Na Freddy Macha, London

 Mchoraji wa rangi, vitabu na stempu, Raza Mohamed anatazamiwa kufanya maonyesho ya picha zake katika ukumbi wa  Mulberry Tea Room, Charlton House, kitongoji cha Greenwich Ijumaa tarehe 17 Juni hadi Jumatano 20, Julai mwaka huu.

Raza Mohamed ambaye ni hazina ya taifa letu amekuwa akichora toka akiwa mtoto wa miaka sita tu mwaka 1952. 
“Nilianza kwa mkaa...” alisema nilipomhoji nyumbani kwa mwanae, jana. 
Soma habari zaidi katika blog la Kitoto:



Raza, hazina ya taifa letu; akiwa na mwandishi wa blog la Kitoto, Freddy Macha, London, Juni 2011. Picha na Louisa Le Marchand



Raza na picha ya “Watoto wakicheza Mdaku” iliyopigwa Unguja na F Macha.





“Chai ya Asubuhi” ni Moja ya picha zake msanii Raza Mohamed zitakayoonyeshwa  Charlton House, Greenwich,  London.  Imepigwa na F Macha


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 4 mpaka sasa

  1. AnonymousJune 08, 2011

    huyu mzee ni kweli hazina ya taifa nakumbuka amechora picha katika vitabu vingi nilivyosoma shule ya msingi.

    MUNGU AMBARIKI SANA MZEE RAZA NA AMZIDISHIE MAISHA MAREFU

    ReplyDelete
  2. AnonymousJune 08, 2011

    Hiyo caption ya watoto wakicheza mdako sijui kama inafaa. Nijuavyo mdako ni shimo moja lakini hapo nionavyo mimi walikuwa wakicheza bao. Kama nimekosea niwie radhi Ankal.

    ReplyDelete
  3. AnonymousJune 08, 2011

    Hiyo picha ya watoto ni kuwa wanacheza bao sio MDAKU!!

    ReplyDelete
  4. AnonymousJune 08, 2011

    Hongera Sana Raza. I am proud of your hardworking and talent.As per our conversation at the Diaspora, you have got what it takes to make a breakthrough on an International market. All Tanzanians are behind you in support.Well done and keep it up! Maseke(East Midlands).

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...