa, na wakaamini kwa asilimia 100 na kufurika. Tena wengine hawaoteshwi na Mungu, bali na shangazi, bibi na mizimu. Kwa ufupi ni watu wenyewe wanaotengeza ndoto na vikombe kwa sababu maadamu kila anayeoteshwa anapata mamia ya watu, kwanini wasiibuke kila siku???

    Ndio maana kwa mtizamo wangu, tatizo kwa sasa ni watu wenyewe kuliko waoteshaji/waotaji. Kama kweli watu watatumia muda zaidi kujiuliza maswali ya dhati na kuwa kama Tomasokwa kupata ushaihidi wa kweli wa waliopona, kabla ya kukimbilia kila kikombe kipya, basi naamini itawakatisha tamaa waotaji na vikombe vipya.

    Basi, ombi langu ni tuendelee kuwasii watu wasikimbilie kwa waotaji ili kuzuia kuchipuka kwa ndoto na vikombe vipya kila kukicha. Inawezekana kabisa wengine wanafanya ndoto kama mradi wa kuchuma na wanajua kabisa kuna ukomo katika hili, kwa hiyo wanngependa kuota na kupata watu haraka haraka kabla kila mtu hajaota kikombe chake mwenyewe. Dadisi.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...