Ankal,
Naandika email hii kwa masikitiko makubwa kwa wizi unaoendelea mlimani city. This past Friday I was with 3 friends at samaki x2, after few drinks we dicided to call it a day at around 11 pm, wote tulikuta tumeibiwa site mirror za kushoto, except me was driving a BMW X5 ambapo nilikuta site mirror imevinjika into 4 pieces maana its not easy kuipachua.
I have been reading from your blog kuhusu wizi wa mlimani city but I think improvement will come from boycotts. Please any one reading this email let's stop from going to bars at Mlimani city and this will make owners raise a flag against management and changes will come positively.
Honestly mimi sitaenda tena pale for life.
Mdau wa Globu ya Jamii
Sent from my BlackBerry® smartphone from Vodacom


"...except me was driving a BMW X5..." What is the point of mentioning this? Why don't you go ahead and mention what your buddies were driving too...crap!! Kama unataka kusema kuna wizi Mlimani City, basi sema, siyo kutuambia story za nani alikuwa na X5, who cares?
ReplyDeleteMdau pole sana
ReplyDeleteLakini kiingereza chako kama cha mtoto wa shule ya msingi shule za KAYUMBA, siku nyingine andika kwa kiswahili ili usijiaibishe. au usichanganye lugha inawezekana kikanyooka-
Ndimi
Mdau nisiejua kiingereza
Ndo maana umeibiwa...umekuja hapa kutamba tu...halafu unataka watu wa boycott kwani ni wateja wote wanaoendesha magari?
ReplyDeleteNawapongeza hawa wezi na waendelee kuwafundisha adabu maana mmzidi na ulevi wa pombe hadi usiku wa manane. Matokeo yake ni ajali za kila siku zinazosababishwa na walevi kwa raia wasiokuwa na hatia.
ReplyDeleteBongo Tambarare...wa Sue hao Mlimani City kwani wamekuharibia hiyo X5 yako...hopefully sio ya UFISADI!!
ReplyDeleteWa-Tz bwana!! mhh..kizuri kipondwe...kibaya kipondwe..!! ujumbe umefika lakini! yeye alitaka kusema kuwa gari yake ni ya ki-falme siyo rahisi kuiba kioo!!
ReplyDeleteNamuunga mkono mdau hapo juu,ni vyema kutumia lugha ya taifa kama ngeli haijatulia.Ni aibu kuandika kama mtoto wa shule.
ReplyDeleteMdau kaibiwa lazima alalamike kwa kitendo hicho. Watanzania wengi hawawezi kumiliki BMW X5 hususan ikiwa mpya. Wezi wengi hulenga kuiba vitu vya magari. Shabaha yao kubwa ni vioo, "power windows", "radio/cd player" na kama utaacha kitu kama simu au mkoba basi wakotayari wavunje kioo ili wachukue kilichokuwemo ndani. Kibaya zaidi wapita njia wakimuona mwizi au baada ya wizi kufanyika huwa wanafurahia kwani wanaamini kuwa wenye magari ni mafisadi!!
ReplyDeleteWaungwana wa 2 hapo juu nawaunga mkono kabisaaa huyu jamaa sijui kajifunzia wapi kingereza.....ebana wacha uswangishi andika kiswahili maana english hujui kabisaa, rudi shule na acha ubishoo eti nilikuwa na drive X5 nani amekuuliza?? ushamba huo, na ukisema kwamba huendi tena Mlimani City unafikiria ndio itafungwa kwasababu yako?? Bongo uwizi uko kokote....
ReplyDeleteAcha ushamba...
Duh, hawa jamaa walikuwa wanakunywa soft drinks au masanga.kwa mtazamao wangu itakuwa masanga.harafu wanaendesha magari.mhhh.mungu ibariki Tanzania
ReplyDeletemdau Norway
Ukienda kunywa pombe usiendeshe..acha usafiri wako nyumbani
ReplyDeletehahahahahaahahahaaaa x5 na blackberry na kuchanganya lugha inaonyesha wazi jinsi ulivyokua limbukeni..ingeibiwa hiyo x5 naona mpaka bei ungeandika na ilikotoka.daah jaman dunian kuna mambo.
