Hoja kuwa barabara ya lami inaweza kufuta misafara ya msimu ya wanyama kuhama kutoka upande mmoja kwenda upande mwingine nina wasiwasi nayo.

Madaraka Nyerere
Kwamba nyumbu na pundamilia wanaovuka  mbuga zenye wanyama hatari kama simba, na chui, na wanaovuka mto Grumeti uliyojaa mamba watashindwa kuvuka Barabara ya lami ni mojawapo ya yale masuala ambayo wengine tunayakubali kwa shingo upande kwa sababu tu wanayoyasema ni watu ambao wanasemekana ni wataalamu wa wanyamapori na mazingira. 

Lakini ni hoja ya kitoto, kwa maoni yangu. 

Inawezekana ipo athari ya kiasi fulani itakayosababishwa na barabara ya lami, lakini siamini kuwa athari hiyo itafuta kabisa uwepo wa wanyama hao kwenye sura ya dunia kama inavyodaiwa na hawa wataalamu.

Sishabikii kumaliza wanyama, lakini naamini mahitaji ya binadamu yanawekwa nyuma ya mahitaji ya wanyama. Tatizo ni kuwa wanaharakati wa mazingira hawaambiliki, na hawana muafaka. Tunaamrishwa kumsikiliza wanaosema wao, na hawasikilizi hoja nyingine zozote. Ni baadhi ya hao ambao katika jitihada za kuzuwia kuuwawa kwa baadhi ya wanyama kwa ajili ya kutengeneza makoti ya baridi kwa ajili ya binadamu, wako tayari kuua binadamu hao hao wanaopinga wasivae hayo makoti.

Hakuna tusi kubwa kwa Watanzania kama kusema kuwa mnyama ni muhimu kuliko mwanadamu. 

Ni kweli kwa baadhi ya wenzetu, wanyama ni muhimu sana hata kuliko binadamu. Na tumeshuhudia wanyama kufanyiwa upasuaji na madaktari bingwa kuwatibu maradhi wakati binadamu wenzao wanalala nje bila kufahamu wapi watakula, wacha kupata huduma ya matibabu.

Barabara zilizopo kwenye hifadhi za wanyama katika mataifa mengi yaliyoendelea kunakotoka shinikizo kubwa dhidi ya ujenzi wa hii barabara zimewekwa lami. Tungekuwa tuna uwezo wa kuweka msimamo tungeomba wale wote wanaopinga barabara za lami kwenye mbuga za wanyama kwanza wafumue lami zilizopo kwenye barabara zinazopita kwenye mbuga zao halafu ndiyo waje tukae meza moja kupanga namna ya kuepusha kuweka lami ndani ya mbuga ya Serengeti. 

Umaskini ni tatizo, lakini wenye hoja inayounga mkono ujenzi wa barabara ya lami kupita ndani ya mbuga ya Serengeti tungekuwa na uwezo wa kifedha ingewezekana kabisa kupata wataalamu wetu wakatufanyia utafiti utakaoonyesha kuwa athari ya barabara ya lami kwa nyumbu na pundamlia siyo ya kutisha. Huu ndiyo utaratibu uliyopo nchi zilizoendelea pande zinazokinzana zinapotaka kuvunja hoja ya upande mwingine.

Hoja yangu ya leo ni kuwa umasikini si sifa nzuri, na ina athari kubwa kwa nchi ambayo inajaribu kuwahudumia raia wake lakini inapata shinikizo kutoka kwa wahisani ambao kauli yao ina nguvu kuliko ile ya raia Watanzania.

Hii ni sehemu ya chapisho la Madaraka kwenye blogu yake, bofya hapa kuisoma yote

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 17 mpaka sasa

  1. AnonymousJune 06, 2011

    wapeee wapeeee vidongeee vyaoooooo; wakimeeeza wakitemaa shauriiyaooooo!!

    ReplyDelete
  2. AnonymousJune 06, 2011

    Hapo Madaraka umenena. Nakuunga mkono mia kwa mia. Mikumi mbona wanyama hawajaisha? Lakini pia ukumbuke kikulacho ki nguoni mwako. Hao jirani zako wanahusika kwa kiasi kikubwa kukwamisha barabara hii kwani wanaona watapoteza biashara.

