Ankal,

Saalekoo,natumai uko poa na unaendelea vyema na libeneke huko pande za Obama.

Leo asubuhi kulitoka mzinga pale makutano ya Morogoro na Samora. Mashuhuda wanasema jamaa wa gari ndogo (Nissan kama sikosei akiwa Morogoro road) aligonga Nissan Civilia bus ikiwa inamalizia junction ya Samora na kusababisha dereva akose mwelekeo akapinduka na kudunda pick up, utaona ilivovuliwa nusu ya sehem ya kuwekea mizigo.

Cha kuchekesha jamaa walikuja na breakdown ndo kuinua basi, kaazi kweli kweli. Mwisho wa siku ilibidi wasamalia waliokuwapo kuamua kuiinua basi baada ya breakdown kuwa inainuka tairi za mbele kila ilipojaribu kuliinua basi. Bongo tambarare sanaa.

Mdau sele
BreakDown ikijaribu kuliinua basi lililokuwa limeanguka mara baada ya kugongwa na pickup.
Hivi ndivyo mambo yalivyokuwa.
Barabara ilifungwa kwa muda mpaka utaratibu wa kunyanyua basi hilo ulipofanyika.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. Mswalie mtume

    Mini bus lilikuwa katika spidi kali sana. Barabara za ndani ndani kama Samora hairuhusi na si busara hata kidogo kuendesha gari kwa spidi ya 80- 100km kwa saa kwani ni sehemu bize sana na lolote laweza kutokea.

    Dereva atawajibika kwa polisi na mwajiri wake pia iweje apinduke sehemu kama ile na apinduliwe na ki Nissan saloon? Pia madereva wangine hupata kiwewe panapotokea hali ya hatari au ajali kiasi kwamba wanachangia kusababisha ajali iwe kubwa zaidi kwa mafano dereva wa basi iliyojaa abiria na aliyekuwa mbio haswa na kuamua kumkwepa au kupiga breki ghafla pale mbwa anapokatiza ghafla barabarani, au mwendesha baiskeli mlevi kaingia ghafla barabarani. Dereva anapindua basi na kuuwa abiria wengi zaidi.

    alex bura, dar

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...