Nahodha wa Taifa Stars,Shadrack Nsajigwa akipeana mkono na Nahodha Mwenzie wa Timu ya BafanaBafana,Morgan Gould kabla ya kuanza kwa mtanange wao jioni ya leo.
Kiungo wa Taifa Stars,Mohamed Banka akijaribu kumtoka mchezaji wa Bafana Bafana katika mchezo uliochezwa jioni ya leo katika uwanja wa Taifa.Stars imelala kwa bao 1-0.




Hili ni kosa la Maximo. Maximo hafai.
ReplyDeleteKAKA MICHUZI MBONA UWANJA WETU UMEKOSA WATU KABISA? WASHAURI VIONGOZI WETU WATULETEE TIME NZURI ZA ULAYA KAMA MANCHESTER AU BARCELONA NA NYINGINEZO AMBAZO TUMEZOEA KUBISHANA MITAANI. HAWA WAMATUMBI MPIRA HAWAJUI NDIO MAANA TUMEGOMA KWENDA AU KUPOTEZA MSHIKO. NA IKIWEZAKANA PUNGUZENI UKUBWA WA UWANJA ILI WATU WAJAE. UWANJA MKUBWA SANA HUO BONGO...HATUNA MUAMKO NA MICHEZO ZAIDI YA UZUSHI NA UMBEA. KAMA UNAVYOJUA....WABONGO NUKSI TUPU...WE LIKE TO WATCH GAMES ON THE TV AND FOR FREE. HALIPI MTU.
ReplyDeleteKWETU MBAGARA.....MBAGARAAAAAAAAAAAAAAAAAAAA AU MBAGALA
Hii game ilichezwa behind closed door?? or??
ReplyDeleteKiwanja kipo mbali na makaazi ya watu ndio maana hakijai. Ukitoka Mwenge mpaka ufike uwanjani ni masaa zaidi ya sita. Kurudi pia foleni kubwa yanini taabu. Hawa wenzetu wazungu viwanja vipo mtaani kwao. Manchester kiwanja kipo hapo hapo Old Trafford, Manchester.
ReplyDeleteTFF WAKATI UMEFIKA LAZIMA MUBADILIKE JANA NILIKUA UWANJANI NI AIBU KUONA UWANJA HAUNA WATU VIINGILIO NI VIKUBWA KIMA CHA CHINI KIWE 1000 NA NILISHANGAA KUONA TIKETI ZILIZOTUMIKA JANA ZA ZAMANI KATI YA SIMBA VS YANGA NA NYINGINE ZA MAJI MAJI VS AFC INAONEKANA TFF WANA MAJUKUM MENGI ZAIDI YA UWEZO WAO WAMUACHIE MTU MWINGINE UWANJA WA TAIFA KISHA TFF IWE INACHUKUA MAPATO TU NAAMINI CLOUDS FM WANAWEZA KUFANYA KAZI NZURI TFF MTAPATA PESA NA WATANZANIA WENGI WATAPATA FURSA YA KUINGIA UWANJANI.CLOUDS NI MFANO TU KATI YA WENGI WENYE UWEZO MKUBWA
ReplyDeleteNataka kuchafua hisia na hali ya hewa wasiopenda kuona jezi za Taifa Stars zenye kung'ara kama hizi za Bafanabafana! nauliza hivi rangi za bendera yetu ni nyeusi na bluu tu? Wale vipofu wasiotaka kutazama na macho wanayo wanajua wanaziona kuwa timu 3 maarufu rangi zao ni nyekundu na nyeupe wakifuata tukitambua kuwa hizi ni rangi zilizomo katika bendera ya UK lakini tunawashuhudia wakivaa jezi aina zote kulingana na 'mshiko' manjano,nyeusi, kijivu, kijani nyeupe full suti! Jezi za kuvutia Taifa stars ukiwaona ujue wa wanafanyia mazoezi...huyu nani anayekataza timu hii isivae kijani na manjano, manjano na nyeusi, bluu na manjano...! hapa ninachozungumza kuonekana rangi ikiimba katika jezi sio vichorechore tu! Amngalia jwezi za Uganda na Rwanda, siku moja nikaona Taifa stars/Queen ikivaa bluu nyeupe ndio walikuwa wamjitahidi sana..! Aliyepata kuwa kiongozi wa FAT Mwina Kaduguda nilipomuuliza kwa nini hali hiyo ambayo ilianzia kutoka enzi zake alisema jezi ni ghali ...! Mmmmm jezi ghali '..my foot..! si kweli..Nasisitiza Jezi za Taifa ziwe na rangi zenye mpangilio kulingana na umuhimu wa mechi ...mechi tunayotaka kushinda lazima rangi za jezi ziwe zinaimbaa....'singing colours! sio kama za jana za 'msiba'Bafanabafana kijezi walistahili kushinda.!! ...huu Usimba na Yanga wa kijinga tukajizufunze Man U na Arsenal wao ujasiri wa kuvaa jezi za manjano wanaupata wapi ambao sisi hatuna...! tuongoze kitaalam na hasa kisayansi na sio kihisia...!Hii ni changamoto kwa Uongozi wa sasa wa TFF...hata jezi basi ...jezi za misiba wapi na wapi..zitieni nuru jamani..!
ReplyDeletewanaojaza Old trafford wanatoka nchi nzima . Same could be said with Anfield and so on so forth .
ReplyDeleteKama kuna marketing team ya ku manage huu uwanja inafaa ifukuzwe kazi. Kazi imewashinda.
Someone need to do something here . Embarasing, kama wanashindwa kuuza product kama South African national team, with all the tools at disposal .
Or Brazil for that matter.
Sold well, people would have flown from as far apart as Nairobi to watch to watch these games let alone Mwenge
Ndugu zangu mi nataka kulia na vazi la Tanzania. Vipi hawa officials tena wengi wao wamenona, kama vile si wamichezo, kuvaa masuti uwanjani huku kwetu hali ya hewa hii ni lazima? nahisi kama vile wanatoa jasho na harufu ile mbaya, maana viumbe vyote na binaadam pia tunaharufu asilia, sasa basi nawaomba hawa wabunifu wetu waje na vazi la TZ ilituepuke ni hili la wenzetu, wao suti ni vazi la kujikinga hali hewa, ni kustiri mwili, hapa je? Mwl Nyerere alituonesha kwa vitendo vazi murua linaweza kutumika katika mazingira ya kwetu.
ReplyDeleteJamani na nyie wanasiasa ebu onesheni mifano, sio kila mahali suti za magharibi, tumieni pamba za TZ. Tuanze kampeni "buy Tanzania" "au "nunua vitu vya kitanzania" au "Buy Tanzanian products and be proud" pamba yetu safii kabisa.... wakati mwingine utakuta balozi au afisa wa nje ya nchi amevaa kitenge, mwanasiasa au ofisa wa kitanzania kavaa bonge la suti na anatoka jasho hasa katika maadhimisho kadha u kadhaa, aisee tunamtazamo finyu kuhusu raslimali zetu... ebu mnasemaji wavaa masuti.
Kwanini wanaweka mikono kifuani hapo juu? Hii ni wakati wa kuimba wimbo wa Taifa? Jamani si tunatakiwa kusimama kikakamavu na mikono ipo chini?
ReplyDeleteWASAUZI wamebebwa ile mechi ilibidi tushinde tumenyimwa penati 3.goli letu moja limeakataliwa,roho inauma sana mbeleko zilitawala.
ReplyDelete