ReplyDeleteKama mwendo mdundo wenyewe ndio huo, wizi hautakaa uishe tz. Yaani mwenzenu anatoa kilio chake ili kusaidia wengine, nyie mnamkashifu kwa lugha aliyotumia. Kwani nani aliyezaliwa na lugha? Au nyie ndio wezi wa mlimani city nini? Mlisubiri aandike ili muwe na hoja. Acheni ufala ndg zanguni mdau wa1+2, siri hiyo mnaijua na ipo siku mtavalishwa matairi na kuchomwa moto. Mdau ughaibuni
ReplyDeleteBongo tumekwisha kwani watu hawaongei lugha zetu, naona hata mawaziri wanatoa hotuba kwa kiingereza. Ni aibu, kila kitu ni kizungu. Yaani hata makocha wa timu kubwa za taifa si WaTanzania, tunatia huruma jamani!! Ingawa tuna macho lakini hatuoni, uzalendo umekwisha. Tulizoea kuwatania wa Kenya, kwamba Kiswahili chao kibovu, sasa na sisi tunaongea hivyo hivyo. Ama kweli "lugha gongana"
ReplyDeleteWaswahili bwana. Ohh "......except me was driving BMW X5" jamani hayo majigambo nadhani ni mambo ya inye nshomile! Utakuta kigali chenyewe ki-starlet ndiyo maana hata wezi walishindwa kutoa site mirror zake maana ni mbovu halafu leo unatutambia BMW?? Kingereza chanyewe kibovu kuliko maelezo. Hizi shule za kata naona ndiyo zinaua kabisa elimu ya Tanzania.
ReplyDeleteMdau
Hiyo ndiyo hali halisi. Lazima mgawane na wasionacho. Wewe unaendesha BMW kuna mwingine angepata milo mitatu kama angeuza kioo cha hiyo BMW. Haikwepeki hiyo.
ReplyDeleteAu la sivyo nunua kinywaji chako kanywe nyumbani pengine utaweza kuepuka hali hii.
Halafu English ya msomi hiyo... Mbona kazi? Hata kama ulikua na jazba na haraka ya kuandika hii habari English yako imeka kichina kweli.
ReplyDeleteKwanza nyie wenye magari ambao mna kunywa pombe halafu mnaendesha magari ni hatari kwa maisha ya watu.
ReplyDeleteNaomba jeshi la Polisi liwe linapitia ktk viota vya unywaji pombe na kuwakamata wale wote waliopata kilevi ambayo wanataka kuendesha vyombo vya moto kama magari au pikipiki na kuwafikisha mahakamani haraka na kuwapa adhabu kali ya faini na kupigwa marufuku kuendesha gari kwa miaka mitano.
Nawashauri wale waendeshao vyombo vya moto kama wanaenda sehemu kupata pombe basi wayaache magari yao nyumbani na kukodisha taxi au bajaj ili kuepusha ajali.
Mdau
Mlimani City.
Mijitu mingine bana....eti "except me was driving a BMW X5"....now we know you are loaded.
ReplyDeleteAngekuwepo Mpoki angekuuliza Kiingereza kinakusaidia nini? si uongee tu Kiswahili ueleweke lol natania, hicho jamani ndio lugha ya kiingereza ya mtaani kama ambavyo kuna lugha ya blogu hapa ankal akiandika kuna watu wanambondea hajui kiswahili au kiingereza kwa sio wabeba maboski na majirani za wanugu (wamarekani weusi) hatuoni kama kachapia inangawa kwa mliosoma Cambridge no class ahead mtaona kabofoa mbayaaa. Alichosema kuna wezi na wizi uangaliwe au wateja wagomee huduma hadi ulunzi uimarishwe yanini malumbano??
ReplyDeleteUshauri wa bure!!! plese Mlimani City weka mabasi ya kisasa kwa wateja wa kila kona. Wale wa Mbezi mpaka Tegeta wape yao, wa Kimara mpaka Mbezi juu weka yao, wa City center weka hata tatu ili kuzuia watu kuendesha wamelewa. Wanaweza kuegesha mahali salama kwenye vituo au majumba ya watu karibu na kituo cha mabasi hayo ili wakitoka hapo waende nyumbani.
