Na Francis Godwin
Pichani ni wananchi wa mjini wa Njombe na maeneo ya Lupembe asubuhi hii wamefika kwa wingi katika Mahakama ya wilaya ya Njombe kwa ajili ya kusikiliza hukumu ya kesi namba 223 ya mwaka 2009 dhidi ya Shoto Shaban ambaye anatuhumiwa kuwapiga wanahabari watano kwa mapanga juni 16 mwaka 2009 walipokwenda kufuatilia sakata la kufungwa kwa kiwanda cha Chai Lupembe

Kesi hiyo ambayo imekuwa na mvuto zaidi imechukua takribani miezi 23 toka ilipoanza kusikilizwa mbele ya hakimu Abeididom Chanjarika wa mahakama ya wilaya ya Njombe na Mei 30 mwaka huu ndio ilikuwa ni siku ya mwisho kwa mashahidi kutoa ushahidi wao .

Wahabari waliotendwa unyama huo wa kukatwa mapanga ni pamoja na Dotto Mwaibale (Jambo leo), Betty Kagonga (Tanzania Daima) Mussa Mkama (mwananchi) Calros Mtoya (majira) na mpiga picha wa kujitegemea Peter Mtitu.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...