Kikosi cha Simba.
Kikosi cha TP Mazembe ya DRC.

Timu ya Simba ya jijini Dar,leo inashuka dimbani kumenyana na timu machachari ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo-DRC, TP Mazembe, katika mechi ngumu na muhimu ya Ligi ya mabingwa Afrika.

Mechi hiyo inanayotarajiwa kuanzia saa 9.30 alasiri ndani ya Uwanja wa Taifa wa jijini Dar es Salaam. Simba inatakiwa kuibuka na ushindi wa mabao 2-0 au zaidi katika mechi hiyo, kwa kuwa mchezo wa kwanza timu hizo zilipokutana nchini DRC, Simba ilichapwa mabao 3-1.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 7 mpaka sasa

  1. wadau kama kuna mtu anaejua website yeyote inayoonyesha hii mechi maana wengine tuko mbali na nyumbali.
    mdau UK

    ReplyDelete
  2. Maajabu yalitokea jijini Nairobi, Kenya ambapo timu ya Sofapaka ya Kenya iliifunga Ismailia ya Egypt 4-0 na hivyo Sofapaka kusonga mbele kwa ushindi wa 4-2 aggregate.

    Simba nanyi leo jumapili 03/04/2011 tunawaombea mfanye kitu kisichowezekana kwa kuifunga TP Mazembe 3 mtungi.

    Mdau
    Msimbazi.

    ReplyDelete
  3. Kuweni tayari kuwafukuza wa-congo wanaopiga box dar. Wacongo wote wataishabikia TP Mazembe.Uzalendo hautawashinda Wacongo ila watanzania tu.Anyway, Baada ya mpira wacongo watawaburudisha na nyimbo za kuipenda Tanzania na Batanzania.

    ReplyDelete
  4. mdau asante kwenye hii kitu

    ReplyDelete
  5. Matokeo ya simba na T.P.Mazembe vipi wadau?

    ReplyDelete
  6. Simba wamechabangwa tena robo dazani kwa mbili. Matokeo ya jumla ni nusu dazani kwa robo dazani.

    Waona mbali tuliliona hili. Simba walicheza sana mpira magazetini. Simba ilipoitoa Zamalek watu hawakuongeaongea. Walienda kuweka kambi sehemu yenye utulivu. Waliongeza nguvu kwenye benchi la ufundi kwa kupata watu waliokuwa wanawafahamu wapinzani wao (kocha wa makipa na Twalib Hilal). Waliweka kambi kwenye sehemu yenye hali ya hewa inayofanana fanana na Misri. Wakacheza uwanjani wakamng'oa bingwa mtetezi.

    Safari hii, kambi kwa ajili ya ugenini iliwekwa kwa manenomaneno zaidi. Mara Msumbiji, mara Kitwe, mara huko huko Kongo halafu ikaishia Arusha kwa siku mbili tatu. Baada ya kulala kwenye mechi ya kwanza, benchi la ufundi badala ya kujiimarisha kujiandaa kwa mechi ya marudiano lilipungua nguvu baada ya kocha mkuu kutokuwepo kwa siku kadhaa. Kocha Kibaden alipoenda kusaidia hakuenda kuendeleza programu ya kocha mkuu, alienda kuisaidia timu kwa namna aliyodhani inafaa.

    Baada ya yote hayo watu wakaishia kuongelea historia ya Zamalek. While Simba is living in history, Mazembe is making it. Enough said.

    ReplyDelete
  7. kwa ufupi game lilikuwa zuri ila tulijiandaa zaidi kiushirikina kuliko kisoka pia hatukuwa na mabeki kwani wapinzani wetu walikuwa wakiandaa mipango ilikuwa inafanikiwa kwangu mimi binafsi shukrani kwa samata na ochan na okwi angalau walikuwa uwanjani wakiwa na mpira walikuwa na uwezo wa kufanya lolote tena kwa kujiamini ila nadhani mvua pia nayo imetibua kidogoo na uzalendo ZEROO na hauzuiliki kwa kweli kaseja leo alikuwa mkimya mnoo kwa kweli nae kwa upande mmoja amechangia ila ndio hali halisi ila tukubali jamaa wako vizuri na wanamalengo kwa ufupi ndio hivyo tena jamaa wangu wangu Uk tumeumia

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...