ReplyDeleteWezi ni wezi tu wapo dunia nzima si Dar hata NY wapo ila wizi unategemea mahitaji ya mahali. Mwizi wa Dar anadhani kioo ni pesa ingawa mwizi wa London anaweza kudhani radio yenye TV screen ni bora zaidi hivyo tusilaumu mji mmoja.
Swala la yeyen kusema BMW sijui hilo si kosa wewe unaweza kudhani kajikweza ila kwa yeye sababu analinedesha muda wote na ana uwezo wa kulinunua akaona sawa. Hii ni sawa na wewe kusikia mtu anasema kuwa jana kwa mara ya kwanza mwaka huu nimekula nyama ya ng'ombe wakati wewe ni kila siku ukamshangaa.
Siyo kila mwenye sangingi ni fisadi, jamani njoo majuu muone jinsi watu wanavyoteseka kutafuta pesa. Hawana lunch time kama nyinyi hawana likizo ya mwezi kama nyinyi. Likizo kama US ni wiki mbili tu kwa mwaka na si kwa baadhi ya watu bali kila mtu hivyo ukisikia nchi tajiri, si sababu ya bahati ila ni juhudi na maarifa. Kubeza mwenzio ni kukosa uungwana au tuseme Mbichi hizo!!!!!
mliocomment number 1+2 ni wapumbavu na ni haters..no wonder ni wazee wa daladala..mkiona mbongo kapiga hatua mnamind...ndio ni X5 yakwake na ana rights ya kuitaja..unajua price ya side mirror ya x5 wajinga nyie....kazi udeiwaka tu
ReplyDeleteAwe limbukeni au la, awe mpenda sifa au la....nadhani alichokuwa anajaribu kukiwakilisha ni uharibifu unaoendelea kila siku pale mlimani city.tusiwe tu watu wa kupenda kuponda hata pasipo na sababu...je angetaja gari yake ilikuwa suzuki maruti mgepiga kelele? na hizi ni element za wivu wa kipumbavu...na hata kama alienda kulewa, kati yenu hapo juu mlioponda ni nani mtakatifu na ajitokeze?
ReplyDeleteSitaki kuingia sana huko, maana ntaishia kua kama nyinyi...kitu cha msingi hapa ilikuwa ni amoni ya namna ya kuukabili wizi huu katika mameneo yale na mengineo ya hapa mjini. Mcity watu huibiwa usiku na mchana kweupe na kuna walinzi pale, si watu wote wanaoenda samaki samaki tu, wengine huenda kufanya manunuzi katika maduka yaliyopo pale, wengine huenda na familia zao kuangalia sinema, wengine huenda na watoto zao kama outing pale na wengine hufanya makutano ya kuzungumzia biashara zao, kazi zao na kadhalika..wote hawa ni waathirika wa hawa vibaka.... inaaminika kuwa angalau matukio mawili ya magari kuvunjwa ama kuibiwa huripotiwa kila siku pale...kwa wale ambao yalishawakuta wanaweza kuelewa ni uchungu kiasi gani anaoupata mtu anapofanyiwa hivi..
sasa sielewi kwanini mtu huyo hapo juu anapoelezea tukio linaloweza kuwa na manufaa kwetu sote kama wakazi wa jiji la dar es salaam tunaanza kuchambua ujinga wake badala ya kujadili point ya msingi aliyoiwakilisha. humu ndani naamini kabisa kuna mawakili, kuna wanataaluma waliosomea mambo ya usalama, na kwa ujumla wetu naamini wengi wetu tuna busara... nilitegemea maoni yetu yangekuwa katika mrengo wa ushauri chanya zaidi kwa manufaa ya wengi badala ya kuanza kuzungumzia kiingereza cha huyu mtu, na kebehi za kumtukana kwa kuwa amesema kuwa anaendesha X5....kama anaamini gari yake ni ngumu kuondoka na kioo kwanini asiisifie? inakupunguzia nini wewe ku ignore mbwembwe zake na kujadili kile kitu cha msingi katikati ya pumba zake?
hatutakuja kuendelea na wala hatuwezi kunyooshea vidole mafisadi kama tutaendelea na uvivu wa kufikiri. tunakuwa attracted kuzungumzia vitu dhaifu sana na kuacha vile vya msingi..tubadilike
Nikiwa sikubaliani na tabia ya jamaa ya kukaa baa mpaka saa hizo mbaya,lakini kwa upande mwingine nampa pole yeye na wenzake kwa kuibiwa vifaa vyao vya magari.Ni kweli wizi wa vifaa vya magari na hata magari yenyewe siku hizi umeshamiri maeneo ya mlimani city hata chuo kikuu na maeneo jirani.Kwa hiyo ni bora tukachukua tahadhari.
