takribani mwezi na zaidi sasa tangu kibanda hiki kianguke,lakini hadi leo hii hakuna taratibu yeyote iliyochukuliwa na wahusika.sijui mpaka adhulike mtu ndio ijuilikane kwamba kunahitajika marekebisho au ndi mpaka mkuu wa nchi aseme?

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 2 mpaka sasa

  1. AnonymousMay 14, 2011

    mdau ungetueleza ni sehemu gani hapo ili hata wahusika watakapoguswa wachangamkie chapuchapu. picha imekaa kama Moroko hoteli vile. aibu kweli jiji hili. wanakalia kukusanya mapato tu, huduma za jamii hamna. angalia pale Bustani ya Magomeni ilivyochoka, miaka nenda rudi. angalia kituo cha daladala Karume kisivyopendeza, wakati kuna abiria lukuki wanatumia pale, na shughuli nyingi za kiuchumi zinafanyika. nchi hii inatia kinyaa

    ReplyDelete
  2. AnonymousMay 14, 2011

    Tatizo la rais wetu viongozi kama hao wasiowajibika wa nini? fukuza kuna vijana wamesoma sasa hivi na tunauwezo wa kuleta maendeleo sasa hebu angalia hicho kituo hivi kweli huyo muhusika hana aibu au ndiyo wale wasiokuwa na uchungu na uzalendo. Nyie mliopata bahati hiyo kwa mjuano sasa mnajisahau na Rais wetu hataki kujifunza hawa watu ndiyo watakao kuangusha sijui kama anayaona haya, Miji yetu miundo mbinu mibovu, mazingira machafu, hivi kweli hizo Phd. wamezitoa wapi? naomba mnaojadili katiba mpya wakuu wa mikoa waachiwe wananchi wa mikowa yao wachague mkuu wa mkowa wao na siyo Rais tuepukane na hii mikirimba.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...