Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk Ali Mohamed Shein,akisalimiana na Madakatari kutoka China waliomaliza muda wao wa kazi hapa Nchini, walipofika kumuaga Rais Ikulu Mjini Zanzibar
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk Ali Mohamed Shein,akizungumza na kiongozi wa Ujumbe wa Madakatari kutoka China waliomaliza muda wao wa kazi hapa Nchini, Dkt. Xiang Jim,(kushoto) na Balozi Mdogo wa Cina anayeishi Zanzibar Mh. Chen Yiman, walipofika kumuaga Rais Ikulu Mjini Zanzibar
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk Ali Mohamed Shein,(katikati)akiwa katika picha ya pamoja na madaktari wa kichina waliomaliza muda wao wa kazi hapa nchini,walipofika kumuaga Rais Ikulu Mjini Zanzibar.
Picha na mdau Ramadhan Othman wa Ikulu-Zanzibar
RAIS WA ZANZIBAR NA MWENYEKITI WA BARAZA LA MAPINDUZI DK ALI MOHD SHEIN AMESEMA HUDUMA ZILIZOTOLEWA NA MADAKTARI KUTOKA CHINA ZIMECHANGIA JUHUDI ZA SERIKALI KUIMARISHA SEKTA YA AFYA NCHINI.
AKIZUNGUMZA WAKATI WA KUWAAGA MADAKTARI KUTOKA CHINA AMBAO WAMEMALIZA MUDA WAO WA KAZI NCHINI AMESEMA HATUA HIYO IMEWEZA KUUNGA MKONO JUHUDI ZA SERIKALI KUIMARISHA SEKTA YA AFYA UNGUJA NA PEMBA AMBAPO TAYARI HATUA KUBWA YA MAFANIKIO IMEFIKIWA.
AMESEMA WANANCHI WA ZANZIBAR PAMOJA NA SERIKALI WAMEFARIJIKA KWA KIASI KIKUBWA KUTOKANA NA KUWEPO MADAKTARI HAO KWA KIPINDI CHOTE AMBACHO WAMEWEZA KUTOA HUDUMA KIKAMILIFU.
AMESEMA LICHA YA CHANGAMOTO MBALI MBALI LAKINI MADAKTARI HAO WAMEWEZAKUFANYA KAZI ZAO KWA UFANISI MKUBWA NA KUWEZA KUHUDUMIA WANANCHI WA ZANZIBAR AMBAOA NAO WAMEKIRI UBORA WA HUDUMA WANAZOZITOA.
DK SHEIN AMESEMA SERIKALI IMEAMUA KUTEKELEZA KWA VITENDO SERA YA AFYA KWA KUWASHIRIKISHA WANANCHI AMBAPO MIONGONI MWA HATUA HIZO NI PAMOJA NA KUIMARISHA HOSPITALI YA MNAZI MMOJA KWA KUIPATIA VIFAA VYA KISASA NA WATAALAMU ILI IFIKIE HADHI YA HOSPITALI YA RUFAA NA KUZIIMARISHA HOSPITALI ZA ABDALLA MZEE NA WETE ILI ZIWEZE KUFIKIA ZA MKOA .
AIDHA AMESEMA SERIKALI INA MPANGO WA KUANZISHA KITENGO CHA KUSHUGHULIKIA MARADHI YANAYOTOKANA NA MATATIZO YA FIGO, MOYO,SARATANI NA HUDUMA NYENGINE.
NAE KIONGOZI WA MADAKTARI HAO ZHU XIANGJU AMESHUKURU SERIKALI PAMOJA NA WANANCHI WA ZANZIBAR KWA KUWAPA USHIRIKIANO KWA KIPINDI CHOTE WALICHOFANYA KAZI NCHINI.
AMESEMA WANAIMANI ZANZIBAR ITAENDELEA KUPATA MAFANIKIO ZAIDI KATIKA SEKTA YA AFYA KUTOKANA NA JUHUDI KUBWA ZINAZOFANYWA NA SERIKALI NA KUELEZA KUWA TIMU NYENGINE ZA MADAKTARI KUTOKA CHINA IKO NJIANI KUWASILI ZANZIBAR.
AIDHA MADAKTARI HAO WALIKABIDHIWA MEDALI NA NAIBU WAZIRI WA AFYA MHE DK SIRA UBWA MAMBOYA KAMA TUNZO YA UTENDAJI MZURI WA KAZI ZAO.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...