ReplyDeletePili,watanzania tuache ushamba.Yaani mtu kuchanganya lugha kidogo mshaanza kumkatisha tamaa.Kama hamujui Kiingereza si muende mkatafute kozi?Kisa hujaelewa unaponda.Badala ya kutazama zaidi ujumbe mnakalia majungu.Ndo maana nchi haiendelei kwa sababu ina watu wengi wenye uvivu wa kufikiri na ufinyu wa mawazo.Yaani mtu akipiga hatua moja mbele,watu wanajitahidi kumrudisha nyuma hatua kumi.Watanzania tubadilike na tupunguze majungu kwenye mambo ya msingi.Sasa Kiingereza cha shule ya msingi kiko wapi?Au kwa sababu nyie hiyo bmw hamna?Acheni majungu.Kwa mara nyingine,pole sana kaka ila uache ulevi na tabia za kukaa baa mpaka mida hiyo mibaya.Na kwa wengine,badala ya kuzama zaidi kwenye kukagua lugha jambo ambalo halitusaidii hapa,ni bora muangalie zaidi ujumbe na huo ndo uungwana na kupeana moyo.
POLE SANA MDAU NAJUA MAUMIVU YAKE MAANA SISI YAMESHATUPATA NA PIA WENGI WAMEPATA MATATIZO HAYO MIEZI MIWILI AU MITATU KAMA SIKOSEI PALE VODACOM MFANYAKAZI ALIIBIWA GARI YAKE KWA KWELI INATIA UCHUNGU UKIFIKIRIA UTAKUTA HUYU KAKA AMEJITAHIDI KUTAFUTA HELA YAKE KWA SHIDA SN LABDA HATA KUBEBA BOX AMEKUJA NYUMBANI NAAMA TZ KUANZA MAISHA ANAKUTANA NA VITU KAMA HIVI.SISI TULIKUWA TUMEINGIA SHOPRITE DAK 10 NYINGI VIOO HAKUNA TENA UKIBANANISHA MAGARI NDIO WANAPENDA MLIMANI CITY MIE SIENDAGI SIKU HIZI
ReplyDeleteWatanzania bwana huyu jamaa ameibiwa na anaifamisha jamii lakini mnamkandia kwa kifupi nimefatilia sana kuhusu mlimani city kwakweli uongozi wa ile center inatakiwa ibebe lawama zote la sovyo wote wafukuzwe!
