Ankal Michuzi,
Nami nipe nafasi nichangie huu mjadala ambao umewashwa moto na ndugu yetu Madaraka Nyerere ambaye ni wakili wa kutetea ujenzi wa barabara hii katika mbuga ya wanyama ya Serengeti huko mkoani Mara. Naomba uweke ramani iliyotolewa na wanaopinga barabara hiyo kiasi hata wamefungua mtandao wa propaganda kujaribu kushawishi watu kwamba mpango huo ni bomu.
Kwanza nianze kwa kumpongeza Jakaya Kikwete, Rais wetu mpendwa ambaye tutamkumbuka kwa mengi baada ya muda wake kumalizika, kama ilivyokuwa kwa Baba wa Taifa Mwalimu Nyerere ambaye leo anaonekana lulu wakati ambapo katika uhai wake alionekana mbaya kwa karibu kila jambo. Yaani binadamu ni wanafiki... We acha tu!
Anyway, tukirudi katika hoja yangu, naomba uangalie kwa makini ramani hiyo na michoro ya barabara (kijani na nyekundu) kabla ya kuanza kuosha kinywa na kunishambulia (kama wewe ni Mtanzania Mzalendo), kwani haina kificho kwamba wanaoendesha kampeni hiyo dhidi ya barabara hiyo ni akina nani na kwa nini.
Nasema hivyo kwa sababu katika ramani inaonesha dhahiri kwamba wanaopinga ni wale wanaohofia kwamba wanyama hawatokwenda Masai Mara wakati wa 'annual animal migration', na kupeleka biashara ya utalii kwa watani wa jadi. Sababu ya hofu hiyo ni dhahiri, ukizingatia kwamba pamoja na kuwa mbuga ya Masai Mara ni kakipande kaduchu tu ka Serengeti (japo wenyewe wanakatangaza duniani kuwa ndio baaab kubwa kuliko Serengeti yetu), si kweli wanyama katika kwamba Serengeti yetu wataathirika kwa ujenzi huo. Hii ni propaganda za kitoto kama anavyoweka sawa kaka Madaraka Nyerere! Mbona mbuga ya Mikumi kuna barabara ya lami na wanyama wanaongezeka badala ya kupungua. Kama ni kugongwa na magari, ambako ni kwa nadra sana, mbona hata binadamu wanagongwa? Na nani anayeweza kutoa ushuhuda wa kisayansi kwamba lami inaathiri wanyama?
Hoja yangu ni kwamba naunga mkono ujenzi huo pamoja na msimamo wa JK kwenye hili kwani Mkwere wetu kaona mbali, na ukichanganya na nia hyake ya kusaidia maendeleo katika mkoa huo wa Kaskazini, hapo piga ua barabara hii ni muhimu kwa mstakabari wa maendeleo ya wananchi wa huko na nchi yetu kwa ujumla. Hao wanaoogopa ni shauri yao kwani hayatuhusu. Waosha vinywa sukutueni mtakavyo lakini ukweli ndio huo. Kwamba barabara hiyo inatishia uhai wa Masai Mara na si vinginevyo kama wanavyojitahidi ionekane.
Na wewe Mtanazania yeyote yule unayetaka sifa za kitoto kwa kuunga mkono wanaopinga angalia hiyo ramani kwa macho yasiyo na mawani ya jua na utajua nini nasema hapa. Wenye kuchukia hili na wanywe sumu wafe kivyao.
