Home
Unlabelled
JK ampongeza Askofu Ndimbo leo
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Most read Swahili blog on earth
Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.
Mkono ataka wawekezaji Buhemba wakamatwe
ReplyDeleteNa George Marato
2nd June 2011
Mbunge wa Musoma Vijijini (CCM), Nimrod Mkono, ameitaka serikali kuwakamata wote waliohusika katika uwekezaji wa mgodi wa dhahabu Buhemba wilayani Musoma ili warejeshe mapato yaliyopatikana kabla ya mgodi huo kufungwa.
Mbunge huyo alitoa kauli hiyo katika ukumbi wa halmashauri ya Musoma Vijijini mbele ya Naibu Waziri wa Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, (Tamisemi), Aggrey Mwanri, ambapo alisema halmashauri hiyo pamoja na kubahatika kuwa na madini lakini haikunufaika na raslimali hiyo.
“Kawambie hao wakubwa watukamatie makaburu na wengine wote walihusika kwa uwekezaji wa kifisadi wa mgodi wa Buhemba, mgodi huu umetufilisi sasa wakamatwe waturejeshee fedha zetu ili tujengee sekondari na miradi mingine ya kijamii,”alisema Mkono na kushangiliwa.
Alisema mgodi huo ambao uliitwa kuwa ni mali ya serikali ulikuwa ni danganya toto ambapo ulitumia njia hiyo kuwafilisi wananchi wa wilaya ya Musoma na hivi sasa umefungwa huku ukiacha mashimo makubwa ambayo sasa yamegeuka kuwa makaburi ya wananchi na mifugo.
Alisema kutokana na halmshauri kutokuwa na vyanzo vya kutosha vya mapato kumechangia ongezeko la umaskini na kukwamisha shughuli za maendeleo lakini endapo wahusika watakamatwa na kurejesha mapato ya mgodi huo kutasadia kuinua hali ya uchumi na mapato kwa maendeleo ya wananchi wa halmashauri hiyo.
“Mgodi huu tangu umekuwa hapa hadi unafungwa haukuwahi kuchangia maendeleo yoyote ya wananchi licha ya kuharibu barabara na kuhamisha wananchi wa eneo hilo bila fidia, lakini serikali hadi sasa imekuwa na kigugumizi kuhusu kuwashughulikia wahusika ili watu wa Musoma wapate haki yao,”alisema mbunge huyo.
Hata hivyo, Mbunge huyo aliitaka serikali kuliagiza Jeshi la Polisi nchini kutumia Kanda Maalum ya Tarime na Rorya kudhibiti magendo yanayovushwa na kupoteza mapato ya taifa, badala ya kanda hiyo kutumika sasa kama kichocheo cha ukwepaji wa kodi.
“Kanda Maalum imewekwa lakini hajisadia kudhibiti magendo ili taifa lipate kodi badala yake kanda hiyo imekuwa kichocheo cha kukwepa kodi na kusindikiza bangi kwenda nchi jirani,”alisema Mkono.
Wakati huo huo, Naibu Waziri huyo Mwanri aliutaka uongozi wa halmashauri ya Musoma vijijini kumpa taarifa za maandishi kuhusu matumizi ya fedha kiasi cha zaidi ya milioni 260.
Alisema taarifa ya CAG ya mwaka 2009/10 imebaini kuwepo kwa matumizi yasiyo sahihi na kutokwepo kwa vielelezo ya matumizi hayo hasa katika miradi ya sekta ya afya, kilimo na maji lakini hadi sasa halmashauri haijatoa vielelezo vya kuthibitisha matumizi hayo. Aidha, mbali na kutaka taarifa hiyo pia aliutaka uongozi wa halmashauri hiyo kumpa taarifa za kueleza sababu za kukaa na kiasi cha shilingi milioni 300 kwa mwaka mzima zilizotolewa na Benki ya Dunia kwaajili ya mradi wa maji katika vijiji vya halmashauri hiyo lakini hadi sasa fedha hizo zimehifadhiwa benki.
“Inashangaza sana wananchi hawana maji nyinyi mmekaa na shilingi milioni 300 mwaka mzima sasa hamjatumia hata senti tano sasa nawaagiza kabla ya majumuisho ya ziara yangu Serengeti niwe nimepata maelezo kwa maandishi ili nijue cha kufanya,”alisema Mwanri.
Katika hali ya kushangaza, Mwenyekiti wa halmashauri ya Musoma vijijni Magina Magesa,alitofautiana na Mkurugenzi wake Karaine Kunei kuhusu uuzwaji wa magari ya halmashari bila ya baraka za mamlaka husika. Hali hiyo ilikuja baada ya Naibu Waziri kuhoji taarifa za uuzwaji wa magari hayo ya elimu na maji na alipomtaka Mkurugenzi kutolea maelezo alidai kuwa magari hayo yaliuzwa kwa kufuata taratibu.
Hata hivyo, baada ya Mwenyekiti kusimamishwa kuzungumzia suala hilo, alimkana Mkurugenzi wake na kusema hakuna kikao wala barua iliyoruhusu kuuzwa kwa magari hayo.
CHANZO: NIPASHE