ReplyDeleteWote waliomkandia mshikaji ni walevi nao! Mmesikia kuwa wizi wa mlimani city uko mchana hata usiku, hauchagui ulikaa baa au ulikuwa unafanya manunuzi. Ninyi mnaokandia Lugha ya mwenzenu ndo wapumbavu kabisa hamna hekima ndani yenu, mbona jamii za nchi nyingine zinatumia lugha zaidi ya 3 au zaidi ili mradi wadau wanaelewa, kwetu mtu akibofoa kidogo inakuwa shida, watu maarufu km akina Drogba wanahojiwa kila siku na wanabofoa kiingereza "mbona watu hawacheki" ila akina Kanumba wakibofoa watu wanacheka hadi wanagaagaa chini, pumbafu zenu mnaocheka, nyote mmepungukiwa na akili!!. Uharibifu na wizi uko Dar na maeneo mengine ya Tanzania, hivi kweli kibaka aliyeiba hivyo vifaa vya gari akitokea akasoma ujumbe mnaoandika humu tabia yake itabadilika kweli au atazidi kuwa kibaka!! Watanzania wengi nawajua wana wivu sana wa maendeleo, ndo maana tumekuwa wabinafsi, mtu aliyekuzidi kipato akipata shida si rahisi umsaidie maana unaona bora naye amepata shida. Hebu badilikeni Watanzania. Mlimani city imarisheni ulinzi, wekeni kamera eneo km hilo muhimu, ili hata vibaka wakijua angalau kuna kamera eneo hilo wataogopa kuibia watu. Ninyi msiopenda maendeleo anzeni kupenda maendeleo ya wenzenu, halafu kama huna zuri la kuongea kwenye maoni yako kwa nini upoteze muda kuandika? Tumia muda wako vizuri usipoteze kuandika utani na ujinga, najua machizi wapo lakini..Mungu awasaidie tu msiendelee kuwa machizi. Kwa mwendo huu Tanzania haitapiga hatua ya maendeleo..maana mtu akiibiwa watu wanashangilia, hadi mtu afe ndo wapumbavu haohao wanajifanya wana huruma..na kumimina pole nyiingi...je mali yake? Ndiyo maana hatuwezi kufanya mabadiliko ya haki nchini kwa sababu ya ubinafsi, wengine wanashirikiana hata kufanya maandamano angalau mishahara ipande, au kushinikiza kitu cha maendeleo ila Watz kila mtu amekuwa mbinafsi, mambo yake yakikubali anasahau cha nduguye. Yaani najuta kuzaliwa Tanzania, hakuna amani kabisa, unaweza kujeruhiwa na vibaka au kuuawa na jambazi wakati wowote, mwenzio akashukuru!! Acheni ujinga Watanzania badilikeni!
ReplyDeleteMdau wa 06:35 anayesema BMW X5 mtu yeyote anamiliki Ughaibuni kwa sababu wanafanya kazi kwa bidii. Hiyo sio kweli. Ughaibuni watu wanamiliki magari hata kwa mbeba box ni kwa sababu ya MIKOPO tu. Na kama wataambiwa wachange pesa kwanza mpaka zitimie wengi wakuwa kama bongo tu. Sasa hivi kuna watu wanamiliki hayo magari hapa bongo baada ya mabenki kuanza kutoa mikopo. Lakini hata hivyo kuna kiana fulani cha ufisadi kwa baadhi ya hao waliopata mikopo ya magari.
ReplyDeleteMkubali msikubali bongo ufisadi upo karibia kwa kila mtu ni nafasi tu wengi wanaikosa. Ana BMW yake hata kama kapata kifisadi msimlaumu yeye walaumuni waliowekwa kusimamia sheria kwani walikuwa wamelala wakati anaiba. Na jamii nayo imelala kwani nguvu ya umma ingeweza kukemea ufisadi kama waliopewa hiyo dhamana wameshindwa.
ReplyDeleteWahaya bwana, eti "except me was driving a BMW X5". St Kayumba.
ReplyDeletewtz bwana wanachekesha sana mtu analeta kero yake ya wizi watu wengine wanaanza kumjaji na gari yake watu wengine wanaonekana jinsi walivyo na wivu na mali za wenzao sijui hizi roho za chuki na wivu zitawasaidia nini jitahidi nawewe upate yako kama huna chakuchangia kaa kimya
ReplyDeletewhat is "Site Mirror"?
ReplyDeleteAlimaanisha "side mirror" ulishaelewa bana. Dah utadhani hapa shule!!
DeleteVioo vyenu sasa viko kwenye maduka ya spare za magari. Lakini usiingie duka. Uliza kijana yeyote aliyeko nje ukimkuta, yeye huyu huwa analetewa vioo vilivyoibiwa auze. Pia ushauri mwengine nenda kwa wakata vioo wakutengezee kioo cha kawaida. Ni kama Sh. 10000, kitakuwa hakiibiwi tena. Binadamu yeyote anawivu na choyo. Huku Ughaibuni ukiwa mtu mweusi unaendesha gari zuri kama hilo X5 basi jirani yako atalichuna rangi kusudi, polisi watakusimamisha kila wanapokuona, mfanyakazi mwezio atapiga simu uhamiaji kutoa taarifa kwamba anawasiwasi na mfanyakazi mmoja kuwa mhamiaji haramu. Hayo ni mambo ya kawaida kwa binadamu.
