Mkurugenzi wa Masoko wa Kampuni ya Bia Tanzania (TBL), Davidi Minja (shoto) akikabidhiana mkataba na Katibu Mkuu wa CECAFA, Nicolous Musonye kwa ajili ya udhamini wa mashindano ya Kombe la Kagame yanayotarajiwa kuanza Juni 25 hadi Julai 9 kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaa Tanzania. Katikati anayeshuhudia ni Rais wa CECAFA, Leodger Tenga .

Bia ya Castle Lager itadhamini mashindano ya klabu bingwa Afrika Mashariki na Kati, Kagame Castle Cup yaliyopangwa kufanyika jijini Dar es salaam kuanzia tarehe 25 Juni hadi 9 Julai 2011.

Akiongea na waandishi wa habari kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam, Mkurugenzi wa Masoko wa Kampuni ya Bia Tanzania (TBL), David Minja alisema “Castle Lager imeona ni wajibu kusaidia mpira wa miguu kwani ndio mchezo maarufu zaidi katika nchi za Afrika Mashariki na Kati. Kagame Castle Cup imetupatia fursa ya kuungana na wanywaji wa Castle Lager kupitia mchezo waupendao.”

Minja aliongeza “Udhamini wetu wa michuano ya Kagame Castle Cup ni muendelezo wa mchango wetu kuendeleza mpira wa miguu ili kuhakikisha Afrika Mashariki inakuwa kinara wa soka barani Afrika kama bia ya Castle Lager ilivyo kinara kwa mauzo, usambazaji na upatikanaji barani Afrika. 

Udhamini wetu wetu pia utatoa mchango mkubwa kuhakikisha kiwango cha soka la Afrika ya Mashariki na Kati kinakua katika ngazi ya vilabu na timu za taifa ili mataifa yetu yaweze kufuzu kushiriki kombe la dunia mwaka 2014.

“Ikiwa ni bia inayoongoza barani Afrika, Castle Lager inawajibika kuwa mstari wa mbele katika masuala mbalimbali kwa kuzingatia umuhimu wa michuano ya Kagame Castle Cup kwa Tanzania ambayo inasherekea miaka 50 ya uhuru wake, tumeamua kudhamini michuano hii. 

Uamuzi wetu kujihusisha upya na mpira wa miguu hapa Afrika Mashariki kupitia Kagame Castle Cup utaiwezesha Castle Lager kuendelea kujenga uhusiano na na walaji wake na kuendeleza uhusiano wa muda mrefu na mchezo wa soka barani Afrika”.

Rais wa Shirikisho la Soka Afrika Mashariki na Kati (CECAFA), Leodgar Tenga alitoa shukrani kwa bia ya Castle Lager kudhamini michuano ya Kagame Castle Cup 2011. “Kwa niaba ya wadau wote wa mpira na shirikisho la CECAFA, tunashukuru sana kwa udhamini wa Castle Lager kwa michuano hii,” Tenga alisema. “Mpira wa miguu katika kanda yetu unaendelea kunufaika na misaada ya kifedha,

washabiki wetu wana kiu ya kuona soka la kiwango cha hali ya juu na mafanikio, kupitia msaada huu wa Castle Lager, tutaweza kuandaa mashindano ya ubora wa hali ya juu na kukuza soka katika kanda ya Afrika Mashariki na Kati. Fedha tunazozipata leo zitaelekezwa kwenye timu ili ziweze kufanya vizuri.”

Castle Lager, bia inayoongoza barani Afrika imedhamini mashindano ya Kagame Castle Cup kwa kiasi cha shilingi milioni 300.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...