Mdau Zebedayo Mugamu
Mkoani Mara

Yaani wewe mugamu sijui nani whatever ur name is, inaonesha ni kwa jinsi gani ubongo wako umeganda kwa hoja za kitoto unazotoa, hao kenya unawasema wewe hata kama sisi tutajenga hiyo barabara still wataendelea kua juu katika sekta ya utalii kwasababu kwanza wenzetu wana vision ya mbali sana kuhusu utalii na pia wana strategies za kueleweka, na hawategemei masi mara tu kama unavyodai, ukuaji wa kenya katika utalii unatokana , na kua wao walianza hizi shughuli za utalii back in 60s, wakati sisi tumeanza kuuchukulia utalii serious miaka 6 au 7 iliopita, na pia hawa jamaa wana ndege zao zinazo zinawafata watalii toka makwao hadi kenya kwa bei poa, so hatuezi kuwafikia hata tuloge vipi kwa uongozi kama huu usio na vision ya miaka 100 mbele. viongozi wetu wanatekeleza majukumu yao kisiasa zaidi kuliko uhalisia wa mambo kwanini hatudhamini viumbe ambao wameifanya nchi hii kua na sifa duniani, na kuiingizia taifa taifa pato kubwa, utalii ni sekta ya pili baada ya kiliomo kwa kuliingizia taifa pato. tunachojaridili hapa ni kua ujengwaji wa barabara utaharibu the natural phenomena (the great serengeti migration) ambayo ilikuepo a millions years ago na ni moja kati ya natural wonder of the world na inatambuliwa na UNESCO. Moja ya madhara ya yatakayotokea iwapo barabara itajengwa ni kuwa wanyama (wildebeest na zebra)watashindwa kuendelea na hilo tendo asilia, na hivyo kusababisha over grazing katika hifadhi ya serengeti, na pia kusababisha uharibifu wa mazingira
ReplyDelete(kivipi umiza kichwa ili ujue).kumbuka kila kitu hapa duniani lazima kibalance ili mfumo wa maisha uendelee(kama ilivyo kwa wanyama jamii ya paka(carnivores) kula wanyama wenzao na still hao wanyama(herbivores) hawapungui, hujajiuliza pamoja na mmomonyoko wa mazingira miaka na miaka, lakini milima imeendelea kumaintain urefu wake ule ule angaalia kitu kinaitwa isostacy? kwa taarifa yako shughuli za kibinaadam ndiyo zinazongooza kwa uharibifu wa mazingira ,refer the ozone layer destruction, global warming n.k. Lengo la kutoa maelezo hayo yote ni kwamba endapo itajengwa barabara serengeti, siyo tu itahatarisha usalama wa wanyama pori na uharibifu wa mazingira utakaofanywa na wasafiri, bali utaharibu mfumo mzima wa ecosystem, kuvutia watu kuweka makazi kandokando ya barabara na kusababisha mgogoro wa ardhi kati ya wanyama na binaadamu, siyo soon baada ya kujengwa bali hata miaka 50-100 ijayo.na pia kupoteza uhalisia na heshima ya hifadhi ambayo kujulikana kwakwe kumetokana sana na migration ya hao wanyama na ecosystem yao. na pia itapunguza idadi ya watalii kuja nchini.nimesikia kua hii barabara ni moja ya ahadi ambazo Kikwete alihaidi kuitekeleza katika uongozi wake.
Angalizo:SIASA IPO NA ITAENDELEA KUWEPO, ILA ASILI KWA MAANA YA NATURE, NI NGUMU KUIREJESHA MARA ITAKAPO HALIBIWA
nawasilisha mdau Moscow
Mdau Zebedayo, fahamu kwamba wanyama hawana mipaka. Hawajui Serengeti ni ya nani na Masai Mara ni ya nani. Uhamisho wanaoufanya kila mwaka sio kwa kupenda au kujiburusisha. Ni uhamisho kwa kufuata chakula na maji. Wao kwa ufahamu wao wanajua wapi kuna chakula na maji lini. Ndio maana huwa wanahama hama namna hiyo. Hivyo kuzuia uhamisho wao kwa kujenga barabara ni kutowatendea haki wanyama na kuhatarisha uhai wao kuendelea kuwepo kwao in the long run na matokeo ni kuikosesha nchi mapato makubwa ya utalii. Serengeti ni ya faida sana kwa watanzania.Pamoja na kwamba Masai Mara ni ndogo na in fact inafaidishwa na kuwapo kwa Serengeti, bado ni maamuzi ya wanyama kwamba msimu huu wanakuwa Serengeti na msimu huu wanakuwa upande wa Masai Mara na hiyo pamoja na wingi wao, ndio inayoifanya Serengeti na Masai Mara viwe vivutio vikubwa. Existence yao na infact, hiyo migration ndio inayowezesha nchi hizi mbili zifaidike sana na mapato ya utalii. Unajua ni watalii wangapi huwa wanakuja kushuhudia migration? Nazungumza kiuchumi zaidi na ki-ikologia pia. Tuangalie maendeleo ya nchi kwa ujumla, sio mkoa mmoja au miwili tu.
ReplyDeleteAnony wa kwanza, napenda ufahamu kwamba wakenya walioanza utalii miaka ya 60s ni wakenya wazungu ambao kwa wakati huo walikuwa wakiendeleza utalii hadi tanzania lakini kwa faida yao.
