NI KITABU CHA KISWAHILI NA KINACHO ZUNGUMZIA MAISHA YA KOCHA HUYO TOKEA KUZALIWA, KUCHEZA SOKA, KOCHA KINDA HADI MAARUFU. NINAAMINI WAPENDA MICHEZO WENGI BILA YA KUJALI NI MAN U AU TIMU NYINGINE WANGEPENDA KUJUA KUHUSIANA NA KOCHA HUYO. TAYARI KIPO MITAANI NA KWA WAUZAJI WA REJA REJA NA JUMLA WANAWEZA KUMPIGIA MKUU WA USAMBAZAJI, GLOBAL PUBLISHERS..kounja kwa namba 0655 310 160.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 7 mpaka sasa

  1. AnonymousJune 08, 2011

    Je mwenyewe anajua kuwa kuna kitabu chake kwa kiswahili?

    ReplyDelete
  2. AnonymousJune 08, 2011

    mtakuja fungwa kwa kutumia habari za watu bila ruhusa kujipatia fedha..

    ReplyDelete
  3. AnonymousJune 08, 2011

    je yeye mwenyewe anafaham kama mmeandika bibliography yake na mnauza??? mana kisheria ni kosa la jinai. mana juzi juzi tu Julian Asanji wa wikileaks kuna kampuni imeingia mkataba nae wa kuandika bibliography yake na wamemlipa millions of dollars. mtazamo wangu tu, au Bongo Tambarare hakuna shida

    ReplyDelete
  4. AnonymousJune 08, 2011

    Je maisha ya Ferguson yatamsaidia nini kijana wa Manzese? Si bora ungeandika maisha ya Charles Boniface Mkwasa?

    ReplyDelete
  5. AnonymousJune 08, 2011

    Mkwasa! wewe anon wa 02:41:00 una matatizo;hiyo ni biashara. Uandike kitabu cha Mkwasa gharama za kuchapisha nk itakula kwao. Ujanja kuwahi. Niche market. Wapo watakaokitoa kifaransa; kiganda nk; lengo?? Njurugu. Big up Global Publishers.

    ReplyDelete
  6. Common mwananchiJune 08, 2011

    Issue kubwa hapa sio Mkwasa, Furguson au hata angetajwa Bi Kidude, maana hii ni biashara na manazi (washabiki hasa wa Manchester United) waliopo hapa ni market segment nzuri tu, ila tatizo langu je haki miliki zimefuatwa au ni mambo ya kibongo bongo? Ikumbukwe, ni kosa katika uandishi wa kitaaluma kuchukua kazi ya mtu na kuifanya yako bila idhini ya muhusika, tunaita plagiarism.

    Lakini hata sheria za haki miliki zinakataza hilo na ndio maana unakuta vitabu vingi vimeandikwa ni marufuku kunakili, kurudufu au kutafasiri kitabu hiki kwa lugha yeyote bila idhini ya mwandishi au mchapishaji. Kama waliokitafasiri wanamezingatia haya basi, hakuna shida ila kama hawakuzingatia wajue wamefanya kosa,na wasijifiche kwenye kichaka cha ujasiriamali Dunia siku hizi ni kijiji, mwandishi, mchapishaji au babu Fergie mwenyewe anaweza kukipata na kama wakiamua kuacha ubongo bongo wanaweza kudai chao kisheria. Mpo tayari? Dadisi

    ReplyDelete
  7. AnonymousJune 09, 2011

    Mbona mnapiga kelele bila sababu. Global Publishers wao wamewambia kuwa kitabu kinapatikana kwa kiswahili. Kinachotakiwa kwetu kwa wanaokihitaji ni kwenda kukinunua. Suala la haki miliki waachie wao Global Publishers. Maana publisher yeyote anaelewa SHERIA YA HAKI MILIKO. Kama wamefuata au hawajafuata ni juu yao

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...