Waziri wa Nchi , Ofisi ya Rais (mahusiano na uratibu),Stephen Wasira (kulia) akibadlishana mawazo na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais (utawala Bora), Mathias Chikawe(kushoto) na Naibu Waziri wa Nishati na Madini, Adam Malima( wa pili kulia) na Mbunge wa jimbo la Kigoma Kaskazini,Zitto Kabwe(wa pili kushoto) wakati wa mapunziko ya kikao cha pili cha mkutano wa nne wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Naibu Waziri wa Fedha ,Gregory Teu (kulia) akibadlishana mawazo nje ya ukumbi wa bunge la Tanzania na Mwenyekiti wa Kamati ya Hesabu za serikali za Mitaa, Augustino Mrema (katikati) na Mbunge wa jimbo la Korogwe vijijini,Stephen Ngonyani (kushoto) wakati wa mapumziko ya kikao cha pili cha mkutano wa nne wa Bunge la Tanzania unaoendelea mjini Dodoma.Picha na Tiganya Vincent-MAELEZO-Dodoma

Kamanda! nahisi kichwa cha habari kimekosewa.... "BUNGUNI DODOMA LEO''' nahisi ulikuwa na maana .."""BUNGENI DODOMA LEO""" au?
ReplyDeleteNchi za Kenya, Uganda na Rwanda Bajeti zao zinasikika moja kwa moja kwenye Mtandao. sisi Watanzania hatuna hata TV au Redio inayosikika "LIVE" kwenye mtadao AIBU sana hii.
ReplyDeleteMagulu
Germany
MAgulu Aibu na wala sio ndogo tutabakia kuwa omba omba kama matonya
ReplyDeleteDuh,Kumbe Mheshimiwa Mrema bado dawa ya Babu(Loliondo) haijamsaidia,maana naona bado ngozi haijakaa sawa.Tuzidi kuomba kwa Mungu amjalie Mh.Mrema apone.
ReplyDeleteAs ante mdau nimerekebisha
ReplyDeleteKwani Mrema hayuko kwenye upinzani tena?
ReplyDeleteAnon Magulu usikonde google clouds fm mimi nimesikiliza bajeti yote. Na nipo Denmark pia wameshaanza live tv yao japo kwikwi kidogo lakini nawapa big5. Redio ni moja tu Tanzania CLOUDS FM. Unajua serikali imebanwa na haka kamuda subiri mpaka uchaguzi ujao upite ndio utapata National TV mtandaoni
ReplyDelete