Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohamed Gharib Bilal, akifunua kitambaa ikiwa ni ishara ya kuwekajiwe la msingi katika , Shule ya Msingi Simai iliyopo Kijiji cha Wingwi Mapofu, Wilaya ya Micheweni Mkoa wa Kaskazini Pemba, wakati akiwa kwenye Ziara yake ya kukagua miradi ya maendeleo katika Miikoa ya Kusini na Kaskazini Pemba leo Mei 17.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohamed Gharib Bilal, akikagua jengo la ofisi ya CCM ya Tawi la Majenzi iliyopo Kijiji cha Kusale, Wilaya ya Micheweni Mkoa wa Kaskazini Pemba, wakati akiwa katika ziara ya kukagua miradi ya maendeleo mikoa ya Kusini na Kaskazini Pemba leo Mei 17.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohamed Gharib Bilal, akipunga mkono kuwaaga wanafunzi wa Shule ya Msingi Simai iliyopo Kijiji cha Wingwi Mapofu, Wilaya ya Micheweni Mkoa wa Kaskazini Pemba, baada ya kuweka jiwe la msingi katika shule hiyo wakati akiwa katika ziara ya kukagua miradi ya maendeleo kwenye mikoa ya Kusini na Kaskazini Pemba leo Mei 17.
Baadhi ya wanafunzi wa Shule ya Msingi Simai, iliyopo Kijiji cha Wingwi Mapofu, Wilaya ya Micheweni Mkoa wa Kaskazini Pemba, wakiwa katika hafla ya kumpokea Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohamed Gharib Bilal, alipofika shuleni hapo leo Mei 17 kwa ajili ya kuweka jiwe la msingi, wakati akiwa katika ziara ya kukagua miradi ya maendeleo mikoa ya Kusini na Kaskazini pemba.
Baadhi ya wanachama wa CCM na Wananchi wakimsikiliza Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohamed Gharib Bilal, wakati alipokuwa akiwahutubia alipowatembelea akiwa katika ziara ya kukagua miradi ya maendeleo katika mikoa ya Kaskizini na Kusini Pemba, leo. Picha na Muhidin Sufiani wa Ofisi ya Makamu wa Rais

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...