Ankal Issa wa Michuzi,
Kwanza nikuongeze kwa kuturejeshea sie wadau waandamizi hizi mada ambazo kwa kweli ndio chachandu ya blogi yetu ya jamii pendwa ambazo hazipatikani kwingine popote. Hongera sana sana!
Mie bwana ni mwanaume rijali mwenye umri wa miaka 38, sijaoa na wala sifikirii kufanya hivyo karibuni kutokana na sababu ambazo ziko nje ya uwezo wangu. Na nikifikiria mali niliyochuma na kufanikiwa kuilimbikiza kiasi mtaani nionekane fisadi ndio nachanganyikiwa. Mie sio fisadi ila ni kismati tu cha kupata njuruku kwa njia halali, hasa kule Mirerani ambako nna vijishimo vitatu vinavyotema kila kukicha. Ni kweli sijapiga kitabu sana (fom two si haba ati), lakini kila kitu nnacho. Magari ya kifahari, nyumba mbili tatu Arusha na Mwanza na moja namalizia Kinyerezi Dar es salaam.
Pamoja na yote hayo nna hamu ile mbaya kuwa na mtoto. Mtoto wa kiume tena. Tatizo, ambalo kama nilivyosema ziko nje ya uwezo wangu, ni kwamba gobole langu inaonesha halina risasi. Maana kama kuwinda swala na kuwala nimewinda sana na kuwala lakini hata siku moja sijaletewa hata wa kusingiziwa. Nimeenda kufanya vipimo hadi nje ya nchi, na imethibitika kuwa pamoja na kuwa na gobole linalofanya kazi barabara, risasi halipandishi, linatema hewa tu kila ninapokuwa mbugani.....
Yaani Ankal natamani nile sumu nife, kwani mafanikio yote haya nilonayo mtoto sina na kuoa naogoa nisije umbuka. Najua wasukutua midomo humu watanijia juu na kunicharura kwa nini nimeleta humu shida hii. Ukweli ni kwamba baada ya kusoma mada kibao na kuona ushauri lukuki kwa wahusika, nahisi nitaweza kuambulia japo moja ama mawili. Hivyo wadau wenzangu naomba msaada kwenye tuta hili, maana umri ndio huo unaenda....
Naomba email yangu weka kwapani
Sema tu Mdau wa Gobole Butu
PALIPO NA NIA PANA NJIA. UMEDAI UMEPATA MATIBABU NJE YA NCHI NA HUJATIBIKA? INATEGEMEA NCHI GANI. KUNA WATU NAWAFAHAMU KWA SURA NA MAJINA WALIKUWA NA SHIDA KAMA YAKO YA KUTOKUWA NA MBEGU ZA KUTIA MIMBA. AMINI USIAMINI WAMETIBIWA NA SASA HIVI WANA WATOTO SI CHINI YA WATATU KILA MMOJA WAO. DAWA ZILIPOANZA KUFANYA KAZI, WAMEZAA KWA FUJO. KWA HIYO ILI UTIBIWE, INABIDI WEWE NA UNATETARAJIA KUMTIA MIMBA MUMWONE DR. ILI AJUE NANI WA KUPEWA DAWA ZIPI ILI UFANIKIWE HAJA YAKO. USHAURI ZAIDI NINGEKUPA KAMA UNGEKUWA NA EMAIL ADDRESS. DR WA VIZAZI. THX
ReplyDeleteDon't really know how to help, but I must acknowledge your great metaphorical prose. However, I wouldn't agree with your comparison of wooing women to hunting gazelles...lol. It's borderline disrespectful. Either way, all the best man. Low sperm count is a serious issue. But I hear it's possible to freeze sperm, manipulate it somehow, and use artificial fertilization, no?
ReplyDeletePole sana bro! Mimi nakushauri uoe na adapt mtoto hata wa ndugu yako. Mueleze ukweli mpenzi wako na naamini kuna mmoja atakuelewa. Hilo Gobole linarusha risasi, sio kama halirushi risasi. Adapt tu wala sio tatizo kabisa kuadapt mtoto na ukimlea kama umemzaa mwenyewe,wala hautajisikia vibaya kabisa. Usikate tamaa bro, nimapenzi ya Mungu. Ukiadapt, Mungu anaweza kukujalia na kukupatia wa kumzaa mwenyewe. kuna watu walikuwa na hilo tatizo na walivyoadapt haikupita miaka miwili wakapata mtoto, You never know bro!
