Waziri wa Afya wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar,Juma Duni Haji
Na Hamad Hija - Maelezo Zanzibar.

Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, kupitia wizara ya Afya imefungua zahanati 130 kwa Unguja na Pemba kwa lengo la kupunguza vifo vya wanawake na watoto.

Hayo yamesemwa na Waziri wa Afya Juma Duni Haji wakati akizindua toleo la nne la kitabu cha Ukweli kuhusu maisha katika Hoteli ya Bwawani mjini Zanzibar leo.

Amesema kila wilaya wamefungua zahanati tano kwa ajili ya kuimarisha huduma za mama na mtoto ambapo takwimu zinaeleza kwamba takribani wanawake 1,500 wenye umri wa kuzaa pamoja na wasichana, hupoteza maisha kila siku kutokana na matiatizo ya ujauzito na kujifungua.

Aidha amesema kiasi cha watoto milioni tatu duniani huzaliwa wakiwa wameshafariki na kiasi cha milioni 3.7 hufariki kabla ya kutimiza mwezi ambapo hufariki mara tu wanapozaliwa.

Kupitia shirika la kuhudumia watoto ulimwenguni UNICEF hapa Zanzibar katika kupambana na tatizo la vifo vya mama na watoto, limefanya kazi na juhudi kubwa ya kuandaa kitabu cha ukweli huhusu misha chenye dhana nzima ya kukinga vifo hivyo kupitia elimu ya afya kwa jamii.

Kitabu cha ukweli kuhusu maisha nikitabu chenye muongozo kamili, ambao utatumika katika kuelimsha jamii na familia kuhusu malezi bora ya watoto,kutoa taarifa muhimu, ushauri kuhusu ujauzito, uzazi salama , magonjwa ya watoto na jinsi ya kuwahudumia watoto kulinda afya zao.

Nae mwakilishi wa UNICEF Bi Dorothy Rozga aliongelea umuhimu wa kutoa elimu ya vitendo ambayo watu wote wana haki ya kufahamu na kuifanyia kazi.ambayo itawawezesha walezi na wabeba majukumu wengine kujifunza mbinu za afya na maamuzi yaliyo sahihi .

Aidha alisema kitabu ambacho kimezinduliwa cha toleo la nne cha ukweli kuhusu maisha kina ujumbe mbali mbali unaozungumzia masuala ya chanjo kwa watoto kabla ya kufikisha umri wa mwaka mmoja, unyonyeshaji maziwa ya mama kwa miezi sita ya mwanzo , malezi kwa watoto wachanga ,umuhimu wa wanawake kujifungulia katika vituo vya afya ili kupata huduma kutoka kwa wataalamu wa afya.

Kitabu cha ukweli kuhusu maisha ni makala ya Umoja wa Mataifa inayoongoza katika uhamasishaji wa afya ya msingi ambacho kimesambazwa duniani kote na kimechapishwa kwa lugha 215 kuanzia toleo lake la mwanzo mwaka 1989.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. AnonymousJune 02, 2011

    uzinduzi ulifanyikwa kwa shangwe na mbwembwe ila machapisho yenyewe hayakuwepo ukumbini, what a dissaopintment!!!!
    Mdau

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...