ReplyDeletendi haohao hata leo hii wanaohofia kupoteza biashara pale Masai mara. Kwanza unasema kenya haitegemei Masai mara sio kweli. Wanaitegemea sana ndio maana wanataka kujenga airport pale masai mara ili watalii waende moja kwa moja pale.
Kasome vizuri makala zimeandikwa na wazungu wenyewe hao hao kunonesha ni jinsi gani wazungu wenzao waliokuwa kenya walivyonyonya Tanzania. Sasa hivi tunasema basi. Hatukubali tena kunyonywa.
Wadau wameshatoa majibu kuwa ili kuleta win-win situation basi hao wanaoguswa na wanyama zaidi kuliko binadamu watoe pesa ijengwe barabara ya chini kwa chini. Ubishi utakuwa umeisha mpaka hapo.
Mimi napinga hoja ya kujenga road hiyo kwa sababu tu ya uzembe wa watanzania ktk kusimamia na kutekeleza sheria. Mngebadilika mkawa wastaarabu mnaofuata sheria na taratibu zinapowekwa, barabara hiyo ingejengwa katikati ya mbuga bila kuathiri wanyama.
JK toa msimamo wako achana na siasa za maji taka.
wewe una ufinyu wa mawazo. wanyama wataathirika kwa kuharibu natural migration yao na ecological balance. wewe ulitaka wanyama wa kenya wakae kenya na watanzania wakae tanzania? unataka kutengeneza ZOO? labda ungetumia hoja nyingine si hiyo
ReplyDeleteMkuu Zebedayo,
ReplyDeleteKupishana kwa hoja haimaanishi sio uzalendo...tunaipenda Tanzania kupitiliza...tutake radhi wana blog ya jamii.
Naunga mkono hoja ya ujenzi wa barabara uendelee.Maendeleo duniani yanaletwa na watu na sio wanyama. Binaadamu kwanza wanyama baadae.
ReplyDeletesisi wasukuma siku hizi tunaoa wake wa kichaga sasa kwenda ukweni mpaka tuzungukie kenya au singida inakuwa safari ndefu sana, kanda ya ziwa na kanda ya kaskazini imekuwa kama ni sehemu zilizo mbali wakati zinapakana, so long as mikumi kuna lami na wanyama wanaendelea kuishi poa na sisi tunahitaji barabara ya lami na hicho kipande anachosema kikwete kwamba kitakuwa cha changarawe mi naona atoe tu kupigwe lami pote, hakuna madhara tuna experience ya mikumi.
ReplyDeleteWewe ndiye mwenye ufinyu wa mawazo. Kwani wanyama hawako adaptive kulingana na new situation. Kama ni mwanafunzi basi umezoea kukariri bila kusugua kichwa. Hata hawa ngombe, mbuzi na kondoo tunaofuga walikuwa ni wanyama wa porini lakini walijiadapt kutokana na mazingira. Barabara itakapojengwa wataadapt tu. Tatizo litakuwa kwenye kuwagonga tu kwa sababu ya uzembe wa madereva lakini si vinginevyo.
ReplyDeleteHakuna kisichowezekana chini ya jua lazima uelewe hivyo!! Barabara yaweza jengwa na wanyama wakaendelea kuishi kama kawaida. Kwani hayo magari ya watalii yanayoingia huko hamyaoni? Si mngeyazuia basi ili tujue kweli mna uchungu na hao wanyama
swali kwa michuzi.
ReplyDeleteNaona una ubaguzi mkubwa sana, post gani hiyo umeweka hata haina point nilikutumia post kuhusu soda ash in lake natron ukaitia kapuni. Na hakuna sababu nyingine ya kujenga barabara upande ule wa kaskazini badala ya upande wa kusini, zaidi ya hiyo sababu ya hicho kiwanda. Unatuwekea hoja ambazo hazina mpango.
Nikirudi kwenye post hiyo, we jamaa umechemsha na hujui unachoongea. Kwa taarifa yenu fupi wakenya wanataka sana si tujenge hiyo barabara ili tuharibu sifa ya serengeti na wao waendelee kuwa juu.
Kwani hiyo barabara ikijengwa kutakuwa na ukuta wa kuzuia hao wanyama wasivunge au vipi, mbona mmeniweka kwenye mataa?
