Bai Ling Bo ( wa tatu kushoto) kutoka Jumuia ya wachina waishio nchini Tanzania akimkabidhi Margaret Mkandawire (kulia) ambaye ni Mkuu wa kituo cha kulelea watoto Yatima cha Kurasini jijini Dar es Salaam zawadi za kuchezea watoto wa kituo hicho. Wachina hao walitetembelea kituo hicho jana kwa ajili ya kusherehekea siku ya mtoto pamoja na watoto yatima na kuwapatia zawadi mbalimbali zikiwemo nguo, vyakula, masanduku ya kuwekea nguo viatu, madawa na vifaa vya kuchezea.
Baadhi ya wachina kutoka Jumuia ya wachina waishio nchini Tanzania wakiwa na watoto kutoka kituo cha kulelea watoto Yatima cha Kurasini jijini Dar es Salaam mara baada ya kumaliza kuwagawia zawadi. Wachina hao walitetembelea kituo hicho jana kwa ajili ya kusherehekea siku ya mtoto pamoja na watoto yatima na kuwapatia zawadi mbalimbali zikiwemo nguo, viatu, masanduku ya kuwekea nguo, vyakula, madawa na vifaa vya kuchezea.
Mtoto Nyambu Jumanne wa kituo cha kulelea watoto yatima cha Kurasini jijini Dar es Salaam akichezea kifaa cha kukimbiza upepo alichopewa na Jumuia ya wachina waishio nchini Tanzania. Wachina hao walisherehekea siku ya mtoto jana pamoja na watoto yatima wa kituo hicho na kuwapatia zawadi mbalimbali zikiwemo nguo, masanduku ya kuwekea nguo, vyakula, viatu, madawa na vifaa vya kuchezea.
Jumuia ya wachina waishio nchini Tanzania wakiwa katika picha ya pamoja na watoto pamoja na walezi kutoka kituo cha kulelea watoto Yatima cha Kurasini jijini Dar es Salaam. Wachina hao walitetembelea kituo hicho jana kwa ajili ya kusherehekea siku ya mtoto pamoja na watoto yatima na kuwapatia zawadi mbalimbali zikiwemo nguo, viatu, masanduku ya kuwekea nguo, vyakula, madawa na vifaa vya kuchezea.Picha na Anna Nkinda - Maelezo

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...