Waziri wa mambo ya Nje wa Marekani Mama Hillary Clinton akiongea baada ya kutembelea mtambo wa kufua umeme wa kampuni ya Kimarekani ya Symbion Power Ubungo, jijini Dar es salaam. Shoto ni Bw, Daniels Yohannes, mkuu wa ,mfuko wa MCC na kulia ni mtendaji Mkuu w Symbion Power Bw. Paul Hinks
 Waziri wa Nishati na Madini Mh. William Ngeleja akifafanua jambo baada ya ziara ya Mama Hillary Clinton ya mtambo wa kufua umeme wa Symbion Power uliopo Ubungo, Dar es salaam
  Mama Hillary Clinton akisalimiana na Bw. Mohamed Saleh, mmoja wa mabosi wazalendo wa Symbion
Mama Clinton akiwa katika mtambo wa kufua umeme wa Symbion Power huko Ubungo jijini Dar es salaam. Kulia kwake ni Mtendaji mkuu wa kampuni hiyo Bw. Paul Hinks na kushoto wapo Mkuu wa mfuko wa MCC Bw. Daniel Yohannes na Waziri wa mambo ya nje na uhusiano wa kimataifa, Mh Bernard Membe.
Kwa picha zaidi BOFYA HAPA

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 6 mpaka sasa

  1. Waheshimiwa kupendeza wamependeza. Lakini UMEME wa uhakika sie wanyonge tutapata?:-(

    ReplyDelete
  2. AnonymousJune 13, 2011

    TANESCO
    JE UMEME WA MGAWO NDIYO UMEKWISHA AU HAYO NI MANJONJO YA KUMUONA
    HILALY CLINTON

    MAANA DUH KESHO TU UMEME HAKUNA
    JE TUTAFIKA?

    ReplyDelete
  3. AnonymousJune 13, 2011

    Ahh kumbe ndo mana iliwashwa, coz boss anakuja? Ngoja aondoke mwezi mmoja tutaanza kusikia hamna mfuta ya kuendeshea mitambo....bongo tambarare!

    ReplyDelete
  4. AnonymousJune 13, 2011

    Huu mradi ni wa akina Clinton au?, maana kutembelewa na Secretary of State wa marekani nchini ni ujio mkubwa. Halafu kaja kimya kimya. Ajabu hii interest inaleta maana fulani ndani au ndio wanaanza kidogo kidogo kuingia katika hema, kichwa kwanza. Watanzania amkeni.

    ReplyDelete
  5. AnonymousJune 13, 2011

    MMMMmmmmh kama naota vile!

    ReplyDelete
  6. AnonymousJune 13, 2011

    Aaaahh! Watanzania kazi yenu ni porojo tu, matumizi ya maarifa na uono wa mbali kimanufaa hakuna kitu!! Hii Symbion si dio ile iliyokuwa Dowans ambayo Mtaalam fulani akapendekeza inunuliwe na serikali ili kuinusuru nchi? Baada ya hapo kukawa na kelele nyingi kuwa eti Mtaalamu kala kitu kidogo, na ndio pale aliposema kuwa wagonjwa mahospitalini wakifa na wanafunzi vyuo vikuu wakashindwa kufanya revision kwa kukosa umeme lawama zisimrudie yeye, Mheshimiwa sana mmoja nae akapendekeza kuwa huyo mtaalamu aadabishwe kwa maneno yake (ambayo kimsingi ni ya ukweli, si wagonjwa walikufa wengi tu?).
    Cha ajabu wenye maendeleo makubwa kuliko wote duniani wamekuja kuinunua mitambo hiyo ambayo sisi tulijidai eti ni michakavu!!!! Procuremeny Act yetu ilikataa!! Hivi hao Wamarekani ni wajinga kununua mali chakavu yenye manufaa makubwa? Tuache kujifanya wajuaji kumbe hamna kitu.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...