Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Ukanda Maalumu wa Uwekezaji (EPZA) Dk. Adelhelm Meru (Kushoto) akizungumza na waandishi Dar es Salaam jana kuhusu mkutano wa pili wa shirikisho la Maeneo huru ya Uwekezaji Afrika utakaofanyika Dar es Salaam mwezi Mei 11-13 mwaka huu

Tanzania inatarajia kuwa mwenyeji wa mkutano wa uwekezaji wa kimataifa utakao fanyika jijini dare s salaam kuanzia Mei 11 hadi 13 mwaka huu.

Akizungumza na na waandishi wa habari jijini jana Mkurugenzi Mkuu wa kanda ya uwekezaji Tanzania (EPZA) Dk Adelhem Meru, alisema pamoja na Tanzania kuwa mgeni katika kanda huru za uwekezaji duniani, ime onyesha mafanikio na kupewa heshima ya kuwa mwenyeji mkutano huo.

Tuna tarajia kupata washiriki na wa taalamu kutoka mataifa mbalimbali ambao wamefanikiwa na kupiga hatua kiuchumi kupitia fursa huru za uwekezaji na wegeni wengine watatoka Benki ya dunia alisema Dk Meru

Kwa mujibu wa mkurugenzi huyo wa EPZA watoa mada katika mkutano huo Alberto Castronovo ambaye ni mwakilishi wa ukanda huru wa uwekezaji duniani kutoka Italia, Mkurugenzi mkuu wa REPOA Profesa Samweli Wangwe, Thomas Farile kutoka Benki ya dunia wataalam kutoka china Africa na Malaysia.

Lengo la mkutano huu ni kubadilishana uzoefu na utaalamu tunataka kujua wenzetu wamefanikiwaje katika fursa huru ya uwekezaji hadi kufikia kiwango cha juu katika uchumi, tunatakiwa kujifunza kutoka kwa wataalamu hao, kutanua nafasi ya uwekezaji na jinsi ya kuimarisha uongozi tunatumaini tutapata majibu ya pamoja yatakayo saidia kukuza na kuendeleza uwekezaji Barani Afrika.

Alisema pia Mkutano huo utafunguliwa na Waziri Mkuu Mizengo Pinda

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...