Familia ya Hatia inasikitika kutangaza kifo cha baba mzazi wa msanii maarufu katika fani ya filamu nchini Mrs Christina Innocent Marolen a.k.a   Mama Bishanga,  Mzee Isaya Innocent Hatia (mtoto wa Mwenye Hatia Chifu wa Wamakua, Ashinnahatia) aliyefariki  dunia katika hospitali ya Ndanda, Masasi, Mkoani Mtwara jana. 
Amefariki akiwa na miaka 82.

Marehemu ameacha mke Mwalimu Agnes Hatia, watoto saba ambao ni Mama Bishanga, na wadogo zake Geofrey anayeishi Namibia, Mwalimu Marck  wa Azania Sekondari, Bernadeta, Isaya anayeishi Finland, Constancia na Oscar. Pia ameacha wajukuu na vitukuu kadhaa.
 
Mzee Hatia atakumbukwa kwa kuwa mmoja wa wafanyakazi bora na wa muda mrefu wa kampuni ya Posta na simu tangu enzi za East Community  huko Nairobi na Mombasa, na pia  Dar es alaam, Dodoma na  Tabora.
 
Mazishi yatafanyika kesho Ijumaa huko huko Ndanda.

Mola aiweka Roho ya Marehemu Mahala pema Peponi
-AMINA

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. AnonymousJune 09, 2011

    Poleni sana ndugu na familia ya Mzee Hatia kwa ujumla kutokana na msiba wa baba yenu mpendwa,Tunaomba mungu ailaze pahali pema roho ya marehemu mzee wetu,kilichopangwa na mola sisi binadamu hatuwezi kukipangua.Pia ningependa kuuliza hizi familia za akina Wamwenye asili yake ni sehemu gani ktk wilaya ya masasi ?? Nauliza hivi kwa kuwa sisi pia baba ya babu zetu alikuwa na jina hili na katika kuulizia tu tukaambiwa asili yake ni wilaya ya Masasi,kwa hiyo babu zetu walizaliwa mkoani Tabora na wakalowea huko,Sisi kama wajukuu tuajaribu kutafuta hasa asili ya baba ya babu zetu(roots) alitoka sehemu au kijiji gani huko Masasi,Nategemea wadau mtanisaidia kutokana na majina haya ya akina Wamwenye mnaweza kujua yana asili ya vijiji gani huko wilayani Masasi.
    mdau Washington Dc.Usa.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...