Salaam,

Nakupongeza kwa kazi nzuri sana. Kuna hili jambo nimelifuatilia kwa karibu nikaona hakuna njia muafaka ya kulifikisha kwa wahusika isipokuwa kupitia blog ya jamii. Maana nimejaribu kuwaona mpaka Viongozi wakuu wa Wizara husika lakini sikufanikiwa. 

Suala lenyewe ni hili. Wizara ya Ardhi chini ya Katibu Mkuu mama Sijaona ilianzisha mradi wa kupima Viwanja katika Jiji la Dar, maarufu kama Mradi wa Viwanja 20,000. Nadiriki kusema pamoja na matatizo madogo ya hapa na pale mradi ule ulifanikiwa sana. Nia ilikuwa kupunguza makazi holela (Skwata).

Baada ya hapo Wizara ikalishusha hilo jambo katika Halmashauri za Manispaa, Miji na Wilaya. Tunaita 'ku-decentralize'. Mpaka ninapoandika waraka huu, hakuna katika Manispaa tatu za Jiji la Dar ambayo imeweza kufanikiwa kupima na kugawa japo viwanja elfu moja. 

Na mpango wenyewe uko hivi, Wizara 'inazikopesha' Manispaa fedha kwa ajili ya kutwaa, (kuchukua maeneo ya watu na kuwalipa fidia) kupima na kuuza, baada ya hapo fedha zinarudi Wizarani. Manispaa inapata faida, wananchi wanapata viwanja vilivyopimwa-Surveyed plots. Huo mfuko unaitwa Revolving Fund. Sasa kuna mengi yamejitokeza

1. Uvamizi katika maeneo ya ukanda wa kijani ‘Green belt’

Watendaji wa Manispaa wamewauzia wananchi maeneo ya ukanda wa kijani 'Greenbelt' kiasi kwamba ile mantiki hasa ya kupima maeneo ili kupunguza Skwata imekuwa haina mantiki tena. Ukiwaambia Manispaa,hakuna hatua wanazochukua,Mimi Binafsi nimemueleza Meya wa Manispaa ya Ilala ana kwa ana. Akaahid kuchuku hatua, lakini nadhani ni ahadi tu.

2. Uvamizi wa maeneo ya wazi,viwanja vya michezo na huduma za jamii.

Katika maeneo mengi ya Mradi wa viwanja 20,000, Wizara ilifanya kazi nzuri sana, ilifanya kitaalam haswa,ikatenga maeneo kulingana na matumizi na mahitaji. Jambo la kusikitisha maeneo hayo pia yanavamiwa na wanaoongoza kufanya hivyo ni watendaji wa Manispaa, Wizara ukiwaambia wanasema kuwa wao ni wasimamizi wa Sera, hilo la kulinda maeneo ni la Manispaa. Nikawauliza hata kama ni Sera, mbona nimemsikia Mhe Rais akisema Dodoma 'I want to you guys out there on the field' je hamuwezi kufika mkakagua maeneo na kutoa maagizo,makaripio au onyo?

Pendekezo

Kwa uzoefu wangu,maana nilishiriki uzinduzi wa Mradi wa Viwanja 20,000 pale Temeke (Tuangoma), na pia nilishiriki kutatua baadhi ya migogoro iliyojitokeza kama vile baadhi ya watu wasiostahili kulipwa fidia nk. 

Nimeshuhudia kwa ukaribu kabisa kuwa Mradi wa Viwanja elf tatu (3000) katika Manispaa ya Ilala umechukua miaka zaidi ya mitatu haujakamilika,na hata juzi hapa walipotaka kuuza viwanja hivyo wameishia kugawa (kuuza fomu) kwa shilingi elf ishirini (20,000/=) na mpaka leo hakuna kinachoendelea maana wao, wametwaa maeneo,hawakulipa fidia wenye maeneo,wakapima wakataka kuuza,wenye nacho wakaja juu (kumbuka kuwa mwongozo unasema unatwaa eneo,unalipa fidia,unapima ndo unauza)wao wametaka kuuza maeneo bila kuwalipa wamiliki wa awali fidia.

Kadhalika Manispaa ya Temeke, juzi kwa mbwembwe wakatangaza kuwa watauza viwanja,wananchi wakaminika kuchukua fomu na kulipia, wakaishia kutoa fomu mia nane tu (800), na hata hilo zoezi nina mashaka. Manispaa ya Kinondoni, mara mbili mwaka jana na juzi waliuza fomu,mpaka leo uliza kama wananchi walipata hivyo viwanja. Ndio maana nasema

Serikali inaweza ku-decentralize mambo mengi lakini kwa hili na hasa kwa Jiji la Dar imethibitika kuwa Manispaa zetu haziwezi. Hivyo basi Wizara ya Ardhi na Maendeleo ya Makazi ichukue tena jukumu hili kama ilivyokuwa kwa Mradi wa Viwanja 20,000. Madiwani na Manispaa watapiga sana kelele, maana itakuwa ni kuwaondolea ‘ulaji’ lakini linapokuja suala la Maendeleo ya watu,acha wachache wapige kelele,wengi wanufaike.

Mtu ni Utu-Tanzania yenye Neema Inawezekana.
Mdau wa Maendeleo ya kweli.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 7 mpaka sasa

  1. AnonymousJune 13, 2011

    MRADI HUU NI UCHOCHORO MKUBWA WA RUSHWA KWA WATUMISHI WA ARDHI WALIOKO MANISPAA, WATU WANAOTAKA WACHAGULIWE KUNUNUA HIVYO VIWANJA WANABIDI WAHONGE PESA ZAITWA ZA SIMU, VOCHA NA SODA KWA WATUMISHI HAO TENA RUSHWA HIZO ZINAFIKA AU HATA KUZIDI LAKI 1 KWA KIWANJA.

