Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii Dkt Hadji Mponda akizungumza na wananchi wa wilaya ya Bagamoyo leo wakati wa maadhimisho ya Siku ya kutotumia Tumbaku duniani ambayo kitaifa yamefanyika katika viwanja vya shule ya msingi Majengo Bagamoyo. Pamoja na mambo mengine amesema serikali imeandaa mpango mkakati wa miaka 5 kwa lengo la kudhibiti matumizi bidhaa za tumbaku nchini.

Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii Dkt. Hadji Mponda (kulia) akipata maelezo kutoka kwa Bi. Rutgard Kagaruki mmoja wa wahamasishaji walio katika mapambano dhidi ya matumizi ya bidhaa za tumbaku nchini kutoka asasi ya kiraia inayopiga vita matumizi ya bidhaa za tumbaku nchini (Tanzania Tobacco Control Forum) wakati alipotembelea banda la maonyesho la asasi hiyo wilayani Bagamoyo leo.
Wataalam wa Afya kutoka Hospitali ya Wilaya ya Bagamoyo wakitoa huduma mbalimbali za Afya kwa Wananchi ikiwemo upimaji wa macho leo wakati wa maadhimisho ya Siku ya Kutotumia Tumbaku Duniani ambayo kitaifa yameadhimishwa leo wilayani Bagamoyo yakiongozwa na kauli mbiu isemayo “ MKATABA WA KIMATAIFA WA KUDHIBITI MATUMIZI YA TUMBAKU DUNIANI”
Baadhi ya Raia wa kigeni wakifuatilia matukio mbalimbali wakati wa maadhimisho ya Siku ya kutotumia Tumbaku Duniani ambayo kitaifa imefanyika leo wilayani Bagamoyo.
Wanafunzi kutoka shule ya Msingi Majengo iliyoko wilayani Bagamoyo wakifuatilia jumbe mbalimbali zilizokuwa zikitolewa wakati wa maadhimisho ya Siku ya kutotumia Tumbaku Duniani ambayo kitaifa imefanyika wilayani Bagamoyo.

Wanafunzi wa Chuo cha Sanaa Bagamoyo (TASuBA) wakiwasilisha ujumbe unaopiga vita matumizi ya bidhaa za tumbaku wakati wa maadhimisho ya Siku ya kutotumia tumbaku Duniani leo wilayani Bagamoyo.Picha na Aron Msigwa – MAELEZO.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 2 mpaka sasa

  1. AnonymousJune 01, 2011

    London School of Hygiene and Tropical Medicine, kwa ushirikiano na British High Commision wameandaa Dinner kwa watanzania waliomaliza chuoni hapo kesho saa 12 na nusu jioni pale Double Tree Hotel. Issa unakaribishwa sana, ili wenzetu waliomaliza shule ulaya na kung'ang'ania huko huko wapate kuona wenzao waliomaliza na kurudi nyumbani wana maisha gani?. Kwanza tulitumiwa form kujaza tupo wapi na tunafanya nini. Nilishangaa sana kuona wote tunahold post za juu kwenye wizara na International organisation mbalimbali. Chakula ni bure nawe kama mgeni unakaribishwa ili utoe kwenye globu yako yenye kuwafikia wengi huko nje. Mgeni rasmi ni Balozi wa UK hapa nchini. Tushirikianekuwatia hamasa ndugu zetu wenye degree, master and PhD holders lakini bado wanang'ang'ana na kazi zisizofaa ulya na marekani. Mungu bariki Tanzani, Mungu saidia wasomi wetu warudi nyumbani.

    ReplyDelete
  2. AnonymousJune 01, 2011

    Hivi ule mpango wa kuuza TUMBAKU Iran na wapi sijui bado upo?

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...