JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

MAKAMU WA RAIS DKT. MOHAMMED GHARIB BILAL KUWA MGENI RASMI KATIKA MAADHIMISHO YA SIKU YA MAZINGIRA DUNIANI

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Mohammed Gharib Bilal  leo anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika siku ya Mazingira Duniani inayoadhimishwa kitaifa mkoani Ruvuma katika mji wa Songea.

Makamu wa Rais Dkt Bilal anamwakilisha Rais Jakaya Kikwete katika maadhimisho hayo ambayo ujumbe wake Kimataifa ni MISITU NI TUNU YA ASILI. Kwa upande wa Tanzani moto ya siku hiyo kwa mwaka huu ni MIAKA 50 YA UHURU, PANDA MITI NA KUITUNZA: HIFADHI MAZINGIRA.

Katika maadhimisho hayo Makamu wa Rais anatarajia kuzungumzia hali ya Mazingira nchini kwa miaka 50 tangu uhuru, Mazingira ikiwa ni moja ya Idara/Wizara iliyochini ya Ofisi yake.

Sambamba na shughuli hiyo Makamu wa Rais atapata fursa ya kukagua mabanda mbalimbali katika Uwanja wa Majimaji ambapo pia atapata kusikia salamu maalum za Mkoa wa Ruvuma katika maadhimisho hayo ambayo yataambatana na ujumbe kutoka kwa Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais anayeshughulikia Mazingira Dkt. Terezya Huvisa.

Imetolewa na:
Boniphace Makene
Mwandishi wa Habari wa Makamu wa Rais
Mei 31, 2011

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 4 mpaka sasa

  1. AnonymousMay 31, 2011

    jumanne ya april mosi????

    ReplyDelete
  2. AnonymousMay 31, 2011

    Michuzi hiyo barua imekosewa, kesho sio jumanne April mosi....KESHO NI JUMATANO, JUNI MOSI. Waombea hao walioondaa hiyo barua wafanye marekebisho sasa hivi...wanapotosha watu

    ReplyDelete
  3. AnonymousMay 31, 2011

    Tangazo lina utata Michuzi, nadhani editor wako hajilipitia hili. Angalia tarehe.

    ReplyDelete
  4. AnonymousJune 01, 2011

    Angalia ni jinsi gani tulivyo makini katika utendaji wetu wa kazi. Jumanne april mosi na taarifa imetolewa tarehe 31 mei 2011. Kazi kwelikweli.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...