BASI LA ABOOD LIFANYALO SAFARI ZAKE KATI YA DAR NA MBEYA LIKIWA LIMEPINDUKA MARA BAADA YA KUMSHINDA DEREVA WA GARI HILO MPAKA KUPELEKEA HAPO LILIPOFIKIA.ABIRIA ZAIDI YA 31 WAMEJERUHIWA KATIKA AJALI HIYO NA KUFANIKIWA KUKIMBIZWA HOSPITALI YA RUFAA MBEYA KWA MATIBABU.AJALI HII IMETOKEA JANA JIONI MLIMA IMEZU MAENEO YA INYALA NJE KIDOGO YA MJI WA MBEYA.
MOJA YA WATOTO WALIONUSURIKA KATIKA AJALI HIYO JANA MAJIRA YA SAA 1.30 USIKU BAADA YA BASI LA ABOOD LILILOKUWA LIKITOKA DAR KWENDA MBEYA KUPINDUKA.
BAADHI YA ABIRIA WAKIWA KATIKA HOSPITALI YA RUFAA YA MBEYA MARA BAADA YA KUPATA MATIBABU.
MUONEKANO WA BASI LA ABOOD BAADA YA AJALI HIYO.

PICHA NA MBEYA YETU.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 11 mpaka sasa

  1. AnonymousJune 02, 2011

    Bad news. Kila siku tunahesabu ajali. Hivi mwarobaini wa ajli nini?????????? Wadau naomba tusaidiane juu ya hili. Mimi nadhani labda serikali ya CHADEMA 2015 inaweza kupunguza kama sio kuondoa ajali kabisa Tanzania.

    ReplyDelete
  2. AnonymousJune 02, 2011

    Mauaji ya ajali tanzania ni kama vita. wengi wamekufa na wengi wamebaki vilema. kama vita tu! je, serikali inachukua hatua gani madhubuti?

    ReplyDelete
  3. AnonymousJune 02, 2011

    Duh hiyo picha ya mwanzo inanipa kiwewe, hiyo kutu ilozunguka kioo kizima ni ishara ya kuwa gari ni kongwe mno na halijafanyiwa matengenezo kwa miaka mingi. Jamani tanzania tunachezea maisha yetu kwenye ncha za vidole jamani!!!

    ReplyDelete
  4. AnonymousJune 02, 2011

    SAFU YOTE YA WIZARA HUSIKA IJIUZURU KWANI HIZO AJALI ZINAWEZA KUPUNGUZWA AHHHHHHHH TUMECHOKA.

    ReplyDelete
  5. AnonymousJune 02, 2011

    Michuzi,pole kwa majeruhi.Juzi hapa wakati wa ajali ya Sumry mimi pamoja na wadau wengine tulisema kuna tatizo katika system nzima ya usafirishaji wa abiria Tanzania kuanzia kwenye sheria za barabarani,barabara zetu ,wamiliki,madereva wenyewe(pamoja na abiria?)na mabasi yenyewe kwa maana ya usalama wake.Mimi narudia tena kuna tatizo hapa..hata kama serikali itaweka gundi kwenye masikio lakini "habari ndiyo hiyo".

    David V

    ReplyDelete
  6. Ugua pole majeruhi. Michuzi kwenye hiyo picha ya kwanza mbona basi linaonekana kama lina kutu vile?

    ReplyDelete
  7. AnonymousJune 02, 2011

    hii nchisasa tumeichoka kila siku ni ajali tu halafu hakuna mikakati yeyote ya kupunguza hizo ajali zaidi ya rushwa tu, mara wauze stika za fire extuinguisher,mara sijui nini yani ni ujinga ujinga tu>viongozi wa tanzania hakuna aliyekuwa serious hata mmoja,haiwezekana nchi iwe kama ipo likzo watu wanakufa kwa ajali kila inapoitwa leo.barabara zote za dar mashimo yani shida sana.

    ReplyDelete
  8. AnonymousJune 02, 2011

    Kila mtu ni wa kulaumu hapa, nami nawalaumu abiria wengi Tanzania. Wanapenda kufika mapema sana waendapo!!! Siku moja nilikuwa nimepanda basi , abiria walikasirika sana na kuanza kumrushia vijembe dereva.
    " Hivi wewe dereva unafikiri sisi tuko msibani???" wengine walisema " halo hivi wewe ni utingo au unajifunza kuendesha???" ebu nenda kajifunze chuoni kwanza ndio uje uendesha." Kwa kweli inasikitisha kuwa na abiria wengi wasioelewa chochote kuhusu usalama wao, bora wafike. Wengine walianza kusimuliana kwamba. " Aise nilipanda basi moja kutokea dar kwenda dodoma, yule bwana mdogo alikuwa anaikanyaga hasa yani mpaka unasikia laha!! hadi nguzo za tanesco huwezi kusihesabu.

    Kwa hiyo abiria nao wana mchango katika ajari kwa kuwa wengi ni wapenzi wa mwendo kasi.

    Mdau Hoja za Moyoni za Ukweli

    ReplyDelete
  9. AnonymousJune 02, 2011

    ohh jamani picha ya huyo mtoto imenitia uchungu sana ohh poor thing too bad

    ReplyDelete
  10. AnonymousJune 03, 2011

    too much!wenye kutuma salamu za rambirambi watume salamu za majeruhi maana ndicho wanachojua tu.no fear

    ReplyDelete
  11. AnonymousJune 03, 2011

    Huyo waziri wa usafirishaji antaka watu wote wafe ili wajuwe kwamba hayo mabasi ni mabovu. Ina maan hatuna sheria za kusitisha usafiri mpka kampun ichunguzwe na kuhakikisha mabasi yao ni salama? Je tufe wangapi ndiyo wahusika wafanye kazi, je kila siku wanfanya kazi gani? kama hawawezi kutetea wananchi?.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...