JESHI la Polisi Tanzania (TPF) leo linazindua Sera ya Ukimwi na Virusi vya Ukimwi katika Maeneo ya Kazi, ambayo italifanya Jeshi hilo kama mfano wa kuigwa miongoni mwa wadau wengine na huduma kwa umma katika kuzuia na kutoa huduma.
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani, Mh. Balozi Khamis Suedi Kagasheki, atazindua rasmi sera hii katika hafla itakayofanyika katika Bwalo la Maofisa wa Jeshi la Polisi (Police Officers’ Mess), Dar es Salaam, ambayo pia itajumuisha hotuba kutoka kwa kwa Mkuu wa Ujumbe wa Ulaya, Mh. Balozi Tim Clarke, Inspekta Jenerali wa Polisi, Said Abdallah Mwema, na Mkurugenzi wa Marie Stopes Tanzania (MST), Dr. Justine Coulson.
Sera hii inatokana na kazi iliyofanyika na Jeshi la Polisi kwa ushirikiano na MST, kwa bajeti ya Euro 750.000 (Shilingi za Kitanzania bilioni 1.6) kama msaada wa kifedha kutoka Jumuiya ya Ulaya. Tangu mwaka 2008, MST imelisaidia Jeshi la Polisi kutekeleza mradi wa kuzuia maambukizi ya HIV na kutoa huduma katika maeneo ya kazi katika wilaya zote za mikoa ya Dar es Salaam, Iringa na Mbeya.
Dhumuni la mradi huu ni kuchangia kupunguza umaskini Tanzania kwa kupunguza maambukizi yaHIV na madhara ya HIV kwenye afya na uzalishaji, hususan miongoni mwa wafanyakazi wa Jeshi la Polisi na familia zao.
Mpaka sasa, mradi huu umewafikia zaidi ya polisi 5000 na wanafamilia wao 28,000 kwa njia ya elimu na taarifa juu ya kuzuia maambukizi ya HIV.
MST imetoa mafunzo kwa waelimisha rika na watoa huduma za kitabibu ndani ya Jeshi la Polisi,iliyopelekea zaidi ya askari 8000 na wanafamilia wao kujitokeza kwa hiari kwa ajili ya ushauri nasaha na kupima afya zao na kujua kama wameambukizwa virusi vya HIV au vinginevyo.
Sera hii katika maeneo ya kazi inaongozwa na kanuni kuu nne; HIV na Ukimwi ni suala linalohusu maeneo ya kazi, haki kazini,usiri, na ustawi wa jumla wa maofisa wa polisi. Inaainisha haki na wajibu wa polisi kwa kuhusiana na HIV na Ukimwi, ikihusishamasuala ya kinga ya maambukizi yanayosambazwa kwa ngono, utoaji huduma na tiba kwa watu wanaoishi na HIV/UKIMWI,Usawa wa Kijinsia, afya na usalama maeneo ya kazi.
Shughuli za mradi zitaendelea kwa mwaka wote wa 2011 kuhakikisha utekelezaji wa sera hii ndani ya Jeshi la Polisi na uelewawa masuala ya HIV/UKIMWI katika maeneo ya kazi miongoni mwa wadau wengine na watoa huduma kwa umma wengine.
Yatajumuisha; kujumuisha sera hii katika mitaala ya mafunzo ya polisi; kukuza uwezo wa polisi kitaifa, kimkoa na kiwilaya;mafunzo ya ‘machampioni’ wa sera ya maeneo ya kazi katika ngazi zote ndani ya Jeshi la Polisi; kuanzishwa kwa mtandao warufaa kwa wafanyakazi wa Jeshi la Polisi na familia zao kuweza kupata huduma za afya zinazohusu HIV; kuandaa nakusambaza vyanzo vya taarifa kwa elimu ya umma na shughuli za vyombo vya habari.
Marie Stopes Tanzania ni mtoa huduma mkubwa kabisa hapa Tanzania za afya za uzazi na uzazi wa mpango na sehemy yamtandao wa ubia wa Marie Stopes International ulimwenguni ambao upo katika nchi zaidi ya 43. Tangu mwaka 1989, MST imekuwa ikitoa huduma mbali mbali za ubora wa hali ya juu, za gharama nafuu na zenye kulenga mahitaji ya wateja ya huduma za afya ya uzazi (SRH) na taarifa kwa wanaume, wanawake na vijana nchi nzima.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...