    ReplyDelete
  3. AnonymousJune 06, 2011

    Ninakuunga mkono ndugu Madaraka kwa yote uliyoyasema. Umaskini wetu umekithiri! Viongozi wetu na wataalamu wetu hawawezi hata kufikili tena. Wanadanganywa kama watoto wadogo. Ni kweli mnyama yupo kwa ajili ya binadamu, sio binadamu kwa ajili ya mnyama. Ingawa binadamu analojukumu la kumtunza vema mnyama wakati wa uhai wake. Hao wanafiki wanaodai kuwa watetezi wa wanyama mbona ktk nchi zao hawana hata mbuga za hifadhi? Badala yake wana zoo uchwala. Hata wengine tunajua historia yao- walipovamia nchi ya watu, wakawauwa wenye nchi yao, na kama haikutosha wakawauwa hata na wanyama wote. Eti leo wataalamu na washauri wakubwa wa hifadhi za wanyama!

    ReplyDelete
  4. AnonymousJune 06, 2011

    Mimi nilishasema kuwa barabara hii ni muhimu sana kwani wakenya ndio wanaoongoza kuipinga wakati nchi yao iko vizuri. Kama wahisani hawataki barabari hii ijengwe hapa basi watoe fedha ya kujenga barabara mbadala, wasitukandamize.

    ReplyDelete
  5. AnonymousJune 06, 2011

    Madaraka, mambo mawili. Kwanaza, mwenzangu naona umekosea kidogo. Tanzania si nchi masikini hata siku moja. Tuna dhahabu, almasi, natural gas, na mbuga kibao. Pia usisahau, viongozi wetu wengi tu (I mean politicians) ni matajiri sana. So that part of your argument is flawed. Lakini la pili, kusema kuwa wahisani wanatu-control sana, hilo ni sahihi kabisa. Viongozi wetu Tanzania tangia tupate uhuru wamekuwa wakiombaomba sana wazungu, wachina na wengineo (nisamehe sana, no harm intended in this..)lakini angalia Tazara , UDSM, na mengi mengineo. Ila, wakati wa Mwalimu, japokuwa tukipokea misaada, alikuwa ana msimamo na akiweza kusema NO to IMF, no to this and that!. Lakini, hivi sasa viongozi wetu wanatia aibu. They have perfected the art of begging to the point that seriously building the country becomes counterproductive to the whole mission of constructing an image of desperation to facilitate misaada (read begging). Kwa mfano, hivi kweli ni nani atakosa kutuona kuwa hatuna maana wakati waziri mkuu wetu anaombaomba bila ya breki? Hebu bofya hapa ujionee mwenyewe how embarassing things can get. Ni Aibu tupu. Ndio maana hutuheshimiwi tena na yeyote.
    http://www.youtube.com/watch?v=j2MTRKdDKXk

    ReplyDelete
  6. AnonymousJune 06, 2011

    Kuongezea, hiyo clip angalia yote lakini focus kuanzia dakika 3.06 mpaka 3.10 halafu uone picha unayopata.

    ReplyDelete
  7. AnonymousJune 06, 2011

    nakuunga mkono sana kuhusu maelezo yako,hatuwezi kukaa na barabara za kizamani kwa kuogopa athari ndogo kama hiyo.Lakini wakati huo huo serikali imekuwa ikidangaya(mislead)wananchi kwa nini barabara za Dsm ukiwa hazitengenezwi?Ukiwa Sinza au sehemu nyingine za mjini utafikiria nchi iko vitani wakati tuna amani na wananchi wanatoa kodi na pesa zinatolewa kila mwaka kwa kukarabati?Tufikiri sana watanzania kama tunataka maendeleo na haki lazima tufikirie mfumo mpya wa kuongoza taifa letu ama sivyo tutakuwa tunatoa bla bla na hali za wananchi zinazidi kuwa duni.Viongozi wetu hawafikirii muda alioongoza kaleta faida gani kwa nchi bali kanuua mashamba mangapi,hoteli ngapi na pesa kiasi gani anazo benki.