ReplyDeletewewe unayesema watu wa ughaibuni wanamiliki magari kwa sababu ya mikopo tu una uhakika?? tena bila aibu umeweka capital letters!dayuum,nahisi ulikua deported ndo maana una hasira..hahaha, mie nnamiliki gari na nilinunua by CASH! UKO HAPO? siku nyingine usirudie kugeneralize vitu usivyovijua...
ReplyDeleteNilichokiona hapa kwa wengi waliochangia mada ni wivu tuu na si kingine, tufanye basi mdau kakosea kuitaja hiyo gari yake, ila ujumbe si umefika? hata wewe uliemshambulia kwa kuongea kiingereza kibovu kutokana na "nyie" mliosema hivyo utakuta wewe mwenyewe hukijui hicho kiingereza, ebu jamani Watanzania tubadilike, namna hii sidhani km tutakujakuendelea
ReplyDeleteIn general naona kuna makosa pande zote mbili mtoa mada na wachangiaji. Mtoa mada ni kweli hakuwa na aja ya kutuambia gari anayomiliki lasivyo ange tueleza pia magari mengine pia. Kwa wachangiaji LUGHA sio ishu hapa sehemu nyingine duniani icho Kingereza hawakijui na achilia mbali kukiongea. Norway kwa mfano vitabu na magazeti mengi ni kinorway. Hata sehemu muhimu kama supermarket label zote zipo kikwao so acheni ushamba. Kuna notion eti mtu akiongea kingereza basi amesoma nendeni hapa uganda tu ama kenya wanaoudumia baa wanatema kingereza kama kawa. In short hizi ni Lugha tu.
ReplyDeleteMdau ninachoweza kumkosoa alikuwa wapi siku zote wakati wengine wanalia wameibiwa? Leo yeye yamemkuta ndo anapaza sauti. Sasa ni wakati wakuchukua hatua. Leo ni X 5 kesho Bajaj yangu watavua matairi. Kwangu mie thamani ya tairi ya Bajaj inaweza nichukua miezi sita kununua. Jamani wakati umefika wote kwa ujumla wetu tufanye kitu cha kueleweka kushinikiza uongozi kufanya liwezekanalo ili mambo yawe mswano.
Haterzzz!!!! watanzania tubadilike jamani, mlimani city kumeozaa. Napata hisia tofauti hapa kwa waliomponda jamaa uelewa wao ni mdogo sana. Poleeeee!!! ila ujumbe umefika.
ReplyDeleteJamani watanzania tunatia aibu ndio maana hatuendelei, tutabaki kutawaliwa na kuwa nyuma kwa sababu ya mitazamo yetu hasi!! Mtanzania mwenzetu katushirikisha shida iliyompata kwa upendo kabisa ili kututahadharisha tusije tukaumia kama yeye, badala ya kupokea ujumbe tunashambulia kwa vitu visivyo na msingi wala tija!!! Kwa mtazamo huu bado tunasafari ndefu ya uwelewa wa mambo, ikiwa jambo dogo kama hili tumeshindwa hata kumpa pole mwenzetu nasikitika kusema hao wenye mawazo hasi hawana tofauti na wale wanaoibia abiria mara wapatapo ajili barabarani! Mungu atusamehe watanzania, ndugu uliyeibiwa pole sana asante kwa upendo wako wa kututahadharisha kuwa makini mara tuendapo maeneo hayo. Ubarikiwe na wasamehe hao watanzania wenye mawazo hasi maana hawajui watendalo.
ReplyDeleteHuu kweli ni ushamba. wote mliomkandia mshikaji hamjaenda shule, manake hujaelewa nia na madhumuni ya hii message ila unaenda kukosoa maandishi. The point ni kukomesha wizi, au kwa sababu nyie hamna gari ndio mnaponda. yeye kaeleza X5 ili ijulikane kama ni ngumu kuiba sight mirror yake. Kuweni na busara kidogo japo. Mnakuwa kama mnatumia sehemu ya makalio yenu kufikiria.
ReplyDeleteTuache kwenda Mlimani City ndio watajua umuhimu wa ulinzi.
