Kampuni ya Simu ya Airtel na Amis kwa pamoja wakizundua huduma ya mtandao kwa wakulima wa Tumbako mjini Morogoro,watatu kutoka kushoto ni Naibu katibu mkuu wa wizara ya kilimo,chakula na ushirika Engineer Mfutakamba pamoja na wadau wa tumbaku,airtel na Amis connect wakifurahia uzinduzi rasmi wa huduma hiyo, ambapo ukitaka kupata taarifa ya tumbaku kwa kutumia mtandao wa Airtel pekee unapiga *154*45-alama ya reli.
Mkurugenzi mkuu wa Bodi ya tumbaku bwana Frank Urio akiongea jambo na mgeni rasmi naibu katibu mkuu wa wizara ya kilimo,chakula na ushirika Engineer Mfutakamba wakati wa uzinduzi rasmi wa huduma ya kupata taarifa kwa wakulima mjini Morogoro iliyoanzishwa na kampuni ya simu ya Airtel na Amis Connect mjini morogoro jana.


We should not be promoting tobacco at all.
ReplyDelete