| Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi,Dk Ali Mohammed Shein |
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi,Dk Ali Mohammed Shein leo amemteua Fatma Gharib kuwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Ustawi wa Jamii na Maendeleo ya Vijana, Wanawake na Watoto Zanzibar.
Taarifa ya Katibu wa Baraza la Mapinduzi na Katibu Mkuu Kiongozi, Dk Abdulhamid Yahya Mzee amesema uteuzi huo umeanza rasmi kunzia leo Juni 15,2011.
Fatma Gharib Bilal aliwahi kuwa Mwalimu na kufanya kazi katika Wizara ya Fedha Zanzibar na kabla ya Uteuzi huo alikuwa akifanyakazi katika Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia maswala ya Idadi ya Watu (UNFPA) Ofisi ya Zanzibar.
Ndugu Fatma Gharib Bilal ana shahada ya Uzamili katika Uchumi aliyoipata nchini Urusi.
Pia Dk Shein amemtaua Omar Khamis Juma kuwa Ofisa Mdhamini katika Wizara ya Katiba na Sheria Pemba.
Uteuzi wa Ofisi Mdhamini umeanza leo Juni 15,2011


Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...