    TENA HUO NI ULAJI NA NJIA YA KUWAIBIA WATU MAENEO YAO KISHA WATUMISHI HAO WANAJIMILIKISHA VIWANJA AMBAVYO HUVIUZA TENA BAADAE.

    TUMECHOKAA NA UOZO WA MANISPAA ZETU ZINHITAJI SHUFFLING KWANZA HAZIENDI NA WAKATI PILI NI SOURCE YA MIGOGORO MINGI YA ARDHI, BORA MASUALA YOTE YARUDI WIZARANI AMBAKO TUNAJUA UNAWEZA KUMUONA KATIBU MKUU UKAMWAMBIA KILIO CHAKO AKAKUSIKILIZA.

    ReplyDelete
  2. AnonymousJune 13, 2011

    AMA KWELI NCHI YETU IMEOZA
    HAO WOTE NAAMINI HAWAKO SERIOUS KATIKA KILA JAMBO NDIO MAANA WAAFRIKA HATUENDELEI

    SIJUI MADIWANI WETU
    MA MEYA WETU WOTE WAMEROGWA KIASI KWAMBA HAWAONI MADUDU WANAYOYAFANYA
    NIPENI FIMBO NITAWACHARAZA KWELI KWELI.

    USIIWEKE KAPUNI HII COMMENT YANGU

    BORA VIWANJA VIRUDI WIZARANI TU.

    ReplyDelete
  3. AnonymousJune 13, 2011

    Wizara ya Arthi enzi za Mama Sijaona ndio mambo yalikuwa yakienda safi sana, walipima viwanja 20,000 Dar, walipima maeneo mengi ya mashamba huko vijijini, walitoa hati za makazi zinazokubalika na vyombo vya fedha na sheria, walianza kutumia mtandao wa komputa kuhifadhi kumbukumbu n.k...mafanikio kede kede. Hata hii migororo ya Arthi mpaka Watanzania wanachinjana haikuwepo...

    Leo, hasa Arusha viwanja vimegawiwa kwa vigogo tu...na hata hatujui kipaumbele cha Wizara kwa sasa ni nini. Rudisheni hilo jukumu Wizarani Wananchi wapate viwanja...

    ReplyDelete
  4. AnonymousJune 13, 2011

    Hivyo viwanja by the time mnatangaziwa wafanyakazi wa manispaa na wa wizara wote sawa sawa, wameshaviidentify na kuvigawa kwa jamaa zao. Hali hiyo niliikuta tokea vile viwanja vya mwanzo Bunju, Tuangoma, na juzi Gezaulole. Mtu mmoja anachukua fomu 100 na analipia unatemea nini. Kule Bunju tuliambiwa tuende ofisi iliyopo mwananyamala, niliwahi pale asubuhi nikamkuta ofisa mmoja ninamjua anachora maeneo na yeye yuko katika kuwatafutia jamaa zake, mimi alinisaidia lakini zile area nzuri zote siku ya kwanza zilikuwa zishaisha. Sasa wanaviuza kwa bei ya juu. Vijana wengi wa Wizara ni matajiri, wanajisifia mambo yamewanyookea. na wengi wameshajenga. Prof. Tibaijuka mwenyewe hawezi kuwapata hawa vijana wa leo anaowaongoza wizara, they are too smart. It is too late to control the lot.

    ReplyDelete
  5. AnonymousJune 13, 2011

    Hahaha ufisadi bongo ni kwa kwenda mbele. Hapo ilitakiwa watu waandamane mpaka foleni ya iheshimiwe. Haya mambo ya wafanyakazi kujichukulia form kinyemela hayakubaliki. Kila mfanyakazi asiye na nyumba anapewa form moja tu basi. Waliobaki wote foleni. Tatizo TZ hatuna utamaduni wa foleni. TZ bado tuna utamaduni wa kupata mali kwa ufisadi. Hiyo ni kila sehemu ya kazi. Kila anayetoa huduma ni fisadi. Awe trafiki, nesi, profesa, mwalimu, tra, daktari, mpimaji viwanja, mbunge, raisi, waziri, bima, nssf, nk. Je hawa wafanyakazi ni CCM? Je mbona CHADEMA hatusikii wakipigia kelele mambo haya.

    ReplyDelete
  6. AnonymousJune 13, 2011

    Mimi ni mmoja wa wale waliofanikiwa kununua kiwanja kupitia ardhi chini ya mradi wa viwanja 20,000. Sikutoa rushwa na wala sina ndugu hapo ardhi na nilipata title deed within a very short time. tena kiwanja changu ni low density. Kama hao manispaa kila mtu anaona ni wazushi basi ardhi warudishiwe kazi ila serikali ihakikishe kuna katibu mkuu mwenye commitment na kazi yake si wale wanaokalia kubrowse internent baada ya kuwa reachable kwa wananchi wenye malalamiko

    ReplyDelete
  7. AnonymousJune 13, 2011

    Kilio Chetu ni uvamizi wa maeneo ya Green Belt (Ukanda wa Kijani) na mabonde (Storm Water Drainage) katika eneo la KINYEREZI. Tumewasilisha malalamiko yetu juu ya hili Manispaa ya Ilala, kuanzia serikali ya mtaa hadi kwa mkurugenzi wa Manispaa na hakuna mvamizi yeyote aliyevunjiwa na wanaendelea kujenga. Tunamuomba Meya Silaa pamoja na mkurugenzi kusitisha uvamizi huo. Manispaa hiyo ina jukumu la Development Control kama sheria ya Mipango Miji inavyoelekeza. Waziri wa Ardhi na Katibu Mkuu TAMISEMI sikia kilio chetu

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...