    ReplyDelete
  8. AnonymousJune 06, 2011

    Kwanza Bw. Madaraka kaongea kitu ambacho Binaadamu yeyote hapa kwetu ataelewa kwa kuongezea tu naomba watanzania waelewe kuwa nchi yetu si masikini hii kauli yao ya kusema kila siku sisi masikini ni kauli ambayo wanataka ieleweke hivyo kwenye jamii yetu ili watuminye vizuri. Nchi yetu ni tajiri ila hawa viongozi wamepoteza uzalendo wanatuibia, wanafuja pesa za wananchi, Angalieni matumizi ya viongozi wa serikali yetu kweli mtasema sisi ni masikini? Haya mambo mengine yatupasa kuyakabili sisi wenyewe siyo kila kitu kuwasikiliza hao binaadamu wa nchi za magharibi kama kweli tunataka Demokrasia Raia hasikilizwi ila kutunishiwa misuli na kufanya watakavyo. huko serengeti kuacheni kama kulivyo (NATURE) ina nguvu zake zaidi ya elimu zenu nchi yetu miaka 50 ya uhuru bado kuna wanafunzi wanakaa chini, kuna barabara ambazo viongozi hawapiti kila mara hazipitiki kwa nini msizishughulikie hizo kwanza? Nchi yetu hawa viongozi wanaleta makataba ambayo hatukuwa nayo kuona leo hii kuna mikoa imedoda na sidhani hata kama wamo kwenye Budget za serikali lakini wanajuwa huko kuna njia za ufisadi basi kunapewa kipao mbele. Angalieni Nchi za Scandnavia ni Norway tu ndiyo yenye mafuta, zingine ni kilimo , uvuvi, na viwanda vitu ambavyo Tanzania yetu tunaweza lakini viongozi hawataki watu muwe na maisha mazuri itakuwa vigumu kwao kutawala.

    ReplyDelete
  9. AnonymousJune 06, 2011

    Lakini huyo jirani yenu Kenya mnamuonaje? Anachangia kwa kiasi kikubwa kukwamisha maendeleo ya Tz ili asipate mshindani. Ni wanafiki hao jamaa. Lazima tuchachamae kupambana na vizabinabina kama hao.

    Hata hivyo lack of seriousness ya watanzania pamoja na ufisadi vinaweza kweli kusababisha wanyama hao wakapukutika. Laiti Watanzania wangekuwa wanafuata taratibu zinapowekwa, hiyo barabara ingepita bila kuua mnyama hata mmoja.

    ReplyDelete
  10. AnonymousJune 06, 2011

    Ni ukweli Madaraka Nyerere unaona mbali.
    KIA .Kilimanjaro international airport kulikuwa na wanyama zamani lakini.
    Swala la wanyama kuisha litakuwepo tu hata tukijindanganya, cha msingi ni kujenga barabara ya chini kwenye sehemu ambazo wanyama wanavuka hata kwa kiwango cha kl 1 mpaka tatu,ili wanaya waendelee kupita kwenye njia zao kama kawaida yao.

    ReplyDelete
  11. Nimesikitika saana na hoja ya ndugu Madaraka, inaonyesha upeo mdogo wa kielimu uliopo miongoni mwetu. Upeo mdogo ambao umechangia kuharibu mazingira na kutuletea majanga mengi ambayo hayakuwepo zamani. Kusema kuwa wanyama wapo kwa ajili ya mwanadamu ni ujinga unaotokana na ukosefu wa fikra na elimu. kila mnyama na mdudu aliyepo katika dunia hii ana nafasi muhimu katika mfumo mzima wa maisha (natural order).
    ukosefu wa kuona mbali pia ni tatizo anfikiri ndugu Madaraka hajafikiria Tanzania baada ya miaka 200 ijayo tutakuwa wapi. tukianza kujenga barabara nani atakayezuia kujengwa mahoteli na mwisho mbuga kugeuzwa zoo.. Tuna utajiri wa nature lakini kutokana na fikra ndogo kama za kina Madaraka kila kukicha tunafilisika. Leo hii wazungu wanajuta kama wangelijua wasingeua wanyama wao hata ikabidi kutenga misitu na kurudisha wanyama waliowatokomeza kwa fikra kama hizo za Madaraka kwamba mahitaji ya wanyama yaje baada ya binadamu. Leo hii kama huna leseni huwezi kwenda kutazama ndege katika misitu. Sie tuna utajiri wa wanyama wa kila aina bali na uzuri wao wanafaida kubwa katika fauna na flora. Wanyama hawapo kwa ajili ya mwanadamu, wapo katika nafasi sawa katika kuhakikisha balance ya Natural order inawekwa na hivyo kufanya maisha katika dunia kuendelea. Jongoo ana nafasi kubwa katika muendelezo wa maisha ya mwanadamu kuliko hayo mwanadamu anayofanya. Bila ya kuwepo Nyuki duniani Wanadamu na wanyama wengine wote watakufa katika kipindi si zaidi ya miaka minne. Kwa hiyo kabla hamjafanya maamuzi kisiasa fikirieni nini elimu inasema. Umasikini tulionao si wa mali bali ni wa FIKRA (ukosefu wa elimu).

