Mshindi wa kwanza wa taji la Vodacom Miss Dar City Center Alexia William akiwa kwenye picha ya pamoja na mshindi wa pili Salha Israel (Kushoto) na mshindi wa tatu Jenifer Kalokola mara baada ya kutangazwa washindi. Shindano hilo lilifanyika mwishoni mwa wiki jijini Dares salaam.
Meya wa Manispaa ya Ilala Jerry Slaa akimkabidhi mshindi wa kwanza wa taji la Vodacom Miss Dar City Center Alexia William zawadi ya shilingi Milioni 1/- zilizotolewa na waandaaji wa shindano hilo. Anayeshuhudia ni mke wa Meya Slaa, shindano hilo lilifanyika mwishoni mwa wiki jijini Dares salaam.
Vodacom Miss Dar City Center Alexia William akipunga mkono mara baada ya kutawazwa kuwa mlimbwende wa kanda hiyo. Wengine kutoka kulia kwake ni mshindi wa pili Salha Israel, wa pili kutoka kulia ni mshindi wa tatu Jenifer Kalokola, wa kwanza kutoka kushoto ni mshindi wa nne Maryvine Kenzia na kulia mshindi wa tano Lilian Paulo, shindano hilo lilifanyika mwishoni mwa wiki jijini Dares salaam.
Mkuu wa itifaki wa kamati ya Vodacom Miss Tanzania Albert Makoye, Mtaalam wa Masuala ya Habari wa Vodacom Tanzania Matina Nkurlu na Afisa Udhamini wa kampuni hiyo Ibrahim Kaude wakisoma ujumbe wenye jina la mshindi wa Miss University (UDSM) Chiaru Masonobo ili walitangaze kwenye shindano la Vodacom Miss Dar City Center lililofanyika mwishoni mwa wiki jijini Dar es Saalam.

Hivi hizi nywele ni zao au ndo pendezesha tu! Hii tunadanganyana jamani Beauty is naturally in and out. mwekeni vile vile alivyo tumuone avae kikawaida bila ya kujirembesha, yaani kama katoka kijijini. Mtoto wa kimasai ni mzuri bila ya kuweka make up na nywele za kafa ulaya. Niiteni mshamba au sipendi maendeleo lakini mhhhhhh!
ReplyDeleteAaaah chaurembo wa ukweli ni Flaviana matata tuu model wa ukweli no feki feki hair yeye na upara wake tuu wa kibantu na uback beauty wake na yuko bomba kichizi.. wazungu wanamkoma!
ReplyDeletemwanamke kujiamini bwana!