HABARI ZIMETUFIKIA MUDA HUU KWAMBA MJINI DODOMA KUNA RABSHA KATI YA WANAFUNZI WA UDOM WA KITIVO CHA SAYANSI YA JAMII NA ASKARI POLISI AMBAO INASEMEKANA WAMEWEKA ULINZI KUWAZUIA WASIKARIBIE JENGO LA BUNGE AMBAKO WAMEENDA KWA NIA YA KUTAKA KUTOA MALALAMIKO YAO YA KUFUTWA KWA MAZOEZI KWA VITENDO (FIELD) HALI ILIYOPELEKEA WAO KUGOMA KUINGIA MADARASANI.
TUNAFUATILIA MATUKIO HAYA NASI KAMA
LILIVYO ADA TUTAWAJULISHA KADRI YATAKAVYOTUFIKIA
TUNAFUATILIA MATUKIO HAYA NASI KAMA
LILIVYO ADA TUTAWAJULISHA KADRI YATAKAVYOTUFIKIA


Kaka Michuzi Hali ilikua ni tete lakini ilikua ina sisimua kama Wanafunzi Na Askari wanaigiza filamu za action maana Askari wakienda Kushoto wanafunzi Wanaenda Kulia Wakija Kulia Tunaingia Kushoto Na Askari Tumewapiga Chenga Ya Mwili Na Tumewazidi Maarifa Wakati wenye wakiwa wamejiandaa asubuhi na mapema kuzuia Wanafunzi tusiingie mjini walikaa barabara kuu ambapo wanafunzi tuliingia na Mbinu za kiinteligensia Na Kupita njia za mikato ambapo waliambulia patupu kuja kushtuka wanaambiwa wanafunzi wameshafika nyerere square ilikua kama filamu hivi lakini kwa habari zaidi najua kuna kijana wetu ameshatupia mzigo na stori nzima ya habari hiyo ilivyokua unaweza bofya link hapo ukachungulia hapo
ReplyDeletehttp://josephatlukaza.blogspot.com/2011/06/just-in-udom-wawazidi-maarifa-askari.html