Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohamed Gharib Bilal na mkewe, Mama Zakhia Bilal, Balozi Obeni Sefue na Waziri Juma Duni Haji, wakisimama na kuimba wimbo wa maalum baada ya kuwasili kwenye eneo la hafla hiyo.
Mwenyekiti wa Jumuiya ya Watanzania waishio New York na vitongoji vyake, Haji Hamis, akizungumza na kutoa utambulisho wa viongozi na wanachama wa Jumuiya hiyo, ambao hadi sasa wamefiki 110.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiwahutubia Watanzania waishio New York na Vitongoji vyake, wakati alipokutana nao kwa ajili ya mazungumzo nao na kuwatambua, ikiwa ni mara ya kwanza tagu alipoteuliwa kushika nafasi hiyo.
Baadhi ya Watanzania waishio New York na vitongoji vyake wakimsikiliza kwa makini Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed gharib Bilal, alipokuwa akiwahutubia.

kwa picha zaidi
BOFYA HAPA



TUTAZINGATIA MAONI NA USHAURI 
KUHUSU KATIBA, ASEMA DKT. BILAL


Na Mwandishi Maalum
New York
Serikali  imesisitiza nia yake ya kuhakikisha kwamba zoezi la kukusanya maoni, ushauri na mapendekezo kuhusu mchakato wa  kutungwa kwa Katiba mpya linafanyika kwa  uwazi na umakini mkubwa.

 Hayo yameelezwa na  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Ghalib Bilal wakati alipokuwa akisalimiana na watanzania wanaoishi katika jijini la New York na vitongoji  vyake.

Katika mazungumzo yake na watanzania hao yaliyofanyika  siku ya jumapili katika Makazi ya Balozi wa Tanzania  katika Umoja wa Mataifa. Makamu wa Rais amesema,  ni dhamira ya serikali kuhakikisha  siyo tu inawapa wananchi fursa ya kutoa maoni,  ushauri na mapendekezo, lakini kila hoja itakayotolewa itazingatiwa kwa kadri ya  uzito wake.

“ Tumeanza zoezi hili,  ni zoezi ngumu lakini  ni zoezi muhimu sana katika kukuza na kudumisha demokrasia yetu. Ni zoezi ambalo linavuta hisia za watu wengi na linafuatiliwa kwa makini sana na wadau mbalimbali wakiwamo wa ndani na nje.” Akasema Makamu wa Rais.

Na kuongeza kuwa  mchakato huo pia unafuatiliwa  na majirani zetu ndani ya Jumuia ya Afrika  Mashariki  (EAC)na Jumuia ya Maendeleo ya Nchi za Kusini mwa Afrika ( SADC). “ Kinachofanyika hivi sasa nchini Tanzania  kinakuwa na rasharasha katika sehemu mbalimbali, wanafuatilia kuona nini kitatokea na hii ni ishara nzuri” akasisitiza.
Akasema kuwa  hamu ya wadau hao kuufuatilia mchakato huo,  inatokana na sababu nyingi lakini kubwa ni kuwa Tanzania bado ni nchi nzuri na inayozingatia   utawala wa kidemokrasia.

Akijibu maswali na hoja mbalimbali zilizotolewa na watanzania hao. Yakiwamo maswali kuhusu matatizo ya umeme, mfumuko wa bei hasa kwenye mafuta,  uraia wa nchi mbili na fursa za kupata  ajira nchini Tanzania.

Katika kuelezea tatizo la umeme, Dkt. Bilal alikiri kuwapo kwa tatizo  hilo, na akaainisha hatua ambazo serikali imechukua kukabiliana nalo, baadhi  ya hatua hizo ni pamoja na  kutafuta vyanzo vingine vya umeme kama vile umeme wa  upepo, umeme wa gesi asilia na umeme utakao tokana na makaa ya mawe.

Akasema  matatizo hayo ya umeme yamekuwa na athari nyingi katika utendaji kazi na ukuaji  wa uchumi. Aidha ameeleza kuwa tatizo la umeme linachangiwa na mambo mengi kama vile upungufu wa mvua na uongezeko la matumizi ya nishati hiyo.
Kuhusu bei ya mafuta, Makamu wa Rais alisema  kupanda kwa bei ya mafuta   ni tatizo la dunia nzima. Hata hivyo akasema kuwa kuna chombo ambacho kimepewa kazi ya kudhibiti bei ya mafuta na  ubora wake.

Akasema chombo hicho (EWURA) kina mamlaka yote,  tena kiko huru na hakiingiliwi na mtu yeyote.  Hadi sasa kinafanya kazi nzuri. Lakini kinauwezo wa kufanya  kazi nzuri zaidi kwa kuwa hakiingiliwi na serikali  na  akaeleza kuwa atashangaa sana kama chombo hicho kitashindwa kutekeleza majukumu.

Kuhusu hali ya chakula, Makamu wa  Rais alisema kuwa baadhi ya maeneo ya nchi yatakuwa na upungufu mkubwa  hasa kwa zao la mpuga kutokana na uhaba wa mvua. Hata hivyo akasema serikali imejiwekea mipango madhubuti ya kuhakikisha kuwa wananchi watakaopungukiwa   chakula wanapata chakula kutoka hifadhi ya taifa.

Wakati huo huo, Waziri wa Afya  kutoka Serikali ya Mapinduzi  Zanzibar, Mhe. Juma  Duni Haji amewataka watanzania wanaoishi ughaibuni kuacha kulalamika na kulaumu.
Alikuwa akichangia kujibu maswali  kuhusu nini serikali inafanya katika uboreshaji wahuduma za afya .

 “ Serikali inafanya lile linalowezeka na kila jambo linafanywa  kwa wakati wake na kwa kipaumbele chake, matatizo ni mengi na hayawezi kutatuliwa yote kwa wakati mmoja. Lakini nitoe rai yangu, acheni kulalamika na kulaumu, muda wa kulalamika na kulaumiana umeshapita. Kinachotakiwa ni kushirikiana sote katika kujenga nchi yetu” akasisitiza Waziri wa Afya. 




Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...