ReplyDeleteBiashara ya utalii ni ngumu kwa mmatumbi kuiendesha. Maana hata huku kwao watalii wanachagua makampuni ya uhakika kununua holiday zao. Kosa ndogo tu wakiliona wanaishitaki kampuni waliyowauzia holiday. Dereva kama hatabasamu tu kwao kosa. Hawa wazungu wa kenya wameiweza hii biashara kwani wanatekelezea hawa watalii wao kila wakipendacho, ndio maana unakuta hata mtoto wa mfalme anafika kwenye hizo sehemu na kukaa wiki mbili. Magari ya kubebea watalii hayana viwango, mtalii akirudi kwao mgonjwa, mfano yule mke wa Cole, alikuja TZ kupanda mlima, aliporudi kachukua malaria. Mambo kama haya yanaifanya TZ isipate watalii wa package ambao ndio wenye pesa za uhakika. Lazima miundombinu iimarishwe ili kurahisisha huduma za watalii. Usalama wa watalii ni muhimu, sasa serengeti hakupitiki wakati wa mvua, unategemea mtalii ameshalipa pesa zake nyingi akwame matopeni kweli?
ReplyDeleteIts crazy that you guys are actually discussing this matter rather than being utterly disturbed. Are economic reasons enough to build a road through the most beutiful and well preserved areas in the world? Are we soo much blind to the fact that animals in the wild need to have their freedom and wild natural habits to fully sustain their lives, grow and multiply. Can we actually take the risk in disturbing the Serengeti National Park just because we are poor. Being poor doesnt mean we are stupid, and for the guys who are for the motion of building the road for economic reasons why dont we just kill all the animals and sell their skins and other artifacts, build another city in Tanzania and we can name it Serengeti in remembrence and move on with alot of money. My point is never mix conservation with economic interest, it never works, building a road over or underground is all disturbance to an ecosystem that is well balanced for thousand of years. Let the national park be pure and untamed, the president focus on other means to eradicate poverty in the country.
ReplyDeleteMie nadhani kabla ya kuchangia lazima tujiulize KWANINI WANYAMA WANA MIGRATE KUTOKA MASAI MARA KWENDA SERENGETI? akitokea mtaalamu wa hili kwa ufafanuzi nadhani atatupa mwangaza wa nini kifanyike japokuwa sioni shida kama barabara ikijengwa kwani wachingiaji wengi nilivyoona ni wanazungumza kinadharia zaidi ikiwa na maana kwamba wengi wao hata mbuga moja hawajawahi kutembelea, nasema hivyo kwa kuwa humo mbugani kwenyewe kuna njia kibao za changarawe ambazo magari yanapita mfano mzuri ni kutoka Fort Ikoma kukatiza Serengeti mpaka geti la Naabi mpaka Ngorongoro na magari kibao yamepita, mie nadhani kwa kuwa barabara ni changarawe sidhani kama kuna ubaya hasa ukizingatia Serengeti kuna barabara nyingi ambazo kwa siku magari yanayopita ni mengi zaidi. Kikubwa ni utekelezaji wa sheria pia waendelee na utaratibu ule ule wa magari kuwepo mbugani iwe saa 12 jioni na isiwe kama mikumi ilivyo ambapo magari usiku na mchana yanapita
ReplyDeleteKAMA KWELI HAO WAZUNGU NDO KIPINGAMIZI CHA BARABARA,BASI WATOE FUNGU LA FWEZA IJENGWE RELI ZILETWE TRENI ZA KWENDA FASTA ILI HAWA WASUKUMA NA WAJITA WAWAWAHI WAKE ZAO HUKO MOSHI.MAANA NAONA WATU WANABISHANA TU BILA KUWA NA PLAN B.KINACHOTAFUTWA HAPO NI KURAHISISHA USAFIRI KATIKA MAENEO HAYO.BASI TREN IWE NDO UFUMBUZI WA TATIZO HILO KWANI MIZIGO ITABEBWA,ABIRIA WATABEBWA MAMBO YATAKUWA MZUKA KABISA.AU MNASEMAJE WASHKAJI NA PLAN B YANGU?
ReplyDeleteHakuna cha Ecosystem wala nini....mambo yatajibalance tu yenyewe..wanaoleta point ya ecosystem wanataka kuonyesha tu ujuaji wao katika suala la ecosystem...Kikwete endelea na mipango ya Ujenzi wa barabara watali watakuja na watashangaa maajabu ya Serengeti kama kawa....Hao wakenya kivyao na sisi kivyetu mambo ngwana kabisa, ...nyambafu!!
ReplyDelete