Mkurugenzi wa Masoko wa NHC Bw. David Shambwe akielezea mpango kabambe wa maendeleo wa miaka mitano wa NHC ambapo limepania kujenga nyumba 15,000 maeneo mbalimbali nchini nikiwa ni pamoja na Kibla apartments huko Arusha, Mindu apartments jijini Dar es Salaam na Medeli apartments in Dodoma, ambapo asilimia 70 ya nyumba hizo zitauzwa. Katika mada yake Bw. Shambwe aliwataka wawekezaji walio Diaspora kujua kwamba NHC itahitaji wawekezaji, wataalamu, wapangaji na hata wanunuzi wa nyumba hizo ambazo 10,000 zitakuwa za bei ya juu wakati 5000 bei ya chini ambapo wakati wa ujenzi wake zitatoa ajira 300,000

Bw David Shambwe (wa pili shoto) akiwa meza ya watoa mada wakati wa mkutano wa London 3 Diaspora. Toka shoto ni Wakili Walter Chipeta, David Shambwe, Crensencius Magori wa NSSF na Peter Malika wa Nyumba Poa
Afisa Uhusiano wa NHC Bi. Mariam Iddi akiwa katika meza ya shirika lake wakati wa London 3 Diaspora Conference jijini London

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 3 mpaka sasa

  1. AnonymousMay 11, 2011

    Kaka Michuzi tunashukuru kwa habari hizi muhimu za maendeleo ya nchi yetu, napata hofu kidogo ya kuamini huu mpango wa NHC ambao in my opinion is a very ambitious plan or too good to be true. Tangu tuanze kusikia huu mpango hatujawahi kuambiwa kuwa NHC itatoa wapi fedha za kufanikisha hili na gharama za nyumba husika ni kiasi gani maana sasa hivi kuna tetes kuwa hali ya fedha Serikali si nzuri. Natumaini hii si siasa na mambo haya yatatekelezwa.

    Mdau UK.

    ReplyDelete
  2. AnonymousMay 11, 2011

    Michuzi hautoni maoni yetu????

    ReplyDelete
  3. AnonymousMay 12, 2011

    Watu wa NHC mnaotaka kuwajengea nyumba watz jitahidini basi mtengeneze ramani za kisasa ili miji yetu isiachwe nyuma na miji ya wenzetu. Uzuri mmeshatembea majuu mkaona miji ya wenzetu ilivyojengwa. Hatutarajii tena kuona kunaibuka miji uchwara kana kwamba utandawazi haujatuingia. Miji hupendeza kwa kupangiliwa mitaa, kujenga majengo kufuatana na ushauri wa kiutaalamu, huduma zingine kama vile umeme, mifumo ya maji safi na taka, mitaro ya kuakaushia maji yanayotiririka kwenye barabara (Drainage systems) n.k. Na hayo mapaa hatutarajii yawe tena ya mabati yaliyoshika kutu. Inatia aibu unakwenda miji ya wenzetu wakati upo angani unaona inavyopendeza lakini kwetu wakati unashuka dar pale ni mabati yenye kutu unayaona toka juu. Sasa basi washaurini wananchi watumie viezekeo vingine si hiyo mibati inayoshika kutu baada ya mwaka mmoja.

    Na nyi mnaojiita wabeba mabox, jamii inawategemea sana mlete utaalamu mnaoupata huko majuu na si kila siku ninyi ndio wa kwanza kulalama; ooh tz hiki hakuna, ooh tz urasimu, ooh afadhali wakenya. Ni ujinga kama hamtashiriki kuleta mabadiliko katika nchi yenu badala yake mnalalamika.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...