Usidhani unanunua kitu pale ndani ya Mlimani City bila kulipishwa security. Kila bidhaa unayonunua pale tayari in portion ya ulinzi unayolipia.
Wabongo kuweni wastaarabu.
Mdau from Bongo
JOBLESS NI WENGI TANZANIA HIVYO FRUSTRATION ZINASABABISHA COMMENTS KWENYE BLOG ZISIZOKUWA NA MAANA
ReplyDeleteKUHUSU WIZI WA VIFAA VYA MAGATI NI TATIZO SUGU LA SEHEMU ZOTE YENYE MAGARI YALIOGESHWA. AKILI KIDOGO ITAKUAMBIA KWAMBA MLIMANI CITY SIO MALI ZA SERIKALI; NA HUDUMA ZA PACKING HAZILIPIWI. WAO HAWAWEZI NA WASITARAJIWE KAMWE WATA KU-GUARANTEE USALAMA WA GARI LAKO. HATA SUPERMARKET ZA ULAYA HATA KEMPINSKI, HATA KANISANI, HATA MOVENPICK, HATA ROSE GARDEN HAKUNA GUARANTEE HATA KAMA UTALIPIA PACKING - SIO GUARANTEE YA USALAMA, BALI NI GHARAMA ZA SEHEMU TU YA KUPACK. NI VIGUMU KIBIASHARA NA KISHERIA KU-GUARANTEE USALAMA WA GARI LILIPAKIWA KWA MAANA MADEREVA WENYEWE WANAWEZA KUWA NDIO VIBAKA. NA JE WEWE MWENYE X5 ULILIPIA HUDUMA ZA ULINZI PALE MLIMANI CITY? AU ULIFIKIRI UKO POLICE CUSTODY? PIA ULISOMA NYUMA YA KADI YA KUPITA GETINI? IMEANDIKWA - PARK AT OWNERS RISK.
SOLUTION/MAPENDEKEZO - MLIMANI CITY WAFIKIRIE KUANZA KU-CHAGI PARKING FEES YA SHS 5,000 KWA SAA ILI WAONGEZE WALINZI WENGI NA KUWEKA SECURITY CAMERA. NB: HATA WAKIFANYA HIVYO BADO ITAKUWA PARKING AT OWNERS RISK - KWANI NDIO MFUMO WA KIMATAIFA UTAKE USITAKE; KUGOMEA KWENDA MLIMANI CITY - WEWE AKILI YA KITOTO SAANA GOMA WEWE; WENZAKO WATAENDA NA HAKUTAKUWA NA KUSHUKA BIASHARA.
ALEX BURA DAR
Watu noma sana, yaani hii blog ya anko michuzi tunaiheshimu kwa habari moto moto tunayopata kila siku alafu nyie mnaifanya kama blog ya wahuni. sio freshi kuweni wataarabu.
ReplyDeleteAnko Michuzi, Nadhani baadhi ya comments uwe una ignore kuliko kutuharibia hii blog yetu.
Mdau from Bongo
ALEX BURA
ReplyDeleteCard ya Mlimani City haijaandikwa "parking at owner's risk"
Tunapopata huduma yoyote pale mlimani City basi tujue ni lazima kiasi cha fedha tumelipishwa ambayo ni kwa ajili ya ulinzi.
hata kama hiyo ni private property lakini inaweza kuboreshwa. Wewe Supermarket za ulaya usifananishe na huku. kule hakuna wizi wa vioo vya magari. usiwe unasema ila uende kwanza ukaone hali halisi before you write on this free of charge blog.
Wizi ni problem kwahiyo tushirikiane kuzuia. Kwani ukimwona mwizi anaiba hata kama sio mali yako unapaswa kumzuia lasivyo na wewe umeshiriki.
Mdau from Bongo.