ReplyDeleteBabu kama kweli hiyo hali imekutokea kikawaida piga goti muombe Mungu atakusaidia ila kama uliweka nadhiri juu ya mali zako muombe Mungu pia atakufungua hicho kifungo na uwe tayari kupoteza ulivyojiwekea nadhiri kwa kutopata mtoto na badala yake upate mafanikio
ReplyDeleteMungu ni Muweza ya yote
Pole na kila la kheri katika mission yako. Ningependa kujua tu, hospitali walikuambia tatizo ni nini? na ni hospitali gani uliyoenda? vipimo gani walifanya/ email kwa mashauriano zaidi:gmariwa@gmail.com
ReplyDeleteSwahiba, nenda vituo vya kulelea watoto yatima kachague wawili mmoja dume na mwingine jike wachukue uwalee inshaalah ALLAH atakujaza imani na watakuwa kama wanao na siku isiyo na jina ALLAH atakuonyesha miujiza kwa kukupatia mke bora ambaye atakuzalia mtoto ambaye atakuwa mtihani kwako kwani anaweza kuwa fisadi wa mali zako.
ReplyDeleteLete subira kwa kumtukuza ALLAH kwa kila jambo, kwani halitokei ila kwa kutaka kwake. +255 71 321 1726
Pole sana kaka, najua ni jinsi gani ujisikiavyo. Acha niende moja kwamoja kwenye mawazo yangu, unajua bro kila kitu hapa duniani ni Mwenyezi Mungu ndo mpangaji, basi kuwa na mafanikio uliyokuwa nayo ni yeye ndo mpangaji, pia na matatiozo uliyo kuwa nayo yeye pia anajua hayo.... Basi ingekuwa vizuri kama ungekaa chini na kumwomba bwana wako kwa dini yoyote uliyo nayo, na pia bro.... najua watu wengi hupenda kuwa na watoto wa damu yao, ila pia kama itashindikana basi kaka waweza kuadapt watoto katika vituo vingi tu vilivyopo vya watoto yatima wasio na wazazi. Ni hayo tu kwa uweze wangu wa mchango juu ya hili swala, and by the way achana na kuwawinda hao swala kwa kufanya majaribio la gobole lako, kwa maana lazima unakuwa hautumii silencer so isije ikakusababisha ukakamatwa(nikimaanisha gonjwa bro). Take care
ReplyDeleteMdau India!
Mdau mbona hii ngoma ni rahisi tu, itabidi uolewe wewe kisha mnafanya adaption ya mtoto wa kiume. Mbona watoto yatima ni wengi tu wameachwa na wazazi wao! huna haja ya kusumbuka kutafuta mke kwani ata-kudissapoint ukwanywa sumu ukafa bure! Ulishawahi kumsikia mwimbaji maarafu wa UK Elton John fuata mfano wake naye alikuwa na matatizo kama yako pamoja na kuwa na pesa lukuki!
ReplyDeleteHaya ndo mawazo yangu natumaini yatakusaidia, inaelekea uliumbwa jinsia ya kiume kwa makosa, jiangalie vizuri huko chini!
Ni mimi mzee wa ushauri.
