
Hii nayo munatuambiaje ikiwa munasema mstari ulivukwa?

Controversial goals from Frank Lampard and Salomon Kalou, who struck in the last minute, kept alive Chelsea's hopes of catching leaders Manchester United.

Kaka Michuzi naomba tutazame sheria ya Goli halali inakuwaje maana watu wanakuwa na mawazo tofauti kuhusiana na hili goli lililofungwa jana kati ya Chelsea na Spurs wengi wanasema sio goli kwa goli, Ili liwe goli kwa vifungu vyote mpira unatakiwa uwe umevuka ule mstari kwa kiasi gani?
Mdau Pascal



Duuh, Mi sijui Watu wanalalamika nini hili ni goli kabisaaaaaaa, ila ni vigumu kwa refa kuwa na uhakika alifanya good guess work. Sasa malalamizhi sijui yanatoka wapi mi najua kwa vifungu vya FIFA mpira unatakiwa uwe umevuka 3/4 (75%) ya mstari kwani mstari wenyewe ni mnene
ReplyDeleteGoal la Lampard lilikuwa Goal halali maana sheria inasema mpira unapovuka mstari zaidi ya nusu kuelekea upande mwengine basi unahesabika umekwisha vuka, Na tukiangalia kwa makini huo mpira ulivuka mstari zaidi ya nusu, angalia vizuri ktk video replay utaona ukweli upo wapi.
ReplyDeleteUpande wa pili wa shilingi, Goal la solomon kalou halikutakiwa kuingia ktk kitabu cha mwamuzi wa mchezo maana kabla jamaa hajafunga alikuwa yupo ktk offside position hata ukiangalia line inayo chorwa tunaona jamaa line inakuwa imemgusa vizuri tu. Ila goal halali ni lile ambalo refa wa mchezo analikubali, So Chelsea won 2-1 with a controversial goal from Kalou and not Lampard. Bila shaka umepata jibu. Haya turudi mzigoni haya yamekwishapita, Siku njema.
Hili goli ni halali kabisa,mpira umevuka mstari na unaonekana dhahiri,anayesema si goli ni mbishi tu.
ReplyDeleteHilo ni goli halali,kinachotakiwa ni mpira kuvuka mstari haijalishi sentimita ngapi au milimita ngapi.Mpira unaonekana dhahiri kuwa umevuka mstari hapo.
ReplyDeleteThe rule states very clearly that the whole of the ball must cross the whole of the line to be a goal, having said that, for this particular issue it didn't. So neither of the Chelsea goals should have stood, second a yard offside.
ReplyDeleteuhalali wa goli ni kuvuka mstari wote.hizo sheria za kuvuka3/4 umezitowa wapi?
ReplyDeleteVideo replays clearly show the ball didn't cross the line after Gomes spilled Lampard's shot
ReplyDeleteKuna siku ballboy alifunga bao na likakubalika huko Brazil! Hii mipira ni kupoteza wakati tu kwa walala hoi, tafuta shamba ulime!!
ReplyDeleteGOLI ALILOFUNGUA KALOU HALIKUWA OFFSIDE, NI GOLI HALALI KABISA KWANI DROGBA ALIKUWA HATOI PASI ALIKUWA ANATAKA KUFUNGA DIRECT. THAS Y OFFSIDE WAS NOT COUNTED.
ReplyDeleteMiaka ya nyuma walikuwa wanaangalia ni sehemu gani ya mpira imevuka mstali ndipo hapo ilikuwa inatumika HIYO (3/4) lakini pia ilikuwa ngumu kwa refa (waamuzi) kuona na kujaji kuwa sehemu kubwa ya mpira imevuka mstari.
ReplyDeleteYakafanyika mabadiliko ya tafsiri ya sheria hii na sasa goli husemwa kuwa ni halali endapo tu mpira (wote) utavuka mstali wa goli.
Kilichotokea jana ni moja tu yamatukio mengi ambayo yanatokea uwanjani na kufanya mpira wa miguu upoteze ile radha yake. Lakini kingine ni kwamba mwamuzi wa kati (Mariner) asingetoa uamuzi kuwa ni goli kama si msaidizi wake (Cairns) kutokana na influensi ya mashabiki.
Goli la pili, Kalou alikuwa ameotea, lakini ni maamuzi ambayo si rahisi na msaidizi wa refa haikuwa rahisi kuona hili kama ilivyokuwa kwa goli la kusawazisha kama ilivyokuwa kwetu washabiki hadi iliporudiwa ndio tukaona kuwa goli/magoli si sahii.
Kwa miaka ya hivi karibuni chelsea tumekuwa tukiyapata maamuzi kama haya kwenye ligi lakini bado hatujaweza kuyapata kwenye ligi ya mabingwa.
Tusiite mbeleko (yakawa ya Mourinho) ila tuseme ni makosa ya kiufundi yanayoweza kutatuliwa kwa kiufundi(goal line technology).
Lakini hapa nyumbani vipi, mambo haya wanayatatua vipi ambapo hata replays hazipo zinazoweza kuonyesha kuwa goli sahii au sio sahii?
TFF wamefikia wapi na kwenda na wakati kama hata kifaa (digital) cha kubadilishia wachezaji au kuonyesha mda wa nyongeza hawawezi kununua na ubao wa kuonyesha magoli wa maboksi,SMH!!!!!!!!!
sheria namba kumi ya fifa inasema hivi,
ReplyDeleteA goal is scored when the WHOLE of the ball passes over the goal line, between the goalposts and under the crossbar, provided that no infringement of the Laws of the Game has been committed previously by the team scoring the
goal.
hii sheria iko ukurasa wa 30 wa Laws of the game ya fifa, kuna picha zinaonesha kuwa mpira ni lazima uingie wote golini ukiingia robo tatu au nusu sio goal. kwa maelezo zaidi bonyeza hii link
http://www.fifa.com/mm/document/affederation/generic/81/42/36/lawsofthegame_2010_11_e.pdf
Mpira ulikwisha kwisha au tunataka walifute goli?Mbona hamuongelei ya taifa ya vijana ya tz iliyofungwa na Uganda jana?
ReplyDeleteWacha na timu nyingine ifaidike kwa mbeleko safari hii. Timu inayobebwa na mbeleko mara kwa mara huko Uingereza inafahamika, au sio wadau?
ReplyDeletemdau wa 01.05pm umeongea point ila inataka mtu mwenye kuelelewa hayo au unasemajeeee?
ReplyDeleteMBELEKO MAN. U KILA MTU ANAJUA KTK DUNIA HII YA MCHEZO WA MPIRA WA MIGUU
ReplyDeleteKwa sheria za FIFA Goal linakuwa counted pale referee anapopuliza filimbi kuashiria mpira kati. Kama referee atafanya hivyo wakati mpira ukiwa umetoka nje basi atakuwa amehatarisha amani uwanjani na hivyo kufungiwa maisha kuchezesha mpira. Ni ukweli usiopingika kuwa jama referees and his assistantas got it wrong for both goals. Ila tunatakiwa kujua kuwa mpira ni biashara na kwa jana ilikuwa na masilahi zaidi kwa Chelsea kushinda ili kuifanya EPL kuwa more exciting. Tunawasubiri pale OT tarehe 8 labla waja na waamuzi wao wa jana. Ila pale hawatatoka salama kabisa.
ReplyDeleteHuyu refa kibarua chake bado kipo valid !
ReplyDeletemdau
kakola , buly
Refa akishapuliza kipenga katka ni goli hata kama mpira haujavuka,. Mbona Wangereza walipocheza na Ujerumani tena kombe la dunia wakiwa nyuma 2-2 mpira uliopigwa na huyu huyu Lampard, ulivuka mstari na kila mtu aliona ila refa akakataa na halikuwa goli. angalia picha ya pili mpira umevuka na ni goliTsubiri tarehe 8 atakayeshinda bingwa
ReplyDelete