Albino Fulani akijiandaa kutoa msaada kwa wanafunzi wenye ulemavu wa ngozi katika shule ya msingi Buhangija mkoani Shinyanga
Albino Fulani akizungumza na mwanafunzi Kabula Nkalango aliyenusurika kuuwawa kwa kukatwa mkono wake wa kulia katika mauaji ya walemavu wa ngozi
Msanii wa Muziki wa Kizazi Kipya Babu Sikare maarufu kwa jina la Albino Fulani ambae pia ni CEO wa Afrobino akiwa katika kituo cha Malezi ya watu wenye Ulemavu wa ngozi cha Shule ya Msingi Buhangija mkoani Shinyanga ambako alitembelea na kutoa misaada ya mafuta maalum kwa watu wenye ulemavu wa ngozi (Sunscreen), Kofia na Mianvuli.
Bwana Sikare alisema kuwa maalbino wasiojiweza wanaweza kuishi miaka mingi wakiwezeshwa kwakupewa misaada ya kuzuia cancer ya ngozi. Aliwashukuru watu wote walio unga mkono "Save Albino Concert" iliyofanyika hivi karibuni huko Houston, TX. Pia aliwashukuru wadhamini wao ESM Travel ya Chicago Usa, Boombastic Sound ya Houston TX, Studio Elements ya Houston TX na Pillarsis ya Tannzania.
nikiona vitu kama Kabula alivyofanyiwa kukatwa mkono, inanipa uchungu sana, Mungu ibariki Tanzania, tusamehe Taifa lako, kwanini kweli tufikie kutafuta hela kwa njia hii?
ReplyDeleteWATU WAMEKUWA WANYAMA NA KUWA NA IMANI ZA KISHIRIKINA KUWAUA ALBINO VIUMBE WASIO NA MAKOSA ILI KUTAFUTA UTAJIRI,NI HABARI ZINAZOTIA HURUMA SANA,NA HII YOTE NI BAADHI YA WATU TANZANIA KUTAKA UTAJIRI WA HARAKA BILA KUTOA JASHO,UNAPOFANYA MAOVU YA NAMNA HII MUNGU NAE ANAKUONA NA MWISHO WAKO NA UTAJIRI UTAKAOPATA UTAKUWA MBAYA TU.
ReplyDeleteMUNGU IBARIKI TANZANIA.
Inawezekana kuwa wanaowakata viungo ni hawa hawa viongozi wetu wanasiasa,wanaamini kwamba akifanya uchwawi kwa mganga ndio atafanikiwa kisiasa,iwe bmbunge waziri diwani,hawa ndio kutoa order ya kiongongu na wananchi kuvamiwa.
ReplyDeleteWafanya biashara pia nao wanaoamini mambo ya uchawi,hali inasikitisha sana,na tatizo kubwa ni kwamba nchi yetu hakuna elimu ya kutosha haya ya ubinadamu,imani hakuna kabisa,iwe muslam au christian,upendo haupo kabisa.
Serikali ina majukumu makubwa kuwalinda hawa walemavu wa ngozi kama albino,ikiwezekana serikali uchukue nafasi kuwachukua na kuwalea wao na kuwapa elimu,afya,makazi bora na ya usalama,na support nyengine