ankal hakikisha unapost hiyo comment iliyotangulia usiiweke kapuni kwani huyu mdau anatafuta maneno na atayapata na mimi nimekuwa wa kwanza kumpa ushauri sijachafua hali ya hewa hapa. Uniweka kapuni hakiamama tutapigana au nitatoboa matairi yote ya gari lako! ohooooooooo
ReplyDeletemdau gobole butu pole sana
ReplyDeletehata mimi nilikuwa hivyohivyo zamani bt baada ya kupata ushauri mambo yangu safi na sasa nina watoto 2 wa ukweli
dawa ni kwamba chukua pilipili 40 zisage then weka kipande cha barafu, ile barafu ikiyeyuka, koroga ile pilipili na yale maji, i mean inakuwa kama supu then kunywa,hakikisha kikombe kijae
dozi hii ni kutwa mara moja na ni dozi ya siku 5 hivyo unatakiwa uwe na pilipili mia 200
baada ya hapo lenga shabaha,walahi utaniambia
ni mimi mdau gobole butu wa zamani
X GOBOLE BUTU
mdau gobole butu pole sana
ReplyDeletehata mimi nilikuwa hivyohivyo zamani bt baada ya kupata ushauri mambo yangu safi na sasa nina watoto 2 wa ukweli
dawa ni kwamba chukua pilipili 40 zisage then weka kipande cha barafu, ile barafu ikiyeyuka, koroga ile pilipili na yale maji, i mean inakuwa kama supu then kunywa,hakikisha kikombe kijae
dozi hii ni kutwa mara moja na ni dozi ya siku 5 hivyo unatakiwa uwe na pilipili mia 200
baada ya hapo lenga shabaha,walahi utaniambia
ni mimi mdau gobole butu wa zamani
X GOBOLE BUTU
Adoption naona ni jibu. Ila adoption bila mke mie naipinga. Hivyo nakushauri ukumbuke hao "swala" waliopita na chagua mmoja wao uoe. Nzuri sana iwapo ana mtoto mchanga umtunze awe wako. (wangapi wanalea watoto wafikiriao ni wao?) Kama hana mtoto basi mu adopt mtoto mkiwa kama family. Njia nyingine ni kuomba msaada kwa rafiki wa karibu au ndugu. Unapata risasi zao na madaktari wanaziingiza kwa mkeo.
ReplyDeletenakutakia mafanikio
Blackmpingo
Ndugu yangu akili kichwani kwako soma maoni angalia maoni unayopewa yapime ndo uyafanyie kazi na mengine uyaache cha msingi piga goti Muombe Mungu akuponye kama hospitali wameshindwa Mungu hashindwi na chochote brother we mrudie lazima utaona mabadiliko nae atakupa mke wa kufanana nawe na watoto pia.
ReplyDeleteKama uko tayari mimi nina mtoto babake amemtelekeza sababu bado ni mdogo naweza kumpa jina lako akawa wako bila shida, sharti tulee pamoja
ReplyDeleteX-Gobole butu!
ReplyDeleteHiyo dawa yako siiamini!nahisi itakuwa sumu!hebu muhakikishie mshikaji km ni dawa au ni sumu.Maana mshikaji anashida,tena sana,hivyo maelezo yote tunayotoa hapa anayazingatia....ukisema mtu anywe pilipili 40....aisee si kifo unamtakia hicho...moja tu mbide iweje arobaini.
Wee umeathirika kisaikolojia. tafuta usauri wa psychologist maana unaweza kupata mwanamke ambaye ameshazaa tayari ukaishi nae na ku-adopt mtoto hata wa ndugu yako na kumpa hata baadhi ya mali yako. Usijali ilia ondoa mawazo ya kujiua maana mtoto si mwisho wa maisha life has other meaning bro!
ReplyDeleteHaa msikaji kumbe bado hata kuoa hujaoa, oa kwanza ili uwe na mke wako wa moja kwa moja alafu fanyashughuli mtoto wa kiume si kujalibishajalibisha pengine Mungu hakupatii kwa kuwa hunatenda dhambi, tafuta mke wako funga ndoa na kumuomba mwenyezi mungu atakusaidia tu.
ReplyDeleteMichuzi, hivi hawa wanaoandika masihara kwenye jambo zito kama hili ndiyo wanaitwa waosha vinywa?
ReplyDeleteMbona watu tumekuwa wa ajabu hivi, inashangaza sana.
Mdau fanya kila uwezalo muone Prof Malise Kaisi awali alikuwa Muhimbili kisha akafungua Kliniki yake maeneo ya Upanga karibu ja Makao Makuu ya Jeshi- Ngome. Kama si yeye basi atakuwa msaada mkubwa kwako katika hili, sina mawasiliano naye na pia nahisi kama vile alistaafu MNH.
