UTEUZI WA KATIBU WA BARAZA LA WAWAKILISHI.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi,Mheshimiwa Dk. Ali Mohammed Shein amemteua Ibrahim Mzee Ibrahim(45) kuwa Katibu wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar.
Taarifa ya Katibu wa Baraza la Mapinduzi na Katibu Mkuu Kiongozi, Dk. Abdulhamid Yahya Mzee imesema uteuzi huo umeanza tangu Mei 4, 2011.
Kabla ya uteuzi huo, Ibrahim Mzee alikuwa Katibu wa Baraza la Wawakilishi ambaye aliteuliwa kwa mara ya kwanza mwaka Januari mwaka 2007 baada ya kustaafu kazi kwa Katibu wa Baraza hilo, Khamis Juma Chande.
Kitaaluma, Katibu Mzee ni mwanasheria mwenye Shahada ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam. Kwa muda mrefu Katibu huyo alikuwa Afisa Mwandamizi katika Ofisi za Baraza la Wawakilishi.
Wakati huo huo, Rais Dk Ali Mohammed Shein, amemteua Abdulwakil Haji Hafidh kuwa Mwenyekiti wa Baraza la Watu wenye Ulemavu Zanzibar. Mwenyekiti huyo pia ni Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Hifhadhi ya Jamii Zanzibar(ZSSF)
Rais amefanya uteuzi huo kwa mujibu wa kifungu Na.9 ya sheria ya mwaka 2006. Uteuzi huo umeanza tangu Aprili 23, 2011.
IMETOLEWA NA:-
IDARA YA HABARI(MAELEZO) ZANZIBAR
MEI 11,2011
ZANZIBAR


Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...