WHITE & BLACK ni makala ya dakika 58, iliyobeba ujumbe kuhusiana na unyanyasaji wanaopata ndugu zetu wenye ulemavu wa ngozi kwenye jamii tunayoishi. Katika Afrika mashariki, jumla watu wenye ulemavu wa ngozi ni mara kumi zaidi kuliko ilivyo kwa watu wenye ulemavu wa ngozi wanaopatikana katika mabara ya Amerika ya kaskazini na Ulaya. Barani Afrika, mtu mmoja kati ya watu 2000 ana ulemavu wa ngozi.
Nchini Tanzania na sehemu nyingine za Afrika Mashariki, waganga wadanganyifu wamekuwa wakitumia viungo vya watu wenye ulemavu wa ngozi katika tiba zao, wakiamini kuwa viungo vya watu wenye ulemavu wa ngozi huleta bahati na mafanikio.
Makala hii ni zao la utafiti uliofanywa na Vicky Ntetema, Mwanahabari aliyebobea kimataifa, ambaye alizunguka nchi nzima akifanya utafiti juu ya mauaji ya watu wenye ulemavu wa ngozi. Kwenye utafiti wake, Vicky anatupeleka mpaka kwa wahanga wakuu wa mauaji hayo ambao kwa macho yaliyojaa woga mwingi wanaelezea namna wanavyopitia udhalimu huu kila kukicha.
Makala hii imechaguliwa kuingia kwenye Tuzo ya Osmane Sembene, Tuzo ya Filamu inayohusisha Filamu zenye ujumbe wa kimaendeleo, itolewayo na Tamasha la Filamu za Majahazi Zanzibar.
Mdau,
UNDER THE SAME SUN,
TAWI LA TANZANIA.
Kwa habari zaidi tembelea:



Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...