    ReplyDelete
  12. AnonymousJune 06, 2011

    Jamani kama Watanzania tulivyoweza kuwa katika frontline ya ukombozi wa Afrika ni lazima tuwe katika frontline ya ukombozi wa mazingira yetu na kuonyesha mfano kwa nchi zingine za Afrika. Kuhifadhi mbuga za wanyama haina maana kwamba tunaweka mahitaji ya wanyama mbele bali ni mojawapo ya maendeleo yetu ya kuvutia watalii wa ndani na wa nje. Sisi kama Watanzania ni lazima tuliangalie suala hili kwa makini sana. Je, kujenga hiyo bara bara ni maendeleo au la, wanyama wataathirika au la na uamuzi ufanywe na jopo la wataalamu na sio wanasiasa pekee yao. Na pia Watanzania tuwe makini kuna watu wa nje ambao wanatupenda na kuipenda nchi yetu hao ndio inabidi tushirikiane nao. Haina maana kuwa hawatupendi eti kwa sababu wanapinga ujenzi wa barabara. Wewe unayeunga mkono ujenzi huo unaweza kutuhakikishia kwamba vijukuu vyetu vitapata nafasi ya kuwaona hao wanyama?

    John Kijiko

    ReplyDelete
  13. AnonymousJune 06, 2011

    Nakubaliana na kauli ya Madaraka kwa kweli watanzania ni maskini wa mawazo sana sioni tatizo lolote la Serengeti kuwekwa lami hayo mashirika ya nje kutuamulia mambo ya ndani ni sawa na baba kuamuliwa maswala ya nyumba yake na watu wa nje tusikubali hata kidogo Serekali inapoteza hela nyingi sana kujaza kifuzi na kupiga crader mara kwa mara pili magari yanaumia sana na na Serekali inatumia pesa nyingi za kigeni kuagiza spare mashirika ya nje hawapati hasara yeyote sisi watanzania wenyewe ndio tunajiumiza kuwasikiliza.

    AMKENI SASA

    ReplyDelete
  14. AnonymousJune 06, 2011

    Lami ijengwe.zile sehemu ambazo wanyama wanatumia kuvuka ziachwe na kifusi lakini kilichokuwa-Graded.Wanyama watachagua sehemu ya kuvukia..Kama wanaona kukanyaga Lami kunawakera basi lazima watakwenda kuvukia kwenye kifusi,wanyama wana akili.!(Porojo-sina uhakika kama ni 'practical'hii).

    ReplyDelete
  15. AnonymousJune 06, 2011

    Namuunga mkono Mwanafunzi. Wewe unautalaamu gani? Zaidi ya wataalam 30 wametoa maoni yanayofanana na nyinyi mnaleta siasa kwenye utaalamu, je tutafika kweli? Subirini Tz itakapokuwa kama Nigeria ambako sasa ni kama hakuna wanyama wa aina yo yote tuone kama hamkufunga hoteli zote na kumpunguza kiwango cha ushiriki wetu katika biashara za kimataifa. Kwanza hapa tulipo karibu watu watakuwa wanabeba magunia ya hela kununua vitu vya kawaida.

    ReplyDelete
  16. AnonymousJune 06, 2011

    Tanzania ni nchi pekee Duniani yenye wanyama wengi. Wewe mura Madaraka kumbuka nasaha za mwalimu Nyerere. Nafikiri humfahamu hii inaonyesha jinsi gani mamba anavyoweza kuzaa nyoka.

    ReplyDelete
  17. AnonymousJune 07, 2011

    Kimsingi Madara anazungumzia upande mamoja tuu ambao unaweza kuonekanika kua mzuri leo lakini kesho ukajutiwa.

    Binadamu tunategemea mzingira yetu na si mazingira yanatutegemea. Ubora wa mazingira yetu yanayafanya maisha ya binadamu kuwa bora. Maendeleo si kuwa na barabara itakayoadhiri mazingira bali maendeleo ni kuwa na vitu vitakavyoendeleza ubora wa mazingira na maisha ya mwanadamu leo na kesho na kuendelea.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...