Ila pia usiache kumuomba Mungu wako wakati ukifanya hivyo itapendeza sana iwapo utakuwa na mwenzi wako wakati huo, yupo mtu wa Mungu Tabata Segerea amewaombea wengi na wametoa ushuhuda. Hivyo usikae bure hangaika na Mungu atakupa.
Nachangia
Naomba unione nikusaidie
ReplyDeleteUsiajali kaka, haya ni mambo ya kawaida tu. ila usichoke kutafuta tiba yaani usiache kuwaona madoctor wanahusika na mambo hayo utafanikiwa tu ila pia usisahau mungu kwani yeye ndiye anayeweza hivyo usiache kumuomba. Pia usisononeke wala kusikitika endelea kujihangaikia utafanikiwa tu kaka
ReplyDeleteankali naomba umpe gobole butu email hii nimsaidie niko inda na najua wanakofanya matibabu hayo,kwa hosp. pia kwa dawa za kienyeji ajama09@yahoo.com plz usi view email yangu mpe tuu musika.
ReplyDeletePole sana mpiganaji hayo yote ni maisha ya mwenyezi mungu, Kwakweli najua upo kwenye wakati mgumu sana haswa misongo ambayo inakuzonga kwa sasa. katika kipindi hiki kigumu unatakiwa uwe mvumilivu na uache papara katika maamuzi ambayo unataka kuyachukua. vile vile pale unapopewa ushauri uwe makini sana as matured person nikimaanisha kwamba sikiliza ushauri then uchambue kama unafaa kufuata au la.Sasa mimi ushauri wangu ni kwamba kutembea na kila mwanamke sio solution kwamba ni bahati nasib kwamba unaweza ukampa mmoja wapo uangalie pia na mgonjwa siku hizi sababu unajua unapochomeka machine kwa hali ya kumtafuta mtoto kwa kila msichana inamaana unatembea peku uwe makii na hilo, pili tafuta msichana mueleze yanayokusibu then muonane na daktari na ujaribu kuficha uhalisi wa maisha wako sababu unaweza kupata demu targert yake ikawa mali. tatuta anayekupenda kwa dhati then baada ya hapo muonane na daktari, DK kwake itakua rahisi kuwashauri kwa pamoja badala ya mmoja. ni hayo tu
ReplyDeleteMO
EE BWANA POLE SANA,HAYA TU NI MAJARIBU OMBA MUNGU ATAKUSAIDIA PIA MUONE BABU LOLIONDO HUENDA UKASAIDIWA,USIENDE KWA MASANGOMA USIJE KUPATA WAKINA NSYUKA.
ReplyDeletePole sana kaka,hiyo ni sehemu tu ya maisha,wakati mwingine Mungu anakuwa na majaribu yake,anaweza kukupa watoto akakunyima pesa,au pesa km wewe akakunyima watoto,nakushauri upige goti usemezane na Mungu maana anasema njoo tusemezana na ueleze shida yako upate haki yako,miaka yako bado ni mdogo kiasi cha kukata tamaa,nenda mbele za Mungu uombe mke mwema na mwaminifu atakaye kuelewa,kisha kaa naye kwa kipindi mkimwomba Mungu afungue milango,ikiwa tatizo ni la kudumu basi uadapt mtoto,kumuka mwanamke mwwema na mwaminifu mbele za bwana sio hawa mabinti wa siku hizi walio after money watakuja kukuchafulia vibaya.NITAFUTE
ReplyDeletepole kaka usikate tamaa, angaika utapona nitafute nikusaidie
ReplyDelete0756 - 288088
pole sana kaka nitafute. 0756 288088
ReplyDeleteMkuu hilo tatizo lako linaweza kutatuliwa na ukawa na watoto. Jamaa yangu alikuwa kama wewe akaenda hosipitali Nairobi akasaidiwa na akampa mkewe mimba kwa njia ya Artificial na sasa ana mtoto. Wasiliana na mimi kupitia pwaga@stud.ntnu.no then nita kuunganisha na yeye atakusaidia.
