Hii ni Video fupi ya Ziara iliyofanywa na Tanz UK ikiwakilishwa na mwenyekiti wake Dr John Lusingu alieambatana na Mkurugenzi wa Aset Asha Baraka. Ziara hii iifanyika mwishoni mwa wiki iliyopita kwa dhumuni ya kutembelea kampuni ya Computer 4 Africa chini ya uongozi wa mwenyekiti Aseri Katanga ambayo inajishughulisha na ukusanyaji wa computer zilizotumika kutoka katika mashirika na taasisi mbalimbali hapa UK, kisha kuzisafisha, kuzikarabati na kuziongezea uhai mpya unaonendana sambamba na teknolojia mpya na mwishowe kuzisambaza Africa Nzima. Tanzania ni mojawapo ya nchi za kiafrika ambazo zimenufaika zaidi katika mpango huu kabambe ambapo shule zaidi ya mia zimenufaika kwa kupewa msaada huu.
Huu ni mmoja wa mifano mizuri ya kuigwa kwa watanzania wote hususani waishio ughaibuni/ Diaspora ili kusaidia kuleta maendeleo nchini kwetu na hatimaye barani afrika bila ya kutegemea serikali pekee.
Asanteni
URBAN PULSE CREATIVE
NATEGAMEA WATANZANIA sasa watambue second hand VITU VILIVYOTUMIKA ULAYA VINA SOKO VILEVILE.Nimemsikia ASHA BARAKA na mwenyekiti wa watanzania akizungumza.
ReplyDeleteNina kaka yangu anauza vitu vya mitumba kama TV,FRIJI,PHOTOCOPY lakini anapata taabu sana kuwaelimisha wananchi wanasema haaaaa hivyo ni vitu chakavu bei kubwa sana na hata mtu anauwezo kidogo ukimwambia njoo kwenye duka langu la mitumba anasema hivyo ni vitu chakavu siji kununua na maneno mengi.
Ndugu zangu tuwaelimishe hawa ndugu zetu wajue hata Ulaya kuna vitu vya second hand au mitumba vinauzwa kwa bei tena kubwa