Makamu wa Rais wa Safari Club International-Tawi la Ottawa Bw. Glenn Vodden akimkabidhi Mheshimiwa Balozi wa Tanzania Canada, Alex Massinda mfano wa hundi iliyotumwa Chuo cha Mweka kwajili ya manunuzi ya Projector. Kushoto kwa Balozi ni Bw. Barry Turner na Bw Joseph Sokoine Afisa katika Ubalozi.

Safari Club International Tawi la Ottawa limetoa msaada wa fedha dola 1,300.00 kwa ajili ya manunuzi ya projector kwa matumizi ya Chuo cha Mweka Moshi. Projector hiyo itatumika kwa ajili ya kufundishia wanafunzi Chuoni ambapo balozi wa Tanzania nchini Canada Mh: Alex Masinda, alikabidhiwa mfano wa hundi hiyo juzi na Bw. Glenn Vodden makamu wa Rais wa Club hiyo. Barry Turner aliyeongozana na Rais huyo aliwahi kufanya kazi katika chuo hicho mwanzoni mwa miaka ya 1970.



Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. Ankal

    kwa kweli chuo cha mweka inabidi kisaidiwe, hata ikiwezekana wadau wa globu wachange mia mia tu; tuwanunulie vifaa. ni chuo muhimu na cha kipekee katika kusimamia wanyamapori na kutunza mazingira.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...