Na Joseph Ishengoma-MAELELEZO, DAR ES SALAAM
Mhadhili mmoja wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam ameonya kuwa bila Serikali kwa kushirikiana na wadau mbalimbali wa elimu kuwekeza katika sayansi na teknolojia, itakuwa ndoto Tanzania kuwa na maendeleo ya kweli.
Prof. Francis Magingo amesema kuwa hakuna taifa hata moja Duniani lililowahi kuendelea bila kuwekeza katika sayansi na teknolijia.
Mhadhili huyo ambaye ni mkuu wa Kitivo cha Sayansi Asili na Sayansi Tumizi cha Chuo Kikuu cha Dar Es Salaam amesema hayo jijini leo wakati akieleza shughuli mbalimbali zitakazofanywa na kitivo chake kuanzia sasa hadi Juni 30,2011 kama maandalizi ya kuadhimisha miaka 50 ya kuanzishwa kwa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam.
“Bila kuwekeza katika sayansi na teknolojia hatuwezi kuendelea kama Taifa. Katika maadhimisho ya miaka 50 ya kuanzishwa kwa UDSM, tutahamasisha wadau mbalimbali wa elimu kuchangia ujenzi wa jengo la sayansi litakalokuwa na maabara za utafiti za kisasa ili kuwawezesha wanafunzi kupata elimu bora kwa vitendo,” amesema.
Maabara ya utafiti ya kitivo hicho inayotumika kwa sasa inauwezo wa kuchukua wanafunzi 60 tu, wakati wastani wa wanafunzi kwa kila darasa la sayansi ni wanafunzi 300. jengo linalokusudiwa kujengwa litakuwa na maabara itakayochukua wanafunzi 400 kwa wakati mmoja na ofisi za walimu.
Prof. Magingo amesema, “serikali imetoa Dola za Kimarekani milioni nne kwa ajili ya jengo hilo litakalokuwa na ghorofa saba. Fedha hizi zinatosha kujenga ghorofa tatu tu, kiasi lilichobaki tutakitafuta kutoka kwa wadau wa elimu wanaoguswa na mazingira yasiyoridhisha kutoa elimu ya sayansi kwa wanafunzi wetu.”
Katika maadhimisho hayo yanayoendelea hadi mwishoni mwa mwezi Juni, kitivo kinatoa huduma za ushauri za giolojia, maji, mimea, fizikia na hesabu bure kwa wananchi wanaofika chuoni hapo kupata ushauri.
Juni 23,2011, Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia Prof. Makame Mbarawa atatoa mada kuhusu tafiti za kisayansi zilizofanyika nchini miaka 50 iliyopita. Wakati Prof. Karafunja Osaki atatoa mada kuhusu Elimu ya Sayansi nchini miaka 50 iliyopita.


kaka michuzi mbona hamuwatangazii kuhusu apple (kuanzia MacBook Pro) na kuendelea kuhusu bidhaa za apple?
ReplyDeleteHi Braza Michuzi. Email hii ni ya kipuuzi, na wala usingeiweka hapa kabisa, kwani unachangia kuieneza. Ukitumia Google utagundua kwamba hizo model za "laptop" ni za simu (tena iliyopitwa na wakati). Aidha, ukituma email kwenye anwani hiyo, utakuta kwamba ina-bounce.
ReplyDeleteHelow ANKAL MICHUZI.
ReplyDeleteI see the promotional advert by Sonny Ericsson on Laptops.If you can recall some years back,such an advert has been existing and is being modified and Ericsson clarified that such promotional adverts are HOAXES.This advert is a continuation of the same and therefore it is a Hoax.There are no T18 and R320 Ericsson Laptops but cell phones and that mail address to be copied doesn't exist.Ni maoni yangu baada ya kukumbuka yaliyopia miaka ya nyuma.
Mdau.