POLE KAKA ULIYE IBIWA BUT HUYO MWIZI ALIJUA KAMA UNAUWEZO WA KUMILIKI X5 LAZIMA UTAWEZA NUNUA HYO SIDE MIRROR NDO MAANA AKAAMUA KUICHUKUA
ReplyDeletePole sana mdau uliyeibiwa. Kwanza, kwa wote waliokuponda kwa kubofoa english, wao nao wamebofoa, kiswahili walichotumia hakikunyooka. Kuhusu kutaja aina ya gari, mimi sioni tatizo, cha msingi ujumbe umefika kuwa Mlimani City wizi umezidi. Zifanyike juhudi za ziada kupunguza hali ya wizi uliokithiri pale. Kwa kweli inaogopesha hata kwenda pale kama huna mtu wa kubaki kwenye gari kuchunga.
ReplyDeletewewe unayejibu kwa hasira inawezekana ndio uliyeleta hii habari, kwanza jamaa anakosa la kuendesha akiwa mlevi, anawezaje kulewa hadi saa5 usiku halafu akaendeshe gari? wezi kweli wapo na inatakiwa uongozi uweke ulinzi ili kulinda hadhi ya sehehu ile. inasikitisha kuona watu wanashindwa kwenda na usafiri binafsi kwa kuogopa wezi ambao wanaweza kudhibitiwa.
ReplyDeletehata mimi nina ndugu yan anmilika BMW ya zamani, lakini vioo vyake havitoki kirahisi kama corolla au toyota, ndio maana mtoa mada akataja aina ya gari kuonyesha msisitizo. Watu wasiohafahamu wakawa na tafsiri tofauti. Pia gari kama X5 huwa haziibiwi vioo kwa Tanzania maana sio nyingi, sawa na hummer, escalade, opel utamuuzia nani? nafikiri ndo maana mtoa mada akatja aina ya gari ili watu wafahamu lengo la wezi ni uharibifu namuunga mkono siendi pale mlimani city siku nyingi
ReplyDeleteMbona kuna askari pale mlimani city! Huwa wanafanya kazi gani hasa pale juu ya vile vijibanda? Na inaonekana watu wanaoharibikawa hawana pa kwenda kuripoti.Au!
ReplyDeleteNYIE WATU KAMA SITA HIVI MLIOCOMMENT MWANZONI NAWASHANGAA SANA. BINAFSI SINA PESA NA HATA GARI SINA, ILA KIUKWELI MMEMPONDA ALIYETOA MADA KWASABABU ZA KIWIVU ZAIDI.
ReplyDeleteJAMANI WE HAVE DIFFERENT BACKGROUNDS, LETS LEARN TO BEHAVE SIO TUNAKUA KAMA WATU WA KIBARAZANI BWANA. ULISHAWAHI JIULIZA KWANINI WATU WANAPENDA KUVAA VIZURI? NI ILI TUONEKANE TUMEVAA VIZURI, THEN TUNAJISKIA VIZURI, HIYO NDO KUWA HUMAN. MTOA MAADA INAWEZEKANA ANAJISIFU NA BIMA YAKE. ACHENI MAJUNGU YASIYO YA MSINGI, PROBABLY BADO WADOGO HATA HAMUELEWI.
INAMAANA BLACKBERRY PIA NI KUJISIFU?? GROW UP!!
Watanzania utawaina tu na mimi nikiwemo. Huyu kaka alijaribu kueleza jinsi alivyoibiwa na kuweka sawa jamii. Ghafla matusi sababu kataja X5. Keep in mind alivyimaliza kutaja hiyo BMW, akasema kuwa walishindwa kuimba side mirror yake. Ila ilivunjwa. Sasa matusi ya nini watanzania???? Kwa jinsi hiyo hatutafika. Wengine eti mbona huelezi hawa wenzako walikuwa wakiendesha nn. Hivi tumekuwaje watanzania??? Nina hakika angetaja bajaji au piki piki badala ya BMW, wote tungekuwa kimya. Tuache uchoyo wa umaskini. Msikilizeni kaka. Kaibiwa basi. Hivyo kuweni makini. Na wale wanaoendesha gari za kifahari, nao wanaweza kuibiwa au kuingia hasara kwa kuvunjiwa mali zao hata kama ni vigumu kunyofoa mali hizo. Hiyo ndo point. Acheni kuoneana wivu watanzania. Huo ni uchawi wa roho. Na hii ni sehemu ya public hivyo kama wewe umelaaniwa, usije kuandika ujinga wowote hapa
ReplyDelete