Spika wa Bunge la Muunganoi wa Tanzania Mhe. Anne Makinda akifungua semina ya majadiliano na viongozi wa vyama vya siasa visivyo na wabunge Bungeni kuhusu uanzishwaji wa chombo cha kupokea maoni ya wananchi juu ya uundwaji wa Katiba Mpya ofisini kwake leo 17/05/2011. Huu ni uratibu mpya ambao Ofisi ya Spika imejiwekea kwa lengo la kukutana na kujadiliana na wadau mbalimbali wa kisiasa, Taasisi za dini, sekta binafsi na vyombo vya habari ili kujenga msingi imara wa mjadala mpana wa uundwaji wa Katiba mpya. Leo Spika Makinda amekutana na wadau kutoka vyama vya siasa vilivyosajiliwa vya UMD, AFP,NLD, UPDP, NRA na APPT-Maendeleo. Kushoto kwa Spika ni Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Katiba na Sheria Mhe. Angela Kairuki
Mkurugenzi kutoka AFP Bi Nasra Asenga akitoa maoni.
Mjadala unaendelea.
Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bungeya Hesabu za Fedha za Serikali Mhe. John Momose Cheyo (katikati) akifafanua jambo kwa ujumbe wa Kamati ya Hesabu za Fedha Serikali kutoka kaitika Bunge la Kenya leo.
Wadau wa semina hiyo wakifuatilia ufunguzi kwa makinikwa makini. Katika Semina hiyo Spika amewataka wadau kuweka uzalendo mbele na kuuenzi umoja wa kitaifa.Picha na Prosper Minja-Bunge

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 4 mpaka sasa

  1. AnonymousMay 17, 2011

    kama ni kuuenzi umoja wa kitaifa basi katiba ishughulikie matatizo ya udini yanayotugawa. Iwepo sheria ya kuchunguza na kuadhibu wabaguzi kwa misingi ya dini makazini, sehemu za huduma kama sibitali, sehemu za sheria kama polisi na mahakamani, mashuleni n.k.

    Tusiache dhamana ya kukemea udini iwe mikononi mwa mabosi ambao wanaweza kuwa wadini na wazalendo wa dini zaidi kuliko taifa.

    Dhamana ya kufuta udini iwe mikononi mwa dola kisheria/kikatiba.


    Sidhani kwa hilo kama tutachafua amani bali kuikomaza. Tusipofanya hivyo basi mjuwe tunafuga wadini serikalini na sehemu nyengine za umma.

    ReplyDelete
  2. AnonymousMay 17, 2011

    Watu hawapendi kuzungumzia tatizo la udini nalo linaendelea kumea mizizi na kuleta matunda machungu. Tuung'owe huu mti kisheria. Tukifumba macho, leo ni mimi kesho ni mwanao.

    Kukemea tuu kwa kulaani ubaguzi hakutoshi.

    Nahisi hutajisikia vyema mwanao akimaliza shule akanyimwa ajira kwa misingi ya kidini au kikabila halafu hana namna wala sehemu ya kulalamika kisheria.

    ReplyDelete
  3. AnonymousMay 17, 2011

    Ndiyo nchi hii inafuata utawala wa kisheria, lazima kila tatizo litatuliwe kisheria, hata ubaguzi.

    ReplyDelete
  4. AnonymousMay 17, 2011

    Kama inafikia watu kubadilisha majina ili kuepuka ubaguzi basi serikali imelala saana au ni lengo la baadhi ya wakuu serikalini kwa makusudi kisirisiri.

    Katiba ya sasa inatakiwa kujibu hili ili watu woote wawe huru kukaa na majina yao bila kuadhibiwa kielimu, kijamii, kirafiki, kikazi, kisheria, kihuduma, kibiashara n.k.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...