ReplyDeletePole sn ila umeniudhi kusema unataka wakiume kwa kuona km wakike hawezi kurithi?????? acha mambo ya kizamani na nakuapia hata ukijapona ilo tatizo utpata majike matupu. Nimependa ujasiri wako wa kwenda kucheki mana wanaume wengi wengi sana hawaaamini hilo ni kuwakndamiza tu wanawake.
ReplyDeleteKM UNA PESA MPK KWENDA CHECKUP ULAYA BASI HATA TATIZO LAKO LITAKWISHA WATU KM WEWE APO WENGI NA WAMESAIDIWA SO INAWEZEKANA
Pole sana kaka yangu na pia napenda kukushauri kuwa tatizo lako ni dogo sana na linahitaji imani kidogo kama punje ya haradani.Kwanza kabisa napenda kujua je mali zako unazopata hazina maagano? na kama hamna nakuomba umuombe mungu yote yanawezekana kwake aaminiye. Ungekuwa umetoa email address ningeomba nionane na wewe ili nikuelekeze mahali sahihi pa kupata ufumbuzi wa tatizo lako. Kuanzia leo neno kunywa sumu usiliweke kwenye mawazo yako kabisa Mungu bado anakupenda.
ReplyDeleteKila la kheri
Pole sana mdau na baada ya pole kama nionavyo hapa ushauri ni mwingi na kila mmoja kaja na lake.Sasa ushauri wangu mimi ni kuoa kwanza,na umchague mwanamke alie na mapenzi ya ukweli na kukubali hayo matatizo uliyonayo lakini mkapime kwanza maana dunia ya leo hakuna kuaminiana.Na kwakua umejieleza kwamba unajiweza kipesa basi nadhani kutokana na kupanda kwa technologia unayo chance kubwa tu ya kubahatika kupata mtoto kwa njia za kusaidiwa kitaalamu.Inabidi ufanye safari wewe na mke utakayemuoa na labda kuanzia ni India kwanza na kama hamjafanikiwa unaweza kutafuta ktk NET na ukapata na ushauri ndani yake.Ikishindikana basi mnaweza kuadopt mtoto mchanga na kumkuza mtoto maana mtoto ktk nyumba ni barka kubwa na kila siku zinavokwenda mtoto huyo mapenzi yatazidi na hutopenda kumkosa ktk nyumba.
ReplyDeletePole mdau, hilo tatizo watu wengi wanalo isipokuwa wengi wanajificha. Chamzingi kama wadau wengine walivyosema ni kwanza uache tabia za kupiga hapa na pale. Hii ni muhimu sana maana hata hao wenye watoto basi baadhi yao wana tatizo kama lako. Pia kuna watu ambao kiafya hawana tatizo lolote lakini bado nao hawapati watoto. Mwenyenzi Mungu ndio mwenye uamuzi wa nani azae na nani asizae. Isipokuwa kila maradhi yanadawa yake isipokuwa kifo tu. Sasa mdau moja ya kitu kinachosababisha kukosa uzazi kwa mwanaume ni kuwa na mbegu kidogo za uzazi. Lakini ili mimba itunge inahitajiwa mbegu moja tu. Kwasasa funga ndoa na mwanamke mjane mwenye mtoto au watoto. Yeye huyu hatokusumbua kwa sababu tayari anamtoto. Fanya hivi, pendelea kula vyakula vyenye kuingiza manii kwa haraka mwilini kama supu ya kuku, mayai, maziwa, njugu, korosho, matunda na mboga mboga kwa wingi, asali, fanya mazoezi, fanya tendo la ndoa goli moja tu kila wiki mbili. Njia nyengine kama una pesa basi IVF, hii sijui kama Tanzania wanaweza kufanya, lakini India watu wanafanikiwa. Pia usiache kumuomba Mwenyenzi Mungu na achana na wasiwasi maana pia unachangia kukosa uzazi. La mwisho utakuwa hujakosa kitu kama utachukua mtoto wa kimasikini ukamlea. Mtoto wa kulea ni sawa na mwanao na Allah atakuwa pamoja na wewe.
ReplyDeletepole
ReplyDeleteKwanza tafuta umpendae ambae unadhani atafaa kuzaa naye, usirukeruke.
ReplyDeleteNendeni hospitalini. Mbegu zako zitachukuliwa zitapandishwa kwa Mama wakati muafaka.Kama ifanyikavyo kwa mifugo sasa.
Na kwa sababu inaelekea vijisenti unavyo, hii sidhani kama itakuwa shida kwako.
njooo nipo tayari kukuzalia mimi nina mtoto ila babake kamchukua, nateseka natamani sana niwe na mwanaume nimzalie na asininyanyase.
ReplyDeleteMimi nina mbegu na mtoto mmoja lakini pia nimeadapt mtototo mmoja pia, ila ninachokushauri; mtoto wako ni wako, na anakuwa na mapenzi ya dhati kwako, yule wa kuadapt mara nyingi hana mapenzi ya dhati, mfano ukirudi nyumbani yule wa kuadapt anakuja kupokea ulichobeba ila wa kwako nakuja na anataka akushike na kukbusu,(utayaona haya ukishaadapt), alafu pia, watoto wa kuadapt wana tabia fulani ambazo zinaendana na wazazi wake, mda mwingine unaweza kuudhika, mfano haelewi ukimwambia kitu, ana hasira, kiburi, dharau nk. Pia ukiadapt na una mwanamke wa kiswahili mwenye uwezo wa kuzaa, basi atamchukia sana huyo mtoto, hapa kwenye blogu wanasema wana roho nzuri, ila ukishamleta huyo mke akazoea, hamtaweza kukaa salama. Pamoja na hayo nakuhururmia kwa kuwa una pesa na huna hata mchumba, inawezekana hutapata mwanamke anayekupenda kwa dhati na hivyo kukuharibia maisha na kupaisha pesa yako. Bora maisha ya amani yasiyo na mtoto wala mke kuliko maisha ya karaha yenye mtoto na mke. Nina mengi ila kama utapenda nitaweza kukupa experience ya maisha kupitia katerero73@gmail.com
ReplyDeleteinawezekana ni laana za kuua albino mpaka shimo lako linatema ! muombe Mungu msamaha !
ReplyDeleteGobole tupu, oa kwanza na kisha wewe na mkeo mkapate ushauri wa daktari na utapata mtoto. Tatizo unaogopa kuoa kwa vile umeambiwa huwezi kumpa mwanamke mimba. Chagua kwa umakini, mke mwema ambaye atakuvumilia na atakuwa tayari kupitia matibabu kwani mengine (IVF na AI) yataka moyo.
ReplyDeleteMtoto ni zawadi, hata ukikosa usimkufuru Mungu kwani vingapi unavitaka huvipati?
Wapo watu wamekaa miaka 10 kwenye ndoa bila mtoto na baadae wakapata. Usikate tamaa, usibweteke. PENYE NIA PANA NJIA
ninavyokuona mimi una psycological problem unahitaji ushauri kwanza
ReplyDelete1. mbona kuna watoto yatima kibao unaweza oa ukamweleza mwenzi wako tatizo then mkaadopt mtoto
2.hilo tatizo linatibika nina uhakika tatizo lako wewe unataka uwapetu wanawake mimba huko barabarani oa mwanamke then mtatue hilo tatizo kwapamoja mana huwezi kwenda kutibiwa nahuku hata mwanamke huna hilo tatizo lako kutibika inabidi uwe na mke tayari then doctor anaweza kuwasaidia kwapamoja sasa weunataka okota mwanamke barabarani nakumpachika mimba.
3. acha mambo yakizamani eti mtoto wakiume acha kubagua mtoto ni mtoto kwani hizo mali mwanao wakike hawezi rithi idology zakizamani hizo futa
4.Nioe mimi kama upo tayari mimi niko tayari kushirikiana na wewe kutatua tatizo lako na nina uhakika litatatuka shaka ondoa kama upo tayari acha contacts zako hapa nitakutafuta
ungeowa kwanza harafu ukasubili mwenyezi mungu akupe mtoto unataka upate ukiwa unazini?
ReplyDeleteau maombi yako yatasikika vipi??
mimi ningekushauri jambo moja! usijetamani kufa eti sababu huna mtoto au huwezi kuzaa! ni dhambi kuujiua au tu kutamani kufa,kunawengi wanatamani kuishi hata bila gobole kufanya kazi lakini wamekufa! nachokushauri ni kwamba,si watu wote wanazaa! na sikwamba ili kwenda mbingini ticket ni watoto!! wewe oa,acha kuzini ni dhambi na Mungu hapendi, tafuta mke mcha Mungu uoe mpendwa,ufurahie maisha ya ndoa na mpenzi wako mkijua kuwa kupata watoto ni mbaraka toka kwa Mungu.kuna vitamins nyingi sana za kusaidia mbegu kuwa active, hata za GNLD nasikia ni nzuri sana. usiwaze mali zako atakula nani,kwani unamchumia mtu mwingine?? unapowachumia watu ndo wanakuwa wavivu! mimi nina miaka mitatu sina mtot ila tunaishi kwa raha sana na mme wangu.. namfurahia Mungu kunipa mme wangu nayeye ananifurahia sana,watoto tumemwachia Mungu atupe akipenda ila maisha tunayafurahia maana hakunioa niwe kamashine kakufyatua watoto bali alinioa maana ananipenda sana na Mungu aliona yafaa tuishi pamoja kwa amani. hivyo acha mawazo ya kukata tamaa,oa ishi maisha yaliyobaki kwa furaha na mkeo! tafuta dawa ndani ya ndoa na c kuzini na ikiwa ni mapenzi ya Mungu mpate watoto!!
ReplyDeletepiga goti kwa mungu kila kitu kinawezekana
ReplyDeletepole kwa hili tatizo ndugu yangu, mimi nimeona watu waliohangaika ni hili tatizo na kufanikiwa, sasa ushauri wangu humu kuna watu wakweli wa kukusaidia wasiliana nao, kuna wengine wachekeshaji achana nao, mtafute huyo mtaalam wa MNH na huyu jamaa aliyeweka e-mail yake, utafanikiwa
ReplyDeletemwisho tafuta ngoma ndoogo uoe, achana na hao wazamani anza maisha yako upya as a fresh!
mtanzania mwenzio
sikuliza Gobole Butu. inawezakana wewe ni SMG ila hujihui tu. kwa sababu hujaoa. kwa kuwa hadi tumiute mtu kuwa ni infertile, hadi awe amefanya mapenzi yasiyo salama kati ya wapenzi wawili (regular unprotected sex between spouses/partners) kwa muda wa zaidi ya miezi 12. na hiyo regular unprotected sex huwa inatokea ndani ya ndoa, au kwa watu wanaoishi pamoja. sasa kama wewe unaonja huku, kesho kule, kesho kutwa kwingine, hatutaweza kuconfirm kama kweli gobole lako linatoa hewa pekee. pia kuna vipimo mbalimbali vya kupima ubora wa mbegu, vinapatikana hapahapa nchini, hakuna haja ya kwenda nje kwa sasa. sasa amua cha kufanya baada ya maelezo hayo
ReplyDeletesasa samunge kwa babu vipi ? kapate kikombe kaka huwezi jua msaada wako anatibu magonjwa sugu yasiyopona hospitali ilo laweza kua mojawapo kaka kila la kheri
ReplyDeleteaaaaaahh ndugu yangu tatizo lako mbona dogo sana tena kama jogoo linawika vizuri sana huna haja ya kuumiza kichwa kama kwelui una nia ya kuwa na mtoto tafuta kwanza mtu umpendae na umuoe awe mkeo halafu kuna utaalam wa kisasa kama risasi zako hazina nguvu wataalam wanapandikiza risasi zako kupitia kwa mkeo natumai utapata mtoto hata kidini inaruhusiwa kuliko kufikiria swala la kunywa sumu mbona vinawezakana tu mfano mzuri aliufanya michael jackson ila yeye hakufanya kwa mkewe wa halali kwahiyo mbona vitu vinawezaka wala huna haja ya ku adapt mtoto mawazo yatakuwa pale pale tu maana utakuwa bado hujatatua tatizo lako